Tunakuorodhoshea majengo saba marefu kuliko yote duniani. Dubai ndiyo
inabeba sifa ya kuwa na jengo lililopanda angani kuliko yote hapa
duniani.
7.Petronas Tower: Kuala Lumpur, Malaysia
Pia
hujulikana kama Petronas Twin Towers, minara pacha hii ndiyo majengo
pacha marefu zaidi duniani, yana urefu wa
futi 1,483na ghorofa 88.
Ujenzi wake kunako miaka ya 90, uliashiria ukuaji mkubwa wa uchumi wa
Malaysia na kuliingiza taifa hilo miongoni mwa mataifa yanayoibukia
kiuchumi duniani.
6.International Commerce Centre: Hong Kong, China
International Commerce Centre lina urefu wa futi 1,588, na jumla ya ghorofa 118. Ndilo jengo refu zaidi Hong Kong.
5.Shanghai World Financial Center: Shanghai, China
Shanghai
World Financial Centre lina nafasi za ofisi, mahoteli na paa maalum
lenye sehemu ya kuangalia mandhari na maduka kwenye ghorofa ya kwanza.
Lina urefu wa futi 1,614 na ghorofa 101. Pia lina paa maalum la
kuangalia mandhari lililoko juu zaidi duniani, futi 1,555 kutoka
ardhini.
4.Taipei 101: Taipei, Taiwan
Jengo
la Tapei 101 linanyanyuka futi 1,669. Lina ghorofa tano za chini y
ardhi na 101 kwenda angani. Ndilo jengo refu zaidi duniani lililojengwa
kwa kuzingatia ubora wa mazingira.Wakati wa sherehe za kitaifa, fashi
fashi huwashwa kwenye jengo hili.
3.One World Trade Center: New York, NY
Pia
hujulikana kama Freedom Tower, jengo hili lina urefu wa futi 1,776
feet, na lina ghorofa 104, na kulifanya kuwa refu zaidi katika mataifa
ya magharibi. Lilijengwa kufikia futi 1776 kama kumbu kumbu ya mwaka
ambao Marekani ilipata uhuru wake.
2.Makkah Royal Clock Tower Hotel: Mecca, Saudi Arabia
Jengo
linaitwa The Makkah Royal Clock Tower Hotel, lilijengwa katika jitihada
za kuubadilisha mji mtukufu wa Makkah kuwa wa kisasa zaidi. Lina sifa
kadhaa – ndiyo hoteli ndefu zaidi duniani, mnara wa saa ulioko juu zaidi
duniani, na pia saa kubwa zaidi duniani. Lina urefu wa futi 1,972 na
ghorofa 120.
1.Burj Khalifa: Dubai, United Arab Emirates
Jina
lake ni Burj Khalifa, awali likijulikana kama Burj Dubai, hili ndilo
baba na mama wa majengo kwa urefu duniani. Lina urefu wa futi 2,723 na
ghorofa 163. Kazi ya ujenzi ilichukua miaka mitano, na ilikamilika mwaka
2009 katikati ya Dubai.
No comments:
Post a Comment