Jamaa wawili walikuwa wamekaa baa wanakata kinywaji (Mmmoja alikuwa mmarekani na mwingine muhindi) Jamaa wa kihindi kwa sauti ya kilevi akaanza kulalama "Huko home bhana wanadai wamenitafutia mchumba natakiwa nimuoe, wanadai ni wa huko kijijini kwetu. Mi nimekataa nimewaambia siwezi kumuoa mtu ambaye simpendi, kwahiyo nina bonge la msala wa kifamilia huko"

Mmmarekani akamuangalia akacheka, akapiga funda jingine akamwambia, unasema una matatizo? Ngoja nikupe stori yangu uone majanga yalivyo.

"Nilimuona mama mmoja mjane ambaye nilikuwa nampenda sana na akaja na watoto wake wawili kutoka kwenye ndoa yake iliyopita. Baada ya miaka kadhaa baba yangu akamzimia mtoto wa huyo mwanamke kwahiyo wakaoana (Hapo baba yangu akawa mkwe wangu na mi nikawa baba mkwe wake, sasa kimantiki yule binti ambaye alikuwa mwanangu sasa akawa mama yangu na mke wangu akawa bibi yangu. Kali kuliko zote ni pale nilipopata mtoto wangu wa kiume, akawa shemeji yake baba yangu. Sasa shughuli ni pale baba yangu na yule mwanangu walipopata mtoto wa kiume, maana sasa akawa mdogo wangu na upande mwingine akawa mjukuu wangu"

"Sasa we unaongelea majanga, angalia hapo mi nimekuwa baba mkwe wa baba yangu, nimemuoa bibi yangu, nimemzaa mdogo wangu nimekuwa mjukuu wa mimi mwenyewe"