Habari wakuu,
Baada ya jana ripoti kusomwa, Kama kawaida moja kwa moja kutoka bungeni
Dodoma tutajuzana hapa kupitia habari clan. Kwa wale wasio na uwezo
kufatilia moja kwa moja pia kwa wale wenye nafasi ya kufatilia lakini
wakapenda kuona mirejesho fursa ambayo haipo kwenye vyombo vingine vya
habari. Tuungane kwa pamoja katika ngwe ya leo kutoka Dodoma.
Matatizo juu ya kukatika umeme yanazidi siku zinavyokwenda hivyo
usisahau kuweka chaji ya kutosha kwenye kifaa chako ili tuwe pamoja siku
ya leo.
KIKAO CHA BUNGE JIONI
Mwenyekiti: Wananchi wananchi wanataka kujua ukweli, na anatoa nasaha zake ili bunge lisilete fujo
Lissu: Anaomba radhi ya kauli ya jana kuhusu tuhuma ya wakili kumuua mkewe.
Escrow: Muhongo kapotosha, viambatanisho haviwakilishi alivyosema.
Muhongo ameleta vitu viwili tofauti na ni upotoshaji mtupu. Pesa za
Escrow ni za umma au binafsi, Muhongo anasema ni za makampuni na PAC
inasema ni pesa za umma. Isingekuwa za umma amri ya kutolewa
zisigetolewa kwa ushauri wa mwanasheria mkuu wa serikali.
Benno Ndulu asingesema siwezi kutoa bila ridhaa ya waziri mkuu na raisi,
pesa za binafsi iweje zitolewe kwa mlolongo wa mawaziri,
Ili PAP wapate pesa ilikuwa lazima wapate ridhaa ya Muhongo lakini hawajapa.
Nyaraka zinathibitisha mgao wa hizi fedha, zimepelekwa benki binafsi na
ndani ya siku moja baadhi ya watendaji wa serikali wamelipwa.
Mgao wa fedha za Escrow kwa maafisa wa umma, maaskofu na wabunge ndani ya siku 1 (bilioni 78); ni pesa za umma.
Mpaka majaji wamehongwa milioni 400 eti michango ya harusi!
Hizi fedha ni fedha za wananchi wa nchi hii! Kuna ushahidi wa kutosha katika ripoti ya PAC (TRA, CAG wamekiri)
Lazima watu wawajibike! Hizi ni fedha za Umma
Kumwondoa rahisi ni vigumu kidogo. Tuanze na Waziri Mkuu, Muhongo, Tibaijuka, Werema na majizi yote! Hawa tunawaweza
Mahakama zetu katika hili hazina mamlaka ktk kesi hii ya IPTL
Kwa ushahidi huu, ni ngumu kuwaamini majaji wetu na mahakama zetu
Kuna mawasiliano lukuki kati ya Ofisi za Umma katika utoaji wa fedha za Escrow. Haziwezi kuwa fedha binafsi
Fedha hazikutakiwa kutolewa na benki na haiwezi kufundishwa kazi na
mwanasheria mkuu, Chombo pekee cha kutoa ushauri wa kodi ni TRA na sio
mwanasheria mkuu na katibu mkuu wa fedha hawezi kujificha nyuma ya
kivuli cha ushauri wa mwanasheria mkuu.
Waliokuwa na mamlaka hawakufanya hivyo lazima wawajibike.
Waziri mkuu anatakiwa awajibike kwa sababu alikua anafahamu juu ya hili
swali, na barua zote zilinakiliwa kwa waziri mkuu, ni kiongezi
anaeshughulikia shughuli za kila siku za serikali.
Usalama wa taifa na financial inteligence unit chini ya wizara ya fedha hawakutimiza wajibu wao nao hatuwezi kuwaacha.
Waziri wa nchi ofisi ya Raisi(Marry Nagu) amesimama kuelezea
kutajwa raisi katika kashfa, anaomba watu wajadili kwa ustaarabu kufika
maamuzi pia kutotumia majina ya majaji.
Mwenyekiti amesimama na kusema anakubaliana nae pia anaomba watu wasitumie vijembe
Lissu: Anakana kutumia jina la raisi kwa dhihaka, na anarudia
aliyoyasema. Wazuri kupewa hongo ni jambo baya, pia mwanasheria mkuu wa
zamani kupewa hongo pia viongozi wa dini na inafedhehesha taifa. Hakimu
kupewa milioni 400 na kampuni ambayo ilikua mahakamani 20. Jambo baya
fedha za serikali kuibiwa. (Anataka kuongolea Mkono Adv lakini kengele
inagonga na kukaa chini)
Mwijage: Naijua IPTL tangu inaanza na imekua ni tatizo, hiki
kibuyu kilianza kula njiwa mpaka kula mbuzi kama alivyonisimulia bibi
yangu, IPTL imekua jini, badala ya kuhamaki tutafute njia ya kuondokana
nahiki kibuyu.
Tatizo mojawapo wa IPTL ni capacity charge kama nilivyoona kwenye hukumu
ya IPTL, Wananchi wamechanganyikiwa na kila unachomwambia kama madawa
na madawati anakwambia Escrow. Nakubaliana na PAC ilatudadavue wote
tutoke na maazimio ya pamoja.
Kingwangala anaomba taarifa: Taarifa kwa mchangiaji, PAC imefanyia kazi
ya CAG, hivyo findings za PAC zinatokana na CAG. Hivyo wachingiaji
wasinukuu sana taarifa PAC badala yake watumie taarifa ya CAG.
Mwijage anaendelea
Naomba wananchi waambiwe ukweli, watu wanapendekeza tubinafsishe mtambo
wa IPTL lakini tuwe waangalifu, tunaweza kujikuta tunabeba deni la
standard charted, hatuwezi kuingia ndoa na standard charted bank.
VAT, Ile pesa ya VAT, tunataka kujua mmedai kiasi gani.
Kuna watu wamechukua pesa, Rugemarira alisema tunalaliwa, Isiwe nongwa yeye kulipwa hizo pesa.
Nani aondoke, sioni tatizo kumsema waziri wa uingereza, hivyo
waziri Masele sidhani kama ana cha kuwajibishwa, sioni waziri mkuu
amehusika wapi. Kuna mtu ni halali, Mhongo ni dalali, huwezi kuwa waziri
wa umeme usikutane na mwekezaji wa Megawats 500. Tukaze pale
panapohusika, tumefika katika hatua mbaya.
Mohammed Chombo: Kama waliotangulia kusema, pia baada ya kupata
ripoti na ufafanuzi wa serikali, nami nichangie nililoliona, Escrow ni
account iliyofunguliwa baina ya watu wawili. Ilibidi ifunguliwe kwa
sababu ya kutoelewana kwa malipo yanayopaswa kulipwa.
Mwenyekiti(Zungu) anaomba order(utulivu wa bunge) kusikiliza anachoongea Chombo.
Chombo anaendelea
IPTL ni ushirika wa watu wawili na mmoja wao ni VIP na ikafika wakati
wakafungua kesi(anaendelea kuelezea historia ya IPTL na TANESCO),
Anatumia neno kuwakejeli wote wanaompinga/ kumpigia kelele
Fedha hizi sio mali ya umma bali ni mali ya IPTL, kama kuna pesa au kodi
ni lazima ilipwe na waliopata pesa hizo mfano VIP. Kwa fedha ambazo
zimebaki kwa PAP pia lazima zilipiwe kodi. Mimi sikupata pesa za IPTL.
Mwenyekiti(Zungu) anasema amemuona Lema anaropoka na anamkanya kama onyo la mwisho
Mheshimiwa nashukuru kwa kunipa nafasi(Amemaliza)
Mfutakamba: Usajili wa IPTL jukumu lake ni BRELA, anaepata hisa
hizo ni tax agent na anapaswa kwenda kulipa kodi, bilioni 30 ambazo
hazijalipwa kodi waende wakalipe kwasababu tunazihitaji.
Kama kuna mgao wa pesa umetolewa ni income hata kama ni zawadi lazima
walipe kodi, ningeshauri wale waliopata mgao walipe kodi. Ningependekeza
tujue hizi ni kesi za Britain zilikuwa ni kesi gani na kama PAP
alisajili Tanzania, bado naona utata kama PAP imesajiliwa Tanzania iweje
iwe kampuni fake.
Huu mradi ulikua gharama yake ilikuwa juu ya kawaida (overpriced), pesa
zilikua mali ya TANESCO lakini IPTL ilendelea kuzalisha umeme na bado
tunadaiwa. Kuna kampuni nyingi zinazalisha umeme hivyo tusije kuingizwa
mtego wa malengo ya kibiashara ya wazalisha umeme.
Nampongeza Muhongo na wizara yake kwa kutuletea umeme wa kutosha.
Tuangalie vielelezo vya PAC kama kuna watendaji katika utendaji wao kuna
hitilafu na sisi tuone.
Kuna wabunge wanatajwa kuwa wamepokea mgao, tuwape natural justice ya
kuwasikiliza. Tujue na wao sababu yao. Waliotajwa wapewe fursa wahojiwe.
Rugemarira amelipa kodi baada ya kulipwa. Waziri mkuu ni mchapakazi.
Makani: Nashukuru kwa fursa, tumeingia kwenye hoja inayohitaji
umakini mkubwa, ili tuweze kwenda vizuri lazima tumuweke Mungu mbele na
ili tumuweke mbele hatuwezi kuweka amabyo yanamuuzi kama uwongo. Hoja
inayonikira ni kuwa kuna fedha za serikali zilikuwa sehemu na baadae
ikaibwa na kuporwa. Wataalamu watusaidia kulingana na taaluma zao na kwa
kufuata maadili ya taaluma zao. Hoja kuu kama fedha ni za serikali ama
laa.
PAC wanakiri sio fedha zote za Escrow ni za umma, katika majibu ya CAG
hakuna mahali alipokiri kuwa fedha hizi ni za umma. TAKUKURU ilipohujiwa
na PAC amesema ni fedha za serikali japo hajakamilisha uchunguzi,
zingeweza kuwa fedha za serikali kama TANESCO wangerudi kwenye meza na
IPTL na majibu yakawa chanya, pili labda suala la kodi.
Si sahihi ukisema moja kwa moja kuwa ni fedha za serikali, majadiliano
kati ya TANESCO na IPTL, hata ukifanya mahesabu, pesa za escrow zote
zingezama katika deni la IPTL wanaloidai TANESCO.
Maoni yangu: Taarifa ya CAG ilikua na mapendekezo, yanatofautiana kwa kiasi kikubwa na PAC(Anataja mifano ya tofauti). NASHUKURU
ZITTO: Anaomba muongozo juu ya muongeaji aliyepita kuhusu CAG hakusema fedha za Escrow za nani.
Ndasa: Muhimili mmoja kuwa na mgogoro na mwingine haileti sifa
nzuri hivyo kila mtu aheshimu muhimili mwingine, wananchi wanaposikia
kuna wizi, tusipoeleza vizuri hata tukiongea vipi humu haitasaidia.
Wananchi wanataka kujua ni kweli hizi pesa zimeibiwa au zimelipwa. Umeme
lazima ulipiwe IPTL kwa sababu hamna cha bure pale. Bilioni 320
zimeibiwa au zimetumika kulipia umeme? Katika hizi 320 bilioni pia
ielezwe kodi ya serikali ni kiasi gani. Wakija mafundi wa kusema
wananchi wataaminishwa kuwa ni wizi hivyo serikali lazima iseme bila
kuficha na msiwe na kigugumizi.
Tunamuwajibisha waziri mkuu kwa kosa lipi, tutendeane haki, mtoto wa
mkulima amefanya nini? Pili wametajwa watendaje kama Muhongo na Masele,
kwenye haki tusiweke ushabiki kisa Muhongo amekutana na Rugemelira
pamoja na Singh.
Kumezuka mtindo wa kusingizia watu, nafsi ya mtu itamsuta,
tusisingiziane. Namshukuru Zitto ni msikivu, PAC ni kamati ya bunge,
tushirikiane tutoe mapendekezo ya pamoja.
Tuwe makini tunavyoenda, kuna mataifa ya nje kama tukiwapa moyo hawa
tutaanza kuuza umeme nje, kuna bomba la gesi limekamilika ndani ya mwaka
mmoja.
Kisangi: Asante, nimpongeze Ndasa kuliweka jambo vizuri kama
wanakati wa nishati. Ntaanza na hitimisho la kamati ya PAC. Sikubaliani
na mapendekezo ya PAC. Sioni waziri mkuu amehusiki vipi pia serikali
wametoa majibu yanayoeleweka. Mapendekezo ya kumuondoa waziri wa
nishati, wapi Prof amehusika? Katibu wa nishati wapi amehusika? Tuache
chuki! Tusiandalia sura tuangalie wamefanya nini! Katika wizara
iliyofanya kazi ni nishati na madini. Huo ulikuwa utangulizi.
Taarifa(Mpina): Taarifa ya PAC si taarifa ya upinzani hivyo kusema ina njama za upinzani sio kweli.
Kisangi anandelea:
TANESCO ina madeni ambayo hata ukichukua pesa za Escrow inabaki
sifuri, mizania ya TANESCO inaonekana kuna madeni, mtu ukikosa kupata
haki yako unakimbilia mahakamani,
Taarifa Lugola: Isingewezeka kwenda mahakamani kwa sababu mkataba ulisema waende ICSD kukitokea mgogoro
Kodi mnayosema haiwezi kufatwa kwa sababu mwanasheria mkuu wa serikali alishatoa msamaha
Kafulila: Hasara ya jambo hili sio bilioni 320 pekee, mwezi wa
tisa mwaka huu ulikuwa ndio USA inasaini makubaliano ya MCC sehemu ya
pili lakini kutokana na kashfa hii hadi sasa haijasainiwa,
Taarifa(Muhongo): Tanzania inaendelea vizuri kuhusu MCC
Taarifa(Saada Mkuya): Si kweli September bali December MCC inakaa kwa ajili ya kupitisha hivyo bado hatujafika huko.
Taarifa(Nassari): Muhongo amedanganya Bunge kuhusu Masele, hajawahi kuteuliwa kuwakilisha vijana.
Kafulila: Hasara tuliyopata ni zaidi pesa za Escrow, hasara ya
kwanza ni MCC, hasara ya pili nchi wahisani kupitia bajeti wamegomea $
milioni 500. Katika MCC 1/3 ilikuwa miradi ya umeme lakini tumepoteza.
Barua ya Mramba(mgurugenzi wa tanesco) aliomba muda kupiga mahesabu ya
overcharge ya TANESCO ambapo waziri kaja kulidanganya bunge.
Zitto(Taarifa): Mkopo kwa ajili ya IPTL una Gvt gurantee, na nazungumza kama authority on this.
Leizer: Tuvunje taarifa zinatupotezea muda
Mwenyekiti: Hakuna taarifa tena
Kafulila: Kwenye hoja hii, fedha ni za umma au IPTL? Tukumbushane
waziri wa nishati wa madini alikua akisisitiza kuwa fedha zilitolewa
kwa hukumu ya jaji Utamwa, nilivyohoji nikaiwa Tumbili. Hukumu hii hapa
na hamna sehema iliyosema fedha hizi ni za Escrow, leo anasema ni kikao
cha Kunduchi beach na si hukumu. Hatusemi hawana mazuri waliyoyafanya
lakini kwenye wizi hukumu iko pale pale. Hawa jamaa wamekula pesa za
Escrow pamoja za VAT, madalali wa wizara ya nishati wamesababisha hasara
zaidi ya mramba ya bilioni 11 lakini leo yuko mahakamani
London walisema fedha za overcharge zirejeshwe lakini mtu ambae hukumu
iko kwa manufaa eti ndo anagoma kutekeleza(comply). Kama Seth
alivyoangusha TANU Kenya ndivyo atavyoiangusha CCM Tanzania.
Transfer of shares ikifanyika waziri wa sekta husika lakini waziri
anasema kampuni binafsi serikali haingilii. Imefika mahala tuwajibika,
tunaposema waziri mkuu awajibike(MUDA UMEKWISHA)
Lusinde: Jambo hili tangu tumeanza kulijdaili, limeingiliwa na makundi kama manne hivi;
1. Waliopata
2. Waliokosa
3. Wanaotaka urais
4. Mawakili na Mabenki
Lusinde: tukiendelea kuchangia kwa kufuata makundi hayo tutakuwa hatufiki popote.
Lusinde: Mnasema fedha sio serikali sasa kama fedha sio za serikali tangu lini CAG akakagua fedha zisizokuwa za serikali.
Lusinde: Watu waliopokea mimi sina shida nao ila nina shida na fedha zilipotoka huko nyuma, zimetoka wapi?
Lusinde: Siasa haina urafiki wala uadui wa kudumu, jana Zittokabwe wakati anawasilisha ripoti naona Mbowe anampigia makofi.
Lusinde: Waziri mkuu katangaza nia ya Urais kimya kimya basi na sisi tumpige kimya kimya maana sijaona sehemu aliyotajwa.
lusinde: tusitangulize chuki kwa sababu umekosa. viongozi wa dini
hupokea sadaka wasizozifahamu. tusiwahoji bali tuhoji zilipotoka.
Lusinde: tukiendelea kuchangia kwa kufuata makundi hayo tutakuwa hatufiki popote. #TegetaEscrow
lusinde: Mnasema fedha sio serikali sasa kama fedha sio za serikali tangu lini CAG akakagua fedha zisizokuwa za serikali.
Lusinde: Watu waliopokea mimi sina shida nao ila nina shida na fedha zilipotoka huko nyuma, zimetoka wapi?
Lusinde: Siasa haina urafiki wala uadui wa kudumu, jana Zittokabwe wakati anawasilisha ripoti naona Mbowe anampigia makofi.
Lusinde: Waziri mkuu katangaza nia ya Urais kimya kimya basi na sisi tumpige kimya kimya maana sijaona sehemu aliyotajwa.
Lusinde: Zitto Kabwe ulipokea fedha kutoka sehemu mbalimbali ukitumia watu tofauti, leo inabidi utupe majibu yako.
Lusinde: Leo mnasimama hapa awajibike awajibike, wewe umewahi kuwajibika? unadhani kuwjaibika mchezo?
Lusinde: Mzee Pinda we nenda na kimya kimya yako hadi Mungu atakapokujalia. Habari ya kukutoa hapa haipo.
Mhe Dk Hamis Kigwangallah anatoa taarifa;
DK Kigwangwalah: Kamati ya PAC ni kamati amabyo wajumbe wake wanatokana na Bunge hili.
Dk Kigwangalah: Kusema watu wote wangeitwa kuhojiwa tusingeleta taarifa kwa wakati tulichofanya ni kusoma mahojiano yao na CAG.
Mbowe: Ni vyema tukatenda haki, katika taarifa ya Muhongo
alimzungumzia Ngwilimi(Ananukuu alivyosema ikiwemo aliamua kuacha kazi
mwenyewe baada ya kudanganya ametumwa Malaysia na mwanasheria mkuu).
Hizi taarifa sio za kweli na taarifa za kumtuma Malaysia alitumwa na
mwanasheria mkuu wa serikali na anaonyesha barua.
Muongozo(Masele): Ningependa muheshimiwa atuonyeshe kama imenakiliwa TANESCO.
Mbowe: Ni aibu naibu waziri kumkana mwanasheria mkuu wa serikali,
napenda kushauri taifa, tunanyukana bila sababu za msingi. Kubwa ni
kujua ni fedha za umma au za watu binafsi. Haiwezekani kuchukuliwa
kinyume za taratibu hata kama sio za serikali. Hii miamala yote
iliyofanyika ni halali?
Tunapofanya maamuzi tuwe makini yasije kuturudia siku zijazo kama Richmond, waziri mkuu anatakiwa kuwajibika na sio chuki.
Mahakama ya kimataifa ilifanya uamuzi kuifaidisha Tanzania wakati fedha
zimeshatolewa na waziri mkuu iliujua huu mchakato. Kamati ni ya PAC na
sio kamati ya upinzani na ina wajumbe 19 kutoka CCM na wajumbe watano
upinzani.
Jambo hili linaivua serikali nguo, na kuvuliwa serikali na kuivua nchi.
Muda umeisha,
Mwenyekiti: Nashukuru mjadala wa amani na anataja ratiba ya kesho pia anaahirisha shughuli za bunge mpaka saa tatu asubuhi
============================== ========
KIKAO CHA BUNGE ASUBUHI
Aliekalia kiti leo ni spika wa bunge mama Anna Makinda na anasoma dua ya
ufunguzi wa bunge. Anaanza na maswali kwa waziri mkuu, katibu anaita
hati za kuwasilisha mezani, taarifa ya mwaka ya Mzumbe na chuo kikuu cha
Dodoma ndio zinaanza kuwasilishwa hapa na wizara ya elimu na Mbowe
anakaribishwa kwa maswali kwa waziri mkuu. Pia waziri mkuu kashasimama
kwa ajili ya kupokea na kujibu maswali.
Mbowe: Anaelezea kashfa za serikali na anaulizia kauli ya Pinda
juu ya Escrow, nini msimamo wake? Huoni kuwa ni muda muafaka kupumzika
kuachia nafasi wengine?
Pinda: Inawezakana una shauku kuona litokee hilo, lakini
inategemea Mungu kapanga nini, naweza kujibu lakini sitafanya hivyo kwa
sababu jambo lenyewe ndo lipo mezani.
Mbowe: Waziri mkuu una wajibu wa kulijibu wa swala langu, una heshima lakini itakua vyema ukisema kama fedha ni za umma?
Pinda: Swala la kujiuzulu sio jipya lakini tusibiri hili swala hapa bungeni
Mnyaa: Kuzuiliwa misaada kwa escrow pia imeathiri ZNZ, nini kauli yako wakati hawajahusika hata kidogo?
Pinda: Sijapata mawasiliano yoyote kutoka ZNZ juu ya swala hilo,
hivyo tutalibeba na kama litahitajika ZNZ kwa ufafanuzi tutafanya baina
ya serkali
Mnyaa: mfumo wa serikali mbili ni rahisi kuhongeka kuliko tatu, Escrow kuhonga serikali mbili, ulikua hujui?
Spika kalikataa swali
Moza: Anaulizia kuhusu kilimo, Je! nini tamko la waziri mkuu kuhusu hifadhi ya Mkungunero kwa wananchi
Pinda: Kinachohitajika kukaa chini na mjenge hoja ili kuona kama
kuna uwezekano wa kubadili matumizi ya ardhi husika. Hoja hii ni ya
halmashauri na sio vijiji, hivyo tujenge hoja tuone tunaamua nini kuhusu
hifadhi husika.
Murtadha Mangungu: Takwimu karibu 4B zinapotea kutokana na foleni,
Pinda: Tunajaribu kutafuta ufumbuzi kupitia hatua mbalimbali, na
sehemu kubwa ni utii wa sheria na kama timu tunaweza kupunguza matatizo
haya.
Sakaya: Kwa mujibu wa katiba mbunge na diwani wanadhaminiwa na
chama, akihama au kuacha wadhifa bado anaendelea kulipwa na kushiriki
vikao, kauli ya serikali? Anamtaja na muhusika
Pinda: Inategemea mfano kwa mahakama haina mjadala, lakini baadhi
ya mazingira yanaruhusu, sitaweza kulijibu moja kwa moja hivyo
nalichukua...
Sakaya: Ni busara serikali mkuongeza siku tatu kujiandikisha
Pinda: Nalielewa tatizo lakini kwa sheria ilivyo na tangazo
lilitolewa, mabadiliko yatakua na athari kubwa hivyo haiwezakani, labda
ningekuwa na uwezekano labda ningeomba tumalize mapema lakini naona kama
haiwezekani.
Swali: Nini kauli yako kuhakikisha wananchi wote wanaandikishwa ndani ya siku mbili
Pinda: Jambo limeamuliwa na sio la siri, ni lazima watu wajiandikishe na ilo la Babati tutalicheki
Mwaijage: Unaonaje serikali kutoa mkopo kuchukua mazao kupeleka kwenye maeneo yanayohitajika badala ya kumsaisia mkulima na mlaji
Pinda: Swali linazama mbele sana, bei ya chakula kwa ujumla ni
nzuri kulingana na vipindi vilivyopita, siwezi kujifunga kwamba hilo la
mkopo linawezekana ila ikitokea upungufu wa chakula tutapeleka kama
kawaida.
MASWALI YA KAWAIDA
Riziki: Mkoa wa LIndi wanaongoza kwa mimba za mashuleni kutokana na kutokua na mabweni
Mwanri: Serikali inashirikiana na wadau ili kuweka miundombinu shuleni, tumetoa pesa pia tumeweka sheria ya ubakaji kuwalinda watoto.
Kessy: Watoto kupata mimba ni nchi nzima, kwanini serikali isiongeze adhabu bila faini
Mwanri: Watoto kupata mimba linatuhusu sote kama kila mtu atasimama katika nafasi haya mambo hayataendelea
Swali(Mlata): Watake radhi wanawake wote waliopata mimba, wewe binafsi ni viongozi wangapi umuwawajibisha
Jibu(Ghasia): Mimba watoto wa shule kila mtu ana nafasi ikiwemo
wazazi na walezi, kila mtu akiamua tutazikomesha hizi mimba za utotoni,
kutembea usiku na kukuta watoto wadogo wanazarura hili ni tatizo kwa
jamii na malezi kwa watoto wetu
Swali(Suzan Lymo): Mabweni yanapunguza mimba, serikali ina utaratibu gani wa kuwapatia fedha TEA ili wajenge mabweni
Jibu(Kawambwa): Kuna mkakati kuhakikisha wasichana wanasoma,
lakini tunafahau tatizo la bajeti hivyo bunge hili limepitisha bajeti na
hatuna pesa zaidi kwa ajili TEA
Swali(Jason Rweikiza): Ni lini azma ya kujenda zahanati itatimia
Jibu(Mwanri): Azma hii inalenga mwananchi kutotembea zaidi ya KM 5
kutafuta hudima ya afya, tutaendelea kutenga bajeti kumalizia vituo
vilivyobaki
Swali(Freeman Mbowe):Kwa nini miradi ya barabara inachukua muda mrefu kumaliziwa
Jibu(Lwenge): Miradi inaendeshwa kutokana na mikataba na pia hela huchelewa kufika kutokana na ufinyu wa bajeti.
Swali(Suzan Kiwanga):Je waziri uko tayari kutembelea maeneo ya kilombero mpaka Njombe kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara?
Jibu(Lwenge): Nakubali kutembelea hayo maeneo
Swali(Kidawa): Kwa nini serikali inayaacha majengo ya serikali katika balozi mbalimbali yanachakaa?
Jibu(Naibu Waziri Maalim): Serikali bado inafanya jitihada kwa
njia ya kutumia mifuko ya hifadhi ya jamii kujenga na kukarabati ofisi
mbalimabali za balozi zetu.
Swali(Blandes): Matukio ya ujambazi yamezidi katika mkoa wa Kagera, serikali ina mkakati gani katika kushughulikia tatizo hili sugu.
Jibu(Silima): Tunatambua kuwa mkoa wa Kagera una changamoto
nyingi za kiulinzi, tutazama uwezekano wa kuufanya mkoa wa kagera
kuufanya uwe mkoa maalumu wa kipolisi pia tutaongeza idadi ya polisi ili
kuongeza ulinzi.
Muda umeisha na wanatambulishwa wageni, wageni 15 wa Simbachawene,wageni
watano wa Magnalena, wageni wa Wenje, wageni wa Kitandula ambao ni
wakandarasi wa maji, wageni wa Vicky Kamata ambao ni watoto wake, Wageni
wa Moza madiwani kutoka Singida, wageni wa Kilufi baba na mama kutoka
Mbarali. Waliokuja kwa mafunzo wanafunzi 15 kutoka St. John, Mwanafunzi
kutoka Mzumbe.
Shughuli za kazi
Ngeleja anatangaza wajumbe kuwa kuna mkutano saa saba mchana sheria na
utawala, miundombinu na biashara. Lembeli anatangazia wanakamati kuwa
kuna kikao
MIONGOZO
Mnyaa: Mjadala wa ripoti ya escrow ni siku tatu na bunge
linaahirishwa kesho, Je tunaongeza Jumamosi au kesho tunaondoa kipengele
cha maswali na majibu?
Makinda: Amekataa kwamba alisema siku tatu ila pia amesema siku tatu zimekamika
Nasari: Bunge linalipa pesa nyingi TBC kwa ajili ya matangazo ya
bunge, lakini matangazo yanakatwa mambo yakihusu serikali, pia umeme
unakatwa sana hasa kipindi ambacho serikali inabanwa
Makinda: Silifahamu kwa sababu humu ndani sioni unakatika wala hayo matangazo siyaoni, miongozo inapunguza muda.
Hamisi Kombo: Matukio kama Richmond na operation tokomeza
serikali haikutoa utetezi, leo kuna utetezi utaletwa, hii inaonyesha
double standard katika utetezi, naomba muongozo kwanini waliohusika
wasijitetee wenyewe badala ya kutetewa na serikali
Makinda: Huo ndio utaratibu, na leo naruhusu upande wa pili wajibu na hawamtetei mtu bali wanajibu
like page yetu hapa kwa habari zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment