Pages

Saturday, 16 August 2014

Lampard atangaza kuachana na klabu yake ya Chelsea wakati mkataba wake utakapotamatika

  
Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard
Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Kiungo mkongwe wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard ametangaza kuwa ataachana na klabu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake unaotarajiwa kutamatika mwezi June mwaka huu.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema ku

Tuesday, 12 August 2014

je wajua? Kampuni ya China yajipanga kujenga ghorofa refu kuliko yote duniani kwa muda wa siku 90 tu.


Kampuni moja nchini China inajiandaa kufanya ujenzi wa ghorofa refu kuliko yote duniani kwa muda wa siku 90 tu.
Kuanzia ujenzi wa msingi hadi kufikia juu, ujenzi mzima utafanyika ndani ya miezi mitatu kwa kiwango cha ghorofa tano kwa siku.
Ujenzi huo ni changamoto ambayo China pekee ndio inaweza kuifanya na kuwa ghorofa hilo litajengwa katika mji ambao watu wengi hawaufahamu wa Cha

Sunday, 10 August 2014

je wajua kazi ya tangawizi?

TANGAWIZI ni chakula cha asili chenye uwezo wa kupambana na ugonjwa wa kichefuchefu na kutapika. Uwezo huu hutokana na vitamin B6 iliyopo kwa kiasi kikubwa katika tangawizi ambayo ni maarufu duniani kote kwa matumizi kama kiungo ‘spice’ kwa vyakula vingine.

Vitamin B6 iligunduliwa mwaka 1934 na Dr. Paul Gyorgy huko Hungary na akabainisha wazi kuwa ml.100 za B6 ni dozi tosha kwa siku kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 19 hadi 70 katika kupambana na kichefuchefu na hata kuzuia kutapika pia.
Tangawizi licha ya kuwa na uwezo wa kumaliza tatizo hili, bado imegundulika kuwa na uwezo tena wa kukinga maradhi ya uvimbe ndani ya mwili wa binadamu ambao husababisha wengi kupatwa na maradhi ya saratani za aina tofauti tokana na uvimbe huo.
Hata hivyo, ukiwa unatumia tangawizi katika kila mlo wako kwa muda mfupi tu utajikuta maumivu ya mgongo, kiuno, maungio ya miguu na mikono yamepungua na kama siyo kuisha kabisa. Hii ndiyo kazi halisi ya tangawizi duniani na leo ni fursa kwak
Kuna jamaa mmoja alikuwa kila siku usiku akilala anaota NGEDERE na PANYA wanacheza mpira ikabidi siku moja aende hospital kumuona dokta alipofika hospital mazungumzo yakawa hivi:-
JAMAA: "Dokta mimi nimekuja ninasumbuliwa na ndoto kila siku usiku nikilala naota Ngedere na Panya wanacheza mpira utanisaidiaje?"
DOKTA: "Kwa hilo tatizo lako ulilosema inabidi nikupe hizi dawa ukifika nyumbani uzimeze, ukizimeza kuanzia leo hauto ota tena ndoto hizo sawa!"
JAMAA: "Sawa dokta ila itabidi nianze kuzimeza kesho kwakuwa leo ndio Fainali nataka nijue nani atashinda katika mechi ya leo"
- Dokta alibaki anashangaa!


Dir Kuna mgonjwa mmoja alikwenda hospitali kupimwa alipopimwa na dokta akagundulika anaumwa ugonjwa wa kiharusi mambo yakawa hivi:-
DOKTA: "Nimekupima nimekukuta unaumwa Kiharusi"
MGONJWA: "Ni kweli dokta ndio mana nilikuwa nina hamu sana ya kutaka kuoa! Kumbe naumwa kiharusi"
- Dokta alibaki anashangaa!
Dir - Kuna Teja mmoja alikuwa amelala chini katika kituo cha Mabasi wananchi kibao wakamzunguka kumuangalia na kila mmoja akaanza kujiuliza kwanini kalala pale chini? Kila mwananchi akaanza kutoa maoni yake:-
MWANANCHI 1: "Jamani huyu atakuwa anaumwa, tumpelekeni kwanza hospital"
MWANANCHI 2: "Mimi ninachoona tumpelekeni kwanza Polisi"
Ghafla ikasikika sauti ya Bibi mmoja akisema:-
BIBI: "Sikilizeni jamani Pengine ananjaa huyu hajala hebu mtu mmoja aende akamnunulie chips na soda ale"
Baada ya yule Bibi kusema vile mara yule mteja akainua kichwa na kusema:-
TEJA: "Jamani msikilizeni Bibi anavyosema"
Wananchi wote waliokuwa wamemzunguka wakaangusha kicheko mmoja wao akasikika akisema "KUMBE JAMAA ALIKUWA ANANJAA KISHAVUTA MI UNGA YAKE SASA UBAO UNAMCHARAZA" hahahaaaa!
Dir kuna wanandoa wawili walikuwa wanaish nyumba moja lakini walikuwa wanaugomvi wakawa hawaelewani ndan ya nyumba yao mpaka wakafikia hatua ya kuwekeana mipaka chumbani ikawa kati yao kama kuna mmoja anashida na mwenzake anamuandikia mwenzie ktk karatasi walikuwa hawaongei. Sasa siku moja usiku mwanaume alikuwa anasafar kesho yake asubuh mapema akamwambia mke wake amuamshe asubuh mapema saa12, wakalala ilipofika asubuh sa12 yule mwanamke akaamka akachukua karatasi akamuandikia "mume wangu amka sa12 imeshafika" halaf akarud kulala yule mwanaume akaamka baadae akamwambia "Mke wangu mbona hukuniamsha?" mwanamke akasema huoni nimekuandikia ktk hilo karatasi. BASI TOKEA HAPO WAKAANZA KUONGEA

Dir - kuna hospital moja ya vichaa ilikuwa imeishiwa dawa za kuwapima vichaa akili zao kama wamepona, ikabidi doctor achore alama ya mlango ukutani halaf akawaambia wale vichaa "ATAKAE WEZA KUPITA HAPA AKAONDOKA HUYO ATAKUWA AMEPONA ANARUHUSIWA KWENDA NYUMBANI" basi wale vchaa wote walivyosikia vile wakaanza kugombania kupita ktk ule mchoro, kuna kichaa m1 yeye hakwenda kugombania akabaki anawatizama pemben huku anawacheka wenzie yule Dokta akajua pengine huyu kishapona akamuuliza "WE UNACHEKA NINI?" akamjibu dokta "NAWASHANGAA HAO WANAGOMBANIA KUTOKA NJE WAKATI FUNGUO NINAYO MIMI".
 
 
 

cheka uongeze siku za kuishi

mwizi aliyependa kutubu

 
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha,kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

"Padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

"Endelea...."
...
...

"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kuitisha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"Utasamehewa... "

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake.Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"

"Utasamehewa... "

Utani na mwanajeshi wamtokea puani

 

NewsImages/6615934.jpg

Wednesday, October 03, 2012 11:33 AM
MKAZI WA Mbagala Mission , Omari Nundo anaugulia maumivu akiwa kitandani hoi kwa kichapo alichokipata kutoka kwa jirani yake baada ya kumtania
Nundo ambaye amefika zahanati ya karibu kupata matibabu sasa anaendelea kuuguza maumivu baada ya kichapo hicho ambacho hakukitegemea kutoka kwa jirani yake huyo

Akiongea kwa masikitiko leo asubuhi, Nundo alibainisha kuwa, alipata kipigo hicho jana kutoka kwa jirani yake ambaye wanaishi nyumba za jirani ambaye hakutaja jina lake

Amesema kuwa, yeye na jirani yake walikuwa katika hali ya kutaniana kama ilivyo kawaida yao wanavyofanya lakini alishangazwa na kuona jirani yake huyo akianza kumpa kichapo cha nguvu na hatimaye kumpa maumivu yaliyomfikisha hospitalini kupata matibabu

Amedai kuwa kwa kawaida yeye na jirani yake huyo huwa wanataniana utani wa jadi ambapo kwa kawaida Tanzania kunakuwa na utani wa makabila kabila fulani hutaniana na kabila Fulani ambapo utani huo ulikuwepo tokea enzi za mababu zetu ndio walioturithisha

Amedai yeye ni myao kutoka kusini na jirani yake huyo ni Mngoni kutoka Ruvuma hivyo kiasili huwa ni watani wa jadi na huwa wanataniana mara kwa mara

Amebainisha kuwa, jirani yake huyo ni mwanajeshi, hivyo siku hiyo walianza kutaniana na yeye ndipo akamwambia “Mtani unaacha mke wako uliyejenga naye nyumba, unakwenda kuoa mwanamke mwingine huoni kama kitu kibaya hicho?

“Mke wako uliyehangaika nae kujenga nae hicho kibanda unamuacha unadanganyika na huyo mwanamke sio vizuri mtani” amebainisha jinsi utani huo ulivyokuwa

Mara baada ya kumaliza hayo jirani yake huyo ambaye kazi yake ni mwanajeshi aliona kama ameguswa na ghafla alianza kumpa kichapo mtani wake huyo bila huruma kwa kuona anaambiwa ukweli na siku zote ukweli huwa unauma

Hivyo Nundo alishindwa kujitetea na alipokea kipigo hicho cha nguvu sababu hakuweza kujitetea kwa kuwa jirani yake huyo alikuwa akimpiga kwa tikiniki za kijeshi

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumuhoji amebainisha kuwa, ni kweli mwanajeshi huyo ameacha mke wake na hivi sasa anatangaza ndoa na mwanamke mwingine

Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa hadi imepeleka Omari kuwa kitandani hoi kwa kipigo alichopata kutoka kwa jirani yake huyo ambacho hajakitarajia

Hata hivyo Nundo amesema hapo umeshaingia uhasama “na kama laiti mmoja wetu amepanga angehama lakini mbaya zaidi kila mtu amejenga mahali hapo, sijui wataishi vipi’ alijihoji mwenyewe



like page yetu

PICHAZ..MAAJABU MAKUBWA..MTO WENYE MAJI YA DAMU WATIKISA DUNIA....!



Njaa sio mchezo hona hii.!!!!!!!


Photo: HUU NI UCHU AU LAANA TOKA KWA MUNGU ?


liklike page yetue page yetu

Wanasayansa kweli wana visa.

Wiki hii wamekuja na utafiti wa ajabu. lakini utafiti wenye manufaa kwa wengi.

Watu wengi, sio wanawake wala wanaume huwa na matatizo ya unyumba lakini hawasemi. Hujitangazia ushujaa wa urongo. Utamsikia mtu akisema mimi? Wee...kube wapi Bure kabisa.

Lakini wanasayansi wa uingereza wamegundua kwamba kuna njia rahisi na eti ya kuaminika bola mtu kutumia madawa ya kusisimua ashiki.

Wanasayansi hao wa shirika la Retailer Littlewoods wanasema siri ya ubingwa kitandani unategemea bed shiti

Hiki ndicho wanachokitaka mashabiki wa YANGA


 LIKE PAGE YETU HAPA
 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets