1. Je, wajua
kwamba binadamu pamoja na akili zake zote, pamoja na mbwembwe zake
nyingi, bado hana uwezo wa kufikisha ulimi kwenye kiwiko cha mkono wake?
2. Je, wajua kwamba kama piza zinazoliwa
kwenye bara la Amerika kwa siku zingepangwa zingeweza kuchukua eneo
lenye ukubwa wa hekta 18?
3. Je, wajua kwamba kila binadamu ana
alama tofauti kabisa na za kipekee katika ulimi wake (tongue-prints)
kama zilivyo za vidole?
4. Je, wajua kuwa mnyama aina ya mamba huwa hana uwezo wa kutoa ulimi wake nje kutokana na maumbile yake?
5. Je, wajua kuwa farasi na panya ndio wanyama pekee wasiotapika?
6. Je, wajua kuwa jicho la mbuni ni kubwa kuliko ubongo wake?
7. Je, wajua kuwa licha ya binadamu kuwa na uwezo wa kubana pumzi zake, bado hawezi kujiua kwa njia hiyo?
8. Je, wajua kwamba kwa wastani kichwa
cha mwanadamu hubeba nywele zipatazo 100,000 na kila unywele unakua kwa
wastani wa sentimita 12.5 kwa mwaka?
9. Je, wajua kuwa siafu ndio viumbe pekee wasiolala maisha yao yote?
10. Je, wajua kwamba mwanadamu ambaye
anaweza kuishi kwa wastani wa miaka kati ya 50-60, anaweza kuzalisha
kiasi cha mate kinachofikia galoni 10,000?
Je, wajua kuwa mwili wa mwanadamu una kiwango cha mafuta chenye kuweza kuzalisha miche saba ya sabuni?
11. Je, wajua kuwa katika ngozi ya
mwanadamu mmoja pekee kuna idadi kubwa ya viumbe hai kuliko idadi ya
wanadamu wote walioko katika ulimwengu mzima?
12. Je, wajua kuwa kama mdomo wako ukiwa mkavu kabisa huwezi kutofautisha ladha mbalimbali?
13. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu hutumia zaidi ya asilimia 25 ya oksijeni yote inayotumiwa na mwanadamu?
14. Je, wajua kuwa kila dakika moja
inayopita, kuna seli kati ya alfu 30 hadi 40 zilizokufa zinazodondoka
toka katika mwili wa mwanadamu?
15. Je, wajua kuwa ubongo wa mwanadamu umeumbwa kwa maji kwa kiwango cha asilimia 80?
16. Je, wajua kuwa kati ya viumbe wote duniani, ni mwanadamu pekee ambaye anaweza kulala kwa kutumia mgongo wake?
17. Je, wajua kuwa ukubwa wa jicho la
mwanadamu daima ni ule ule toka anapozaliwa hadi anapozeeka? Pua na
masikio hukua kwa kadiri mwanadamu anavyozidi kukua.
18. Je, wajua kuwa paka ana uwezo wa
kubadili sauti yake na kufanya milio zaidi ya 100 tofauti tofauti wakati
mbwa ana uwezo wa kufanya hivyo na kutoa sauti kumi tu?
19. Je, wajua kuwa visiwa vya Hawaii huvisogelea vile vya Japan kwa umbali wa inchi 4 kila mwaka?
20. Je, unajua kuwa kutengeneza karatasi
mpya kutokana na karatasi za zamani zilizoisha matumizi yake kunaweza
kusaidia kupunguza matumizi ya nishati kwa asilimia takriban 70
kulinganisha na kutengeneza karatasi hizo kutokana na miti?
No comments:
Post a Comment