Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi
siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine
iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea
sehemu mbalimbaliDuniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo hivyo kumuwezesha mtalii kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani umbali wa mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji.
LIKE PAGE YETU KWA HUFAHAMU ZAIDI
No comments:
Post a Comment