Mtoto wa miezi minne aliyezaliwa kwenye hospitali teule wilayani Muheza,
amekuwa gumzo na kustaajabisha wakazi wa mji huo, wakiwamo wazazi wake,
kutokana na kuzungumza akiwa na umri huo.
Mtoto huyo aliyezaliwa
Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na
kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa
na mtu yeyote akitaka kumsalimia.
Akizungumza mama wa mtoto huyo
Bi Rosemary Mhina , mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai
kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi
saba, alikuwa akilia tumboni.
"Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo
lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma,
utamsikia mtoto analia timboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule,
nikaja huku Bombo na Tumaini, nilipopigwa 'ultra sound' madaktari
wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa
kifaa hicho," alisema Bi Rosemary Mhina.
Akielezea zaidi kuhusu
namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo
alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa alipofikisha miezi miwili, siku moja
alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupe
maziwa"
Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka
maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na
mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si
mazuri mama nakuonea huruma"
Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya
kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume(Jina limehifadhiwa) ambaye amedai
kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru Arusha, alimpa
sh.30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi
sita.
"Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa,
hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto
wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu",
alidai Rosemary.
Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe
naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza
kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini
kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko.
"Kipindi
kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala
wakaniparua huku mwanangu Upendo akinicheka", alidai.
Mambo makubwa hayo je ingekuwa wewe ungefanyaje?