Pages

Tuesday, 30 December 2014

Jamaa mmoja alienda kuposa kwa mzee mmoja

Mzee: Yaani wewe umekuja kuposa huku unatafuna big G? Si dharau hiyo!  
Jamaa: Natoa harufu ya sigara.  
Mzee: Unasemaje? Unavuta sigara pia!?  
Jamaa: Nikitoka klabu kulewa ndo huwa navuta. Mzee: Tobaa! Unalewa!?  
Jamaa: Nilianza kulewa nilipokuwa jela.  
Mzee: Yaani na kufungwa pia umeshawahi!?  
Jamaa: Ah si niliua mtu.
Mzee: Duh kumbe wewe muuaji!? Astaghafillulah. Jamaa: Si kuna mzee mmoja bwege nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, mimi nikamuulia mbali.
Mzee: Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, mke tu umepata! Mkeo huyu hapa baba! 

Jamaa mmoja aliyekuwa kichaa si alionekana kapona akaruhusiwa kutoka hospitali:

Madaktari wakamchukua katika gari la wagonjwa hadi mtaani kwake kisha wakasimamisha gari karibu na nyumbani kwake na kuulizwa, 
“unapakumbuka kwako?” 
Akajibu “Ndio napakumbuka nyumba yangu ilee”, 
Wakatoka wanafunzi wawili katika ile nyumba wamevaa sare za shule, jamaa akasema,
“Wanangu walee wanatoka wanaenda shule”, 
Mara akatoka mwanamke kabeba kikapu, jamaa akasema,
“Na mke wangu yulee anatoka anaenda sokoni”, Ghafla akatoka mwanamume kavaa tai na kabeba brifkesi, jamaa akasema,
“Enhee! na mimi yulee naenda kazini!”

Mama kapanda daladala na mwanae wa miaka miwili, akataka kumnyonyesha, pembeni kakaa na njemba moja:

Mama: Nyonya basi mwanangu
Mtoto: (Anatingisha mabega kumaanisha hataki)
Mama: Au nimpe anko
Mtoto: (Analia) sitaki (anadaka nyonyo anaendelea). 

Punde akaacha tena kunyonya
Mama: Nitampa anko kama hautaki
Mama: Nimpe
Njemba: ahaaaa mama kuwa na msimamo basi nshapitiliza vituo vitatu kama unanipa nipe au kama vipi nishuke kituo kinachofuata
Mama: Heeeh?

UMESIKIA MAAJABU YA PANYA HAWA


Umesikia maajabu ya panya hawa?
Panya hao waliogunduliwa/fundishwa chini Tanzania katika chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro wana uwezo wa ajabu.

Panya hao wana uwezo wa kugundua mabomu yaliyotegwa aridhini, pia panya hao wana uwezo wa kugundua vimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu kupitia koozi la mgonjwa. 

JE WAJUA HILI :VUVUZELA NDANI YA KAMUSI YA OXFORD?

Kamusi maarufu ya kiingereza ya Oxford imeliingiza jina la Vuvuzela katika kamusi yake ya kiingereza na kuanza kutumika katika lugha hiyo. Vuvuzela ni kati ya maneno 2,000 mapya ambayo yameingizwa katika kamusi hiyo. Vuvuzela ni tarumbeta la plastiki na lilipata umaarufu sana duniani wakati wa fainali za soka za kombe la dunia zilizofanyika nchini Afrika Kusini mwaka huu.
LIKE PAGE YETU HAPA

HAPA NDIO KWA MWALIMU NYERERE

Hapa ndipo nyumbani kwa baba wa Taifa Hayati Mwalimu JK Nyerere, nyumba ya mwalimu ipo Butiama mkoa wa Mara na ndipo  alipozikiwa. Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na alikuwa kiongozi wa mfano Afrika na Duniani kwa kuwa kiongozi muadilifu.
fahamu zaidi kwa kulike hapa

Je wajua kuhusiana na kipepeo?


Unajua kwamba miguu ya mdudu kipepeo ina uwezo wa kutambua aina ya chakula? Mdudu huyu mwenye uwezo wa kuluka, chakula chake kikuu ni maua. Miguu yake ina uwezo wa ajabu katika kutambua wa aina ya chakula. Mdudu huyo ana uwezo wa kutambua aina ya chakula kwa kutumia miguu yake miwili ya mbele. Kipepeo huwa ana miguu sita.

Monday, 29 December 2014

Kichekesho cha Mlevi na Mchungaji Kanisani

Waumini waliambiwa watoe michango ili wazungushie ukuta eneo la makaburi.
Mchungaji akauliza kuna mtu ana swali?
Mlevi akauliza “Je kuna Marehemu yoyote aliyewahi kutoroka? Kama hakuna, ukuta wa nini sasa? Au ndio ufisadi hadi kwenye makaburi…?
Mchungaji kimyaaaaa!

Vichekesho kati ya mume na mke kanisani

Vichekesho kati ya mume na mke kanisani Je unajua vichekesho kanisani? ulishasikia mojawapo, hebu fuatilia hii hapa.
Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar es salaam. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole.  Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia kanisani kusali. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,

Mtoto wa Miezi Tisa Ashitakiwa Kwa Jaribio la Mauaji Pakistani

Mtoto wa Miezi Tisa Ashitakiwa Kwa Jaribio la Mauaji Pakistani
Mtoto wa miezi tosa (9) mafichoni kule LAHORE Pakistan kwa sababu ana kesi ya kujibu. Mtoto huyo pichani ambaye hata hawezi kunyanyua chupa yake ya maziwa anadaiwa kushiriki kwenye jaribio la mauaji.
Baby huyo anayeitwa Musa Khan sasa yuko mafichoni kwani polisi wanamtafuta. Wiki iliyopita mtoto huyo alipelekwa mahakamani na kutajiwa kesi hiyo ya jaribio la mauaji katika mojawapo ya mahakama mjini LAHORE.
Pamoja na mtoto huyo Baba yake na Babu yake wanahukumiwa pia. Sakata hilo lilianza pale polisi mmoja na mfanyakazi wa kampuni moja ya gesi aliyekuwa anakusanya bili za muda mrefu waliporushiwa mawe na waandamanaji wanaopinga kupunguzwa kwa gesi na kupandishwa bei.
Kesi ya kichanga hiki inaonyesha wazi udhaifu ulioko kwenye sheria za PAkistani
Hata hivyo taarifa za hivi punde kutoka LAHORE, Pakistani zinasema kuwa mahakama hiyo imemfutia kesi mtoto huyo..
like page yetu kwa taarifa zaidi
 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets