
“…. Kwa
kuwa suala hili ni suala nyeti, Watanzania wote wanafuatilia jambo hili
kwa umakini kujua hatma ya jambo hili naomba Mheshimiwa naibu Spika
utupatie mwongozo wa Bunge na Watanzania kuhusu uhakika wa Ripoti hii
kuletwa Bunge hili ili kuondoa mashaka ambayo yamekuwa yakijengeka
kwamba kuna mikakati.. kuna njama ambazo Mahakama inataka kutumika kama
kichaka cha kuweza kuficha wezi wa hizi fedha, na kwa hiyo Watanzania..
ili kusudi Watanzania waliamini Bunge lako tukufu kwamba ndiyo ‘Supreme
organ’ kwenye uendeshaji wa nchi hii na kwamba jambo hili litajadiliwa
katika Bunge hili na tutafanya maamuzi ya mwisho…“– David Kafulila.

Naibu Spika Job Ndugai akajibu; “… Asante sana, nitatolea mwongozo jambo hili mwishoni…”
Baada ya hapo akateuliwa Mbunge Esther
Bulaya, ambapo kutokana na mwongozo alioutoa ulikuwa sawa na wa Mbunge
Kafulila akaombwa asubiri ili wachangie wengine, mwongozo kuhusu ESCROW
ungehitimishwa mwisho wa kikao hicho.
Naye Moses Machali alipewa nafasi akasema haya; “…
Ukifanya ‘situational analysis’ ya mwenendo wa Bunge letu hivi sasa,
Bunge limegubikwa na kupuuzwa na kudharauliwa na mihimili mingine
ikiwemo Serikali na sasa Mahakama nayo imeanza ku-penetrate kwenye
kudharau hili Bunge…”
“… Suala
langu ni nini.. Unadhani Wabunge ambao pengine tungependa kuona haki,
kinga na madaraka ya Bunge hayaporwi, tufanye nini au tutumie nguvu gani
za ziada ili kuweza kudhibiti Mihimili mingine ambayo imekuwa inataka
kupora uhuru na Madaraka ya Bunge kama ambavyo imeainishwa kwenye Ibara
ya 100… kama hili suala ambalo ESCROW leo hii linatikisa…”– Machali
No comments:
Post a Comment