Pages

Wednesday 29 October 2014

MOJA KATI YA MATUKIO YA AJABU DUNIANI YAKIAMBANA NA UPENDO, AFUNGA NDOA NA MAITI


 picha hii hapa ni wakati wa mapenzi yao kabla ya kifo kilichotokea
Moja kati ya matukio ya kushangaza sana hapa Duniani, ni tukio la kijana mmoja, aliyeomba kufunga ndoa na mchumba wake ambaye alifariki ghafla kutokana na ajali

Tuesday 28 October 2014

Pata Picha ya Haya Mjanga

Jamaa wawili walikuwa wamekaa baa wanakata kinywaji (Mmmoja alikuwa mmarekani na mwingine muhindi) Jamaa wa kihindi kwa sauti ya kilevi akaanza kulalama "Huko home bhana wanadai wamenitafutia mchumba natakiwa nimuoe, wanadai ni wa huko kijijini kwetu. Mi nimekataa nimewaambia siwezi kumuoa mtu ambaye simpendi, kwahiyo nina bonge la msala wa kifamilia huko"

Mmmarekani akamuangalia akacheka, akapiga funda jingine akamwambia, unasema una matatizo? Ngoja nikupe stori yangu uone majanga yalivyo.

JE WAJUA? CHUMBA CHA MAAJABU KILICHOPO JUU YA DUNIA.

Image
Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali

MAUZAUZA:KAMANDA WAKITENGO CHA MADAWA YAKULEVYA " NZOWA " ATUMIWA PAKA 3 OFISINI

Paka watatu wenye macho mekundu walimshangaza Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa pale alipowakuta katika mlango wa ofisi yake na kumng’ang’ania miguuni.
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Godfrey Nzowa akiwa ofisini kwake.
Sakata hilo lilitokea wiki iliyopita wakati Kamanda Nzowa akitoka ofisini na mgeni wake aliwakuta paka hao mlangoni.Kufuatia hali hiyo, wageni na baadhi ya askari anaofanya nao kazi walionekana kushangazwa na tukio hilo huku wakijiuliza kwa nini paka hao wamzingire kamanda huyo na kuwaacha watu wengine?

Saturday 25 October 2014

Igeni Imani Yao

Noah with a tool for building the ark

“Alitembea Pamoja na Mungu wa Kweli”

1, 2. Noa na familia yake walifanya kazi gani, na walikabili matatizo gani?
NOA alinyoosha mgongo na misuli yake iliyokuwa na maumivu makali. Mwazie akiwa ameketi kwenye ubao mpana, akipumzika katikati ya kazi, huku akitazama safina kubwa iliyokuwa ikijengwa. Harufu kali ya lami iliyoyeyushwa ilitanda hewani na alisikia sauti za vifaa vya kutengeneza vyombo vya mbao. Akiwa mahali alipoketi, Noa aliwaona wanawe wakifanya kazi kwa bidii kwenye sehemu mbalimbali za jengo hilo kubwa la mbao. Wanawe, wake zao, na mke wake mpendwa walikuwa wamefanya kazi ya kujenga safina kwa makumi ya miaka. Walikuwa wamefanya kazi nyingi, lakini haikuwa imekamilika!
2 Watu katika eneo hilo waliwaona kuwa wapumbavu. Noa alipoendelea kujenga safina, watu walimcheka waliposikia kuhusu gharika ambayo ingefunika dunia yote. Walidhani Noa aliwaonya kuhusu msiba wa kuwaziwa, ambao haungetukia kamwe! Hawakuelewa kwa nini mwanamume angepoteza maisha yake, na ya familia yake, akifanya kazi kama hiyo ya upumbavu. Lakini Yehova, Mungu wake hakumwona hivyo.
3. Noa alitembeaje na Mungu?

HII NDIO MELI YA KUBEBA ABILIA KUBWA KULIKO ZOTE DUNIANI

Meli hii inaitwa "Allure of the Sea" ilizinduliwa tarehe 20 November, 2010 na ilianza kufanya kazi kwa mara ya kwanza 1 December, 2010, inakadiliwa kuwa na uzito wa tani 225,282 na pia ina urefu wa 362 m (1,187 ft)  na kimo chake ni 72 m (236 ft) kwa kwenda chini na ina wafanyakazi wapatao 2,384  na inakadiliwa kupakia watu kuanzia 5,400 mpaka 6,296.  Meli hii ina vyumba

Picha Zisizo Za Kawaida No.9: Jengo Refu Kuliko Yote Duniani Linavyostahimili Radi!

It was a thunder lightning night ...... Hit the world talest tower DUBAI TOWER As long as half hour and the lighning was hitting the tower and the thunder sounded All over the neighouring area something more than usual.


Mnakumbuka tetemeko lilivyotikisa PPF Tower? Mabomu ya Mbagala Je?

Hii radi ingetokea Bongo pale PPF au Mkapa Towers Ingekuwaje? Elezea Picha unayoipata . . .





like page yetu kwa maajabu zaidi

Haya ndiyo majengo saba marefu zaidi duniani, si mchezo

Tunakuorodhoshea majengo saba marefu kuliko yote duniani. Dubai ndiyo inabeba sifa ya kuwa na jengo lililopanda angani kuliko yote hapa duniani.

7.Petronas Tower: Kuala Lumpur, Malaysia
Majengo ya  Petronas Twin Towers
Pia hujulikana kama Petronas Twin Towers, minara pacha hii ndiyo majengo pacha marefu zaidi duniani, yana urefu wa

ORODHA NA PICHA ZA MAGARI YENYE SURA MBAYA DUNIANI

 
Black Falcon,ambalo limeundwa na Kampuni ya DARTZ Motorz Company,ya Uchina

 
Sehemu ya Tangazo la Gari hilo linalotarajiwa kuanza kuuzwa katika soko la magari la Mashariki ya Kati na Arabuni mapema mwaka huu

 
Gari hilo Black Falcon kama linavyoonekana kwa ndani; Limetengenezwa kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya NYOKA inayosherehekewa nchini China

GARI BAYA ZAIDI KUWAHI KUTENGENEZWA DUNIANI...Ona hapo chini...






PICHA JUU: TOYOTA BB miongoni mwa magari yanayotajwa kuwa mabaya zaidi duniani

 
Miongoni mwa mengine pia limo Aston Martin Lagonda hilo hapo juu.



600-Aurora huenda likavunja rekodi,ambalo limeelezwa kufanana na mnyama Faru anaemkimbiza adui yake! baadhi ya Watoto wakiliona hili huanza kulia akiwemo mtoto wa Martin Jusper wa Uingereza anaelimiliki

Maelezo ya hili yamejitosheleza katika picha AMC PACER ambalo liliundwa mwaka 1975.Ni baya lakini limeelezwa kuwa miongoni mwa magari yenye spidi kubwa enzi hizo.

Orodha bado ni ndefu; Pichani ni CHEVROLET CORVAIR ambalo likisahaulika 'haki haijatendeka!

Kampuni ya Magari ya FORD ni miongoni mwa makampuni maarufu ya magari duniani lakini hapa 'designing' iliwashinda! Hilo ni FORD EDSEL  liliundwa miaka 50 iliyopita.

Chevrolet hivi leo ni gari inayopendwa na kuhusudiwa na wapenzi wa magari duniani lakini designing hii duh! Hiyo ni Chevy Chevette
 iliyoundwa miaka kama 60 iliyopita lakini baada ya kutembea 40,000 Injini yake ikasambaratika kutokana na 'kuchemsha'
like page yetu kwa habari zaidi

WILAYA ya Rungwe Jijini Mbeya ina mambo mengi ya kustaajabisha na miongoni mwa mambo hayo yapo kwenye Mto Kiwira. Mto Kiwira unazidi kupanda chati kuliko mito mingine wilayani humo kutokana na kuwapo kwa Daraja la Mungu. Lakini pia karibu na daraja hilo yapo maajabu mengine yakiwamo ya chekeche la uchafu unaokusanywa na maji kabla ya kuingia eneo maarufu la Kijungu. Kijungu nayo ni sehemu ya Mto Kiwira, ni eneo la ajabu kwa sababu mwamba wake umeumba kitu kama chungu kinachopokea maji yote na kuyapeleka chini bila kupitisha juu ya mwamba. Inaelezwa kwamba mtu anayetaka kuvuka salama kwenye mwamba juu ya Kijungu kutoka upande wa Mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia na akitokea Magharibi atumie mguu wa kushoto tu ili asitumbukie. Maajabu mengine ni kuwapo kwa taarifa zinazodai mtu akizama kwenye mto huo, lazima afuatwe mzamiaji mmoja aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo, aliyezama hawezi kuonekana mpaka siku saba zitakapopita. Lakini jambo kubwa linaloonekana na kustaajabisha ni kuwapo kwa daraja linaloaminiwa na wakazi wa eneo hilo na wilaya nzima ya Rungwe kwamba lilitengenezwa na Mungu kwenye eneo la Mto Kiwira unapotenganisha Vijiji vya Lugombo kwa upande wa Mashariki mwa mto huo na kile cha Mboyo kilichopo Magharibi.

WILAYA ya Rungwe Jijini Mbeya ina mambo mengi ya kustaajabisha na miongoni mwa mambo hayo yapo kwenye Mto Kiwira.
 Mto Kiwira unazidi kupanda chati kuliko mito mingine wilayani humo kutokana na kuwapo kwa Daraja la Mungu.
 Lakini pia karibu na daraja hilo yapo maajabu mengine yakiwamo ya chekeche la uchafu unaokusanywa na maji  kabla ya kuingia eneo maarufu la Kijungu.
 Kijungu nayo ni sehemu ya Mto Kiwira, ni eneo la ajabu kwa sababu mwamba wake umeumba kitu kama chungu kinachopokea maji yote na kuyapeleka chini bila kupitisha juu ya mwamba.
Inaelezwa kwamba mtu anayetaka kuvuka salama kwenye mwamba juu ya Kijungu kutoka upande wa Mashariki lazima atumie mguu mmoja wa kulia na akitokea Magharibi atumie mguu wa kushoto tu ili asitumbukie.
Maajabu mengine ni kuwapo kwa taarifa zinazodai mtu akizama kwenye mto huo, lazima afuatwe mzamiaji mmoja aliyerithi kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo,  aliyezama hawezi kuonekana mpaka siku saba zitakapopita.
Lakini jambo kubwa linaloonekana na kustaajabisha ni  kuwapo kwa daraja  linaloaminiwa na wakazi wa eneo hilo na wilaya nzima ya Rungwe kwamba lilitengenezwa na Mungu  kwenye eneo la  Mto Kiwira unapotenganisha Vijiji vya Lugombo kwa upande wa Mashariki mwa mto huo na kile cha Mboyo  kilichopo Magharibi.
like page yetu kwa habari zaidi 

JE,WAJUA?!TAJIRI WA DUNIA YUPO TANZANIA..BAJETI YAKE NI KUFURU ...!!!SOMA ZAIDI HAPA...

TAJIRI namba moja duniani, Bw. Mukesh Ambani (53) (pichani) raia wa India amewasili nchini jana alfajiri kimyakimya kwa safari ya kitalii.
Tajiri huyo aliwasili juzi saa 10.15 alifajiri Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi akifuatana na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa waratibu wa safari hiyo hapa nchini, Bw. Godfrey Famandes zimeeleza kuwa lengo la safari yake ni kutembelea hifadhi za taifa, hususan Hifadhi ya Serengeti.


Bw. Ambani kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa ndiye tajiri namba moja akimiliki dola za Marekani bilioni 63.2 (zaidi ya sh. trilioni 90), akifuatiwa na Carlos Slim Helu kutoka Mexico mwenye dola za Kimarekani bilioni 62.2993 na Mmarekani William Bill Gates akifuatia kwa karibu akimiliki dola za Marekani bilioni 62.29.

 
Katika kundi hilo dogo la matajiri watano duniani nafasi ya nne inashikiliwa na Warren Buffett kutoka Mexico ambaye anamiliki dola 55.9 na kufuatiwa na Lakshmi Mittal wa India mwenye kitita cha dola bilioni 50.9.

Akizungumza na njia ya simu jana, Bw. Famendes ambaye ni Mkuu wa Oparesheni wa Kampuni ya Gapco Tanzania ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo na mwenyeji wa
tajiri huyo, alikiri kuwasili kwa tajiri huyo na kusita kuzungumzia safari hiyo zaidi.


Safari yenyewe ni ya binafsi zaidi, hivyo sina cha kukueleza zaidi ya kukuthibitishia kuwa ni kweli amewasili…sina uhakika na idadi ya wafanyabiashara aliofuatana nao, alisema Bw. Famendes kwa njia ya simu.

Habari zaidi kuhusiana na safari hiyo zimeeleza kuwa tajiri huyo pamoja na wenzake wamewasili Hifadhi ya Serengeti, ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, na tayari jana walifanya mzunguko wa kwanza wa kutembelea hifadhi hiyo na kujionea maajabu ya dunia ya hifadhi hiyo.

Kuja kwa mfanyabiashara huyo na wenzake na fahari kubwa kwa Tanzania, kwani ni kielelezo kuwa tayari dunia imeanza kujua vivutio tulivyo navyo, nchini na umuhimu wake duniani, alisema mmoja wa wakurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) huku akisizitiza kuwa hana habari lakini akiahidi kufuatilia ujio huo.

Bw. Ambani alizaliwa Aprili 19 mwaka 1957, huko Aden (Colony of Eden) sasa Yemen akiwa na uraia wa India. Kwa sasa anaishi Antilia, Mumbai Maharashtra na mke wake Nita Ambani, wakiwa na watoto watatu, Akash, Anant na Isha

like page yetu kwa habari zaidi

JE WAJUA? HUYU NDIYE MBWA TAJIRI KULIKO WOTE DUNIANI, ANA UTAJIRI WA KIASI CHA DOLA ZA KIMAREKANI 373 MILLION.


Pichani ni Mbwa anayeitwa Gunther VI aina ya German Shepherd ambaye ana utajiri wa kiasi cha dola za kimarekani Million 373.
Ni ajabu kusikia mbwa naye anakuwa katika orodha ya viumbe vyenye hela duniani japo kwa wenzetu nchi za magharibi hilo kwao ni jambo la kawaida sana, leo hii katika session ya Je wajua nimeona nikuletee huyu Mbwa ambaye anashika namba moja katika Mbwa ambao ni matajiri ambaye anakadiriwa kuwa na kiasi cha dola za kimarekani Million 373.
Vitabu vingi mbalimbali vimeandika kwamba Mbwa ni rafiki mkubwa wa mwanadamu ambapo hapa namzungumzi huyu mbwa tajiri duniani aitwaye Gunther VI, Mbwa huyo ambaye amepata urithi kutoka kwa baba yake aitwaye Gunther III’s ambaye ndiye alikuwa mrithi wa hela hizo.

Pichani ni Billionea Karlotta Liebenstein enzi za uhai wake akiwa na mmoja wa mnyama aliyekuwa akimpenda .
chanzo cha mbwa hawa kuweza kuingia katika rekodi ya dunia ni kutoka kwa mwanamama mmoja billionea mjerumani aliyekuwa akiitwa Karlotta Liebenstein ambaye alifariki mwaka wa 1991, inasemekana  alikuwa na mapendo sana na wanyama hivyo kabla ya kufa aliandika usiha kwa kila mnyama wake aliyekuwa akimfuga apewe  kiasi ambacho alichokisemkwa wanyama aliowapenda,  ambapo baba wa Gunther VI ndiye aliyeandikwa mrithi wa kiasi hicho cha hela nae haikupita muda akafa na kurithishwa hela zote Gunther VI.
Pia mbwa huyo anafanyiwa huduma za hali ya juu pamoja na kula vyakula vya hali ya juu ambavyo huwa hawali mbwa wengine, mbwa huyo Gunther anamiliki jumba kubwa na la kifahari jijini Miami Marekani ambalo jumba hilo linapakana na jumba la mkali wa miondoko ya pop mwanamama Lady Madona, Mbwa huyo ana gari yake maalu ya kutembelea na bwawa la kuogelea maarufu kama swimming pool. Hayo ndio mambo ya Dunia.

Je wajua? Hili ndilo basi refu kulipo yote Duniani, Lina viti zaidi ya 256... Shuhudia hapa



The world’s longest bust will soon debut on the streets of the city of Dresden, Germany. The bus which said to sit 256 passengers has been described as a train on wheels.

Designed by Fraunhofer IVI and the Technical University, Dresden, the three-section Autotram Extra Grandbus is 98 feet long. And, interestingly, it does not require any special training for its driver!

The Autotram Extra Grand Bus is said to be as easily maneuverable as a commonly sized bus, and it makes use of a computer system to aid its driver with turning. The system’s primary purpose is to ensure that the rear section of the bus precisely follows the front and middle sections at all times. Also, in addition to this sophisticated guidance system, the bus incorporates green technology by way of a hybrid gas and electric engine that can travel five miles operating purely on battery power.

This technological monster will hit the streets of Dresden in October after completing safety testing outside of the city. Meanwhile, its makers say that they’ve already received inquiries from other cities around the world about getting their own versions of the bus, since it costs much less to put into operation and maintain than commuter rail systems, yet still carries a massive amount of passengers.
like our page for more news

Je, wajua kwamba Kondo la Nyuma au ‘Placenta’ huliwa na wajawazito?

kondo
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.
  • Hugeuka kuwa uchafu pindi mama anapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?

Taarifa zinazohusiana

Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.

Njia za kula Kondo la Nyuma

  • Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vile
  • Inaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembe
  • Kupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.
‘Mama ale Kondo la Nyuma?’
Baadhi ya wanawake husaga kondo hilo na kunywa maji yake saa chache tu baada ya kujifungua, baadhi wanaihifadhi na kutengeza tembe ambazo wanameza na wengine wanaikata vipande vipande kwa kuweka chini ya ndimi zao.
Wanafanya hivyo kwa kuamini kuwa tembe hizo zinaweza kuwapa nguvu na pia kusaidia maziwa ya mama kuongezeka.
Kampuni moja nchini Uingereza inayotengeza biadhaa mbali mbali kutoka kwa Kondo la Nyuma, hulipisha watu kati ya pauni 150 au dola elfu kumi na saba kwa kila tembe na chini ya dola hamsini kwa maji ya kondo hilo linaposagwa.
Baadhi hutengeza maji ya sharubati kwa kuichanganya na matunda
Baadhi wanaamini kuwa Kondo la nyuma huwa na madini mengi ambayo hayapaswi kutupwa tu.
Lakini kampuni hiyo inakumbwa na kesi mahakamani ambayo huenda ikaisababisha kufungwa.
Kampuni hiyo ilishitakiwa na wataalamu wanaohofia kuwa bidhaa hizo zinaweza kuwa na Bakteria ambayo inaweza kusababisha athari za kiafya kwa wanaotumia bidhaa zinazotokana na kondo la nyuma.
Charlie Poulter, kutoka mtaa wa Reading, anaamini kuwa alipokunywa maji ya kondo la Nyuma pindi baada ya kujifungua ilimwezesha kupata nguvu.
“nilikunywa harakaharaka, kwa sababu sikutaka kutafakari kuhusu harufu na ladha yake, alisema Charlie”
“nilikuwa nimejifungua na nilihisi kuishiwa na nguvu sana na pia kwa kiasi kidogo nilijidharamau. Kwa hivyo nilihisi kuwa ikiwa nitakunywa maji hayo ingenisaidia kupata nguvu na kupona haraka,” alisema mama Charlie.
‘Kondo la Nyuma ni nini?’
Baadhi ya wanawake huikausha na kuikaanga kama nyama
Hii huwa ni kiongo cha mwili ambacho huwa kimeshikana na nyumba ya mtoto pamoja na kitovu.
Kiungo hicho hubeba hewa ya Oxygen na madini kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.
Pia husafirisha uchafu kutoka kwa mtoto hupitia kwa kiungo hicho hadi kwa mama.
Baada ya mtoto kuzaliwa kiungo hicho hutoka mwilini mwa mama anaposukuma mtoto au hutolewa na madaktari mama anapofanyiwa upasuaji.
Binadamu kwa kawaida hajulikani kwa kula sehemu hiyo ya uzazi. Ni kawaida kwa baadhi ya wanyama wa baharini na wanyama wengine wa kufugwa. Lakini kwa mwanmadamu , bila shaka ni jambo geni.
Nchini China baadhi ya madaktari wa kienyeji hutumia sehemu hiyo ya mwili kutengeza dawa za kienyeji lakini utamaduni huu wa watu kula Kondo la Nyuma umeanza tu kusikika katika mataifa ya magharibi.
‘Je wanasayansi wanasemaje?’
Hadi leo hakuna utafiti wowote kuhusu wanawake wanaokula Kondo la Nyuma.
like page yetu kwa hufahamu zaidi

Friday 24 October 2014

Vituko vya mwishoni mwa wiki, achana talaka




Tuesday, June 07, 2011 11:19 AM
KATIKA hali ambayo haijazoeleka katika jamii, mwanamke mmoja [jina kapuni] [26] ameshangaza wanafamilia kwa kuchana talaka iliyoandikwa na mume wake mara baada ya kukabidhiwa na mumewe huyo.
Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe kwa kile kilichodaiwa kuvunja moja ya amri alizopewa na mume huyo wakati wanaingia katika mkataba kabla ya kufunga ndoa yao.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe akiwa mkoani Pwani katika moja ya sherehe za unyago mkoani humo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo aliondoka jijini Dar es Salaam akimuaga mumewe huyo kuwa anaenda kwenye sherehe ya harusi ya moja ya ndugu zake katika ukoo wake kama mbinu ya kuruhusiwa na mume wake.

Imedaiwa awali mume huyo kabla hajamuoa mwanamke huyo walikubaliana kuwa mkewe asiwe anahudhuria shughuli za ngoma za unyago zinazopendelewa kufanywa mara kwa mara katika familia yao ikiwa ni kuenzi utamaduni endelevu wa kabila hilo. Walioana mwaka mmoja uliopita baada ya kuafikiana masharti hayo.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo aliweza kuvumilia kutohudhuria shughuli hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na kudaiwa kupata malalamiko kutoka kwa ndugu zake kuwa ametengana na familia kwa kuwa hahudhurii shughuli hizo na ilidaiwa kuwa familia yake ilitishia kumtenga iwapo hatakuwa akihudhuria sherehe hizo.

Mwanamke huyo alimdanganya mumewe na kumuomba ruhusa kuhudhuria moja ya harusi kumbe alikuwa anakwenda kuhudhuria shughuli hizo za kitamaduni ambazo mume wake huyo alimpiga marufuku.

Mume huyo alifanya uchunguzi na alibaini kuwa hakukuwa na shughuli ya ndoa bali kulikuwa na shughuli ambayo hapendi mke wake ahudhurie na alimpiga marufuku kuhudhuria.

Imedaiwa mume huyo alipandwa na jazba na aliandika talaka moja apelekewe mkewe.

Mkewe alipokabidhiwa talaka hiyo aliichana hadharani na akidai hakuna kosa alilolifanya na aliendelea na shuhguli zake zilizompeleka huko na kudaiwa atarudi nyumbani kwake leo.
Kitakachoendelea mtafahamishwa
   

Thursday 23 October 2014

Vichekesho kati ya mume na mke kanisani

Vichekesho kati ya mume na mke kanisani Je unajua vichekesho kanisani? ulishasikia mojawapo, hebu fuatilia hii hapa.
Kulikuwa na familia moja ya wacha Mungu vizuri tu pale Dar es salaam. Walikuwa wakisali kanisa moja la kilokole.  Mwanaume alikuwa na tabia ya kulala usingizi kila akiingia kanisani kusali. Siku moja mke wake akagundua dawa ya kumfanya jamaa aache kabisa tabia hiyo mbaya ya kulala kanisani. Unajua ni dawa gani hiyo?
Kukiwa tu ndo ibada imeanza, jamaa alianza kuuchapa usingizi na mke bila kukawia akamminya kwa haraka akamwambia,
“Mchungaji amekuteua ufunge ibada kwa maombi”
Mwanaume akasimama haraka na kuanza kushusha maombi makali ya kufunga ibada
“Baba katika jina la Yesu tunakushukuru kwa ibada nzuri, Asante kwa ujumbe wa leo kutoka kwa mtumishi wako Mchungaji, Asante kwa miujiza ya uponyaji. Tunaomba ututangulie tunapokwenda majumbani kwetu kupumzika, Kanisa  woote tuseme Amen”
Baada ya kumaliza sala tu, alijikuta kanisa nzima likimkodolea macho huku wengine wakicheka sana, na wengine wakiwa midomo wazi na wengine wakiinama kwa aibu kwani ibada ndo tu ilikuwa imeanza na jamaa anashusha sala ya kufunga ibada!
hii kali.
Nimesikia kuwa huyo bwana aliacha hiyo tabia ya kulala lakini sikujua mahusiano yake na mke wake yaliendelea kuwa mazuri au la.

like page yetu kwa vimbwanga zaidi

Vituko vya Housegeli na Mama Mwenye Nyumba

“Kichekesho cha msichana wa kazi za nyumbani na mama mwenye nyumba juu ya vijiti vya kusafishia meno.
jamani nyie watoto wa nyumba hii, vijiti vya meno nimeleta juzi tu leo vyote vimeisha, mnazipeleka wapi?”
Ndipo housegirl akadakia na kusema “Mama mimi simo humo maana kila nikimaliza kutumia tu navirudishiaga humo humo”
like page yetu kwa vichekesho zaidi

Vituko vya Konda wa Daladala na Abiria

Vituko vya Konda wa Daladala na Abiria Kwa wale mnaotumia sana usafiri wa umma au daladala utakuwa umekumbana na mojawapo ya ya vituko vya makonda na abiria wa daladala kama ifuatavyo
Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
Konda; Yesu bado hajatoa albam.
Matozi; humu ndani joto
Konda; kapande friji
Abiria; kuna siti?
Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?
Sistaduu: Konda unanibana
Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!
Mama: sikai siti za mwisho
Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?
Abiria : we konda  vipi kuwa  kama umeenda  shule
Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule
Kama una mengine tafadhali ututumie na tutakuwekea kiunganishi cha blogu au web yako hapa bure

Vituko na Vichekesho vya Mmasai na Mpogoro

Vituko na Vichekesho vya Mmasai na Mpogoro Kule Morogoro katika kibanda cha kuuzia vinywaji baridi kulitokea vichekesho vya mmasai mmoja na mpogoro mojawapo ya hivyo vichekesho hiki kidogo lakini inachekesha na kuvunja mbavu.
Kijana mmoja wa kimasai mtanashati, mwenye umri wa wastani alikwenda kujipatia kinywaji baridi katika kibanda hicho cha mpogoro.
Fuatilia mazungumzo yao:
Mmasai: Ile soda nyeusi iko? (akimaanisha cokacola)
Mpogoro: Ndiyo ipo
Mmasai: Mpe mimi
Mpogoro: Hii hapa
Mmasai: Fungua
Mpogoro: Nimeifungua hii hapa
Mmasai: Nipimie ya silingi kumi:
Mpogoro akaduwaa, sikujua kilichoendelea baada ya hapo
like page yetu kwa vichekesho zaidi

{Vichekesho} Swali nani kati ya hawa ni mchawi kuliko mwenzie?

1) Alizama baharini kwa muda wa dakika 30, akaibuka akiwa mkavu kabisa.
2) Alizama baharini na mshumaa unaowaka kwa muda wa dakika 30 akaibuka nao ukiwa unaendelea kuwaka.
3) Alitandika mkeka juu ya bahari akalala, alipoamka asubuhi akaanza kukung’uta vumbi
Nani mkali kuliko Mwenzie?.
like page yetu kwa vichekesho zaidi

MAAJABU YA TANGA-MTOTO WA MIEZI 4 AZUNGUMZA

Mtoto wa miezi minne aliyezaliwa kwenye hospitali teule wilayani Muheza, amekuwa gumzo na kustaajabisha wakazi wa mji huo, wakiwamo wazazi wake, kutokana na kuzungumza akiwa na umri huo.

Mtoto huyo aliyezaliwa Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa na mtu yeyote akitaka kumsalimia.

Akizungumza mama wa mtoto huyo Bi Rosemary Mhina , mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi saba, alikuwa akilia tumboni.

"Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma, utamsikia mtoto analia timboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule, nikaja huku Bombo na Tumaini, nilipopigwa 'ultra sound' madaktari wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa kifaa hicho," alisema Bi Rosemary Mhina.

Akielezea zaidi kuhusu namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa alipofikisha miezi miwili, siku moja alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupe maziwa"

Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si mazuri mama nakuonea huruma"

Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume(Jina limehifadhiwa) ambaye amedai kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru Arusha, alimpa sh.30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi sita.

"Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa, hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu", alidai Rosemary.

Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko.

"Kipindi kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala wakaniparua huku mwanangu Upendo akinicheka", alidai.

Mambo makubwa hayo je ingekuwa wewe ungefanyaje?

AIBU; MAMA HUYU AFANYA MAAJABU YA MWAKA AFIKISHWA MAHAKAMANI KUTOKANA NA UFIRAUNI ULIOFANYA. SOMA HABARI KAMILI HAPA


Mama mmoja aliyeolewa na mwenye watoto watatu ambae anaishi Hull, Uingereza, amefikishwa mahakamani baada ya kugundulika kuwa alipata ujauzito baada ya kufanya mapenzi kwa wakati mmoja na mtoto wa shule, mmoja mwenye miaka 15 na kaka yake mwenye miaka 17.
Mama huyo anaejulikana kwa jina la Claire Louise Roundil(32), alimnasa mtoto wa miaka 15 kimapenzi baada ya kumuonesha picha zake zaidi ya mia moja akiwa mtupu, picha zilizoonesha zaidi sehemu za matiti.

Baada ya kumteka akili na hizo picha mama huyo alimpeleka chocho na akampa huyo mtoto share ya mmewe. Lakini aliendelea kumbadilishia location mara kwa mara ili kumpa mzuka zaidi wa kufanya nae sex.

Ripoti ya polisi ilionesha kuwa mama huyo alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na kaka yake huyo mtoto na alimpata kwa style ile ile kama alivyomnasa mdogo wake, yaani kumuonesha picha zake akiwa mtupu kisha anamteka akili na kumpeleka kajificheni kumpa burudani, na mara nyingine shughuli iliishia kwenye gari la mama huyo.

Hata hivyo uchunguzi wa polisi ulionesha kuwa baada ya mama huyo kupata ujauzito ilimbidi autoe, na alipoulizwa alisema kuwa hata aliyempa mimba hamjui kati ya hao watoto wawili kwa sababu alikuwa anafanya nao mapenzi wote.

Moja kati ya sababu za kufanya hivyo imesekana kuwa alikuwa na matatizo makubwa katika ndoa yake na matatizo ya kifedha ambavyo vyote viliichanganya sana akili yake.

Na hivyo ikaonekana kuwa “She is not the type of defendant the court needs to send to prison immediately.”  Na akapewa kile kifungo kinachoitwa kisheria “suspended sentence” baada ya kukiri tuhuma zote. Ikimaanisha aliwekwa chini ya uangalizi mkali wa mahakama kwa muda wa miezi tisa.

Na wakati wa kutoa hukumu jaji John Dowse alimwambia mahakama itaweka kumbukumbu ya haya mashtaka, na kwamba ajue kuwa anarekodi hii maisha yake yote.

Hata hivyo baba mzazi wa wavulana hao alisikika akilalamika akisema “kama ingekuwa ni mwanaume ndiye kafanya mapenzi na msichana wa miaka 15 angefungwa hata bila kutia mashaka, lakini kwa sababu ni mwanamke ndo kafanya hivi kwa wavulana kaachiwa, she took advantage of both my son, mwanangu mkubwa alipomuacha akamrukia mdogo, alikuwa amepanga yote haya. Akamaliza kwa kusema “It was disgusting what she did.”

Haya kila kubwa lina Kubwa Lake, na hili ni miongoni mwa makubwa.
like page yetu kwa habari zaidi

MAAJABU YA DUNIA ! MTOTO WA MIAKA 5 ALIYEBEBA UJAUZITO NA KUJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NCHINI PERU.

World's Youngest MotherLINA akiwa amelezwa mara baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji.























LINA MEDINA
 
LINA AKIWA MJAMZITO.
  
LINA AKIWA NA MTOTO NA MMOJA WA MADAKTARI WALIOMFANYIA UPASUAJI NA KUJIFUNGUA MTOTO HUYO KATIKA KITANDA CHA WATOTO CHA MATAIRI MANNE.

LINA Medina aliyezaliwa tarehe 27 Sept. 1933, huko Ticrapo, mkoa wa Huancavelica, nchini Peru, anatajwa kua Mama mwenye umri mdogo kuwahi kutokea katika historia ya Ulimwengu.

Tarehe 14 Mei 1939 Lina akiwa na umri wa miaka 5 na miezi 7, alijifungua mtoto wa Kiume aliy

e mpa jina la Gerardo Medina.

Ilianzaje? 

Mwanzoni mwa mwezi Machi 1939 wazazi wa Lina ~ Tiburelo Medina na Victoria Losea waliamua kumpeleka Hospitali baada ya kuona tumbo likiongezeka kupita kiasi.

Wazazi wa Lina walidhani huenda ana uvimbe tumboni, lakini madaktari waligundua kua alikua ana ujauzito wa miezi 7. 

Dr. Gerardo Lozada aliamua kumpeleka Lina kwa wataalam zaidi nao wakathibitisha kua ni kweli alikua mja mzito.

Alizaaje ?.

Mwezi mmoja na nusu baada ya kupelekwa hospitali kwa mara ya kwanza, Lina alijifungua mtoto wa kiume kwa njia ya upasuaji, kutokana na njia yake ya uzazi kua ndogo. 

Upasuaji ulifanywa na Dr. Lozada, Dr. Busalleu, na Dr. Colareta.

Alivunja Ungo lini?.

Dr. Edmundo Escomel alitoa ripoti kamili juu ya kesi ya Lina kupitia jarida maalum la maswala ya kiafya na matibabu liitwalo La Presse MĂ©dicale. 

Ripoti hii ilibainisha kwamba Lina alianza kupata siku zake tangu akiwa na umri wa miezi 8, alitofautiana na ripoti ya awali iliyosema kua amekua akiona siku zake tangu alipokua na umri wa miaka 3. 

Ripoti hii pia ilisema kua Lina alianza kuota maziwa akiwa na umri wa miaka 4, alipofikisha miaka 5 nyonga yake ilikua imesha tanuka.

Alizaa mtoto gani ?.

Mtoto alizaliwa na uzito wa kilo 2.7 na alipewa jina la daktari wake Gerardo.

Gerardo alilelewa akijua kwamba lina ni dada yake lakini alikuja kujua ukweli akiwa na umri wa miaka 10.


Gerardo aliendelea kukua akiwa mtoto mwenya afya njema lakini alifariki mwaka 1979 akiwa na miaka 40 kwa ugonjwa wa mifupa ujulikanao kwa jina la kitaalam la Bone marrow.

Nani Baba wa mtoto ?.

Lina hajawahi kumtaja baba wa mwanae wala mazingira yaliyopelekea yeye kupata mimba. 

Dr. Escomel alipendekeza kwamba inawezekana hata Lina mwenyewe alikua hajui, na kusema kuwa hakutoa majibu yanayojitosheleza.

Tuhuma kwa baba mzazi: 

Hata hivyo Baba mzazi wa Lina alikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la Unyanyasaji wa kingono wa mtoto (Child Sexual Abuse) lakini aliachiwa baadae baada ya kukosekana ushahidi wa kutosheleza. 

Na hivyo basi Baba halisi aliyempa mimba Lina hakuwahi kujulikana.





Maisha ya Lina baadae:
Miaka kadhaa baadae Lina aliolewa na RaĂşl Jurado ambaye mwaka 1972 walipata mtoto wa kiume. 


Lina yupo hai mapaka sasa na anaishi maisha ya kimasikini huko Lima nchini Peru
like page yetu kwa matukio zaidi

Bodaboda ni sanaa Uganda

Katika barabara za jijini Kampala -mji mkuu wa Uganda-siku hizi kuna vitu ambavyo vimepambwa ambavyo si vya kawaida.
Kuna picha kubwa za michoro ya sanaa ikiwa juu ya pikipiki -maarufu kama Bodaboda.
Hii ni sehemu ya tamasha la sanaa la kisasa la michoro. Shabaha ya maonyesho haya ni kufichua maisha na sauti ambazo hazijawahi kusikika.

Wednesday 22 October 2014

MAENEO YA MAAJABU YA DUNIA

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets