Pages

Monday 16 February 2015

Friday 13 February 2015

Tazama picha za mtu mrefu zaidi na mtu mfupi zaidi Duniani walipokutana kwa mara ya Kwanza.

Tall III
Tumekuwa tukisikia rekodi mbalimbali zikivunjwa na watu duniani na rekodi hizo maalumu huwa zinatunzwa katika kitabu cha kumbukumbu cha Guiness World Records.

Thursday 5 February 2015

TUVUNJE MBAVU KIDOGO NA VITUKO VYA USWAHILINI.

KATIKA hali isiyotarajiwa na wengi, juzikati abiria mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mkazi wa jijini Dar es Salaam alilazimika kuendesha daladala baada ya trafiki kumtia nguvuni dereva.
Ilikuwa asubuhi wakati daladala hilo lilipoanza safari yake Kituo cha Gongo la Mboto kwenda Sinza, kondakta wake aliendelea kuita abiria kwa muda mrefu licha gari hilo kuwa ‘nyomi’.
Wakati abiria wakimtaka kondakta huyo kuruhusu gari kuondoka, aliwajibu kwa kebehi kwamba daladala huwa halijai inayojaa ni ndoo ya maji.

Baada ya muda kondakta alimruhusu dereva kuendesha gari, bila kuchelewa lilianza kushika kasi na abiria wakawa na matagemeo ya kuwahi makazini mwao.
Basi hilo lililopofika Kituo cha Mombasa, Ukonga askari wa usalama barabarani aliona jinsi abiria walivyokuwa wakining’inia mlangoni, akalisimamisha.
Askari alimtaka dereva kutoa faini ya shilingili 20,000 lakini suka alisema hakuwa na kiasi hicho kwani ndiyo kwanza walianza kazi.

Dereva: Naomba unisamehe afande nakiri nimefanya kosa, kwani ndiyo kwanza naamka hivyo sina kitu kabisa.
Askari: Kama ulilijua hilo kwa nini unaendesha gari huku abiria wakiwa wananing’inia?

Mabishano yalikuwa marefu na kuwafanya abiria kuanza kupiga kelele za kumtaka dereva kuwapeleka kwani walikuwa wakichelewa kazini.
Baada ya kelele nyingi zisizo na majibu, abiria mmoja aliamua kwenda kukaa kwenye usukani na kuanza kuliendesha daladala ambalo dereva alikuwa ameliacha katika ‘sailensi’.
Abiria waliaanza kushangilia kwa kitendo hicho, dereva alianza kulikimbilia gari hilo na kumuacha askari akiwa ameduwaa asijue la kufanya.

Dereva alikodi pikipiki na kuanza kulifukuzia daladala hilo na kufanikiwa kulikuta kwenye foleni maeneo ya Vingunguti.
Dereva alianza kumfokea abiria aliyekuwa akiliendesha gari hilo bila ruhusa yake lakini abiria walionekana kuwa upande wa abira mwenzao kwa kumshambulia dereva.
like page yetu kwa vituko zaidi

Monday 2 February 2015

MAAJABU YA DUNIA;ANGALIA PICHA YA MZEE AMBAYE HAJAOGA WA KUNAWA KWA MDA WA MIAKA 37!


UKIWA KAMA MSOMAJI WA BLOG HII UNASEMAJE KUHUSIANA NA SWALA KAMA HIL...

JE, WEWE NI MTUMIAJI WA SMARTPHONES? JIELIMISHE KWA KIFUPI KUHUSU HIZI BIDHAA.

Smartphones ni aina ya simu zinazojizolea idadi kubwa ya watumiaji siku hadi siku hapa kwetu Tanzania.
Watumiaji wengi hufurahishwa na jinsi zinavyofanya kazi kwa ustadi na mbwe mbwe nyingi.

HIVI UNAYAFAHAMU MAJANGA KUMI YA ASILI YANAYOONGOZA KWA KUUA WATU KATIKA MUDA MFUPI? SOMA KWA UFUPI UPATE KUJUA YANAVYOTOKEA.

Majanga ya asili(Natural Disasters) ni matukio yanayotokea kwa wingi duniani hutumia muda mfupi lakini madhara yake huwa ni makubwa.
Katika muda mfupi yanayotumia huondoa maisha na kujeruhi watu pamoja na uharibu wa mali.
Majanga haya huwa hayana eneo maalumu popote yanaweza kutokea japo kuna baadhi ya maeneo huwa ni mara kwa mara yanajirudia.
 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets