Saturday, 27 June 2015
VIUMBE WA AJABU WAISHIO ANGANI! - 8
INASEMEKANA kuwa wanasayansi wa Kimarekani wameshatuma vyombo vya anga karibu kila sayari katika mfumo wetu wa sayari ili tu kutafuta namna ya kudhibiti nguvu ya UFO na hawa aliens ambao wametawala anga.
Baada ya kuzichunguza hizi sayari, wakaamua kuzifutilia mbali ila tu sayari ya Mars na pengine kwa kuwa wapo wanaoamini kuna uwezekano wa binadamu au viumbe wengine kuweza kuishi.
Data zinaonesha kuwa mwaka 1976, Marekani ilituma wanasayansi wawili kwenye sayari ya Mars. Kila mmoja alikuwa na chombo ambacho kingechimba ndani ya mchanga wa Mars na kuuchunguza kama kuna dalili yoyote ya binadamu au kiumbe kuishi. Hawakupata kitu chochote. Kwa ulinganisho, ikiwa utauchunguza mchanga kutoka kwa changwa tasa au tope lililoganda kutoka Antaktiki, utagundua kuna viumbe wamejazana huko. Mwaka wa 1997, Marekani ilituma wavumbuzi kwenda anga la Mars. Hawa wazururaji wa anga walichukua sampuli na kufanya utafiti mwingi. Walibainisha kuwa hakuna dalili ya maisha huko. Tangu wakati huo, kuna safari nyingi zimefanywa kwenda Mars. Matokeo kila mara yamekuwa ni yaleyale.
Jamaa hao wanabainisha kuwa kumekuwa na ugunduzi wa sayari mpya katika mfumo wa jua la mbali. Wengine wanapendekeza kuwa kuwepo kwa sayari nyingi kunathibitisha kwamba lazima kuwe na maisha mahali kwingine mbali na duniani ambako hawa viumbe wa ajabu wanatanua.
Ukweli ni huu kuwa kati ya hizi sayari zote hakuna ambayo imewahi kuthibitishwa kuwa inaweza kukidhi maisha ya binadamu. Umbali wa ajabu uliopo kati ya dunia na sayari hizi unafanya vigumu kuchukua uamuzi kuhusu uwezo wao wa kuishi humo. Tukijua kwamba ardhi pekee ndiyo inakimu maisha, wavumbuzi wanataka kwa vyovyote vile kugundua sayari nyingine katika jua lingine ya kuweza kuishi ili waunge dhana kuwa maisha yanajibika.
Kuna sayari nyingine nyingi nje ya zile zinazofahamika lakini kwa hakika hatujui vya kutosha kuzihusu ili kuthibitisha kwamba zinaweza kukimu maisha ya viumbe.
Biblia inasema nini kuhusu jambo hili? Ardhi na wanadamu ni wa ajabu katika uumbaji wa Mungu. Maandiko yanafunza kuwa Mungu aliumba ardhi kabla hata hajaumba jua, mwezi au nyota. Matendo Ya Mitume 17:24, 26 maandiko yanasema: “Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye kwa kuwa ni Bwana wa Mbingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono. Naye alifanya kila taifa la wanadamu kutoka katika mmoja wakae juu ya uso wa nchi yote, akiisha kuwawekea nyakati alizoziamuru tangu zamani na mipaka ya makazi yao.”
Kwanza, mwanadamu hakuwa na dhambi na kila kitu katika ulimwengu kilikuwa kizuri sana (Mwanzo 1:31). Mtu wa kwanza alipohasi (Mwanzo 3), matokeo yalikuwa ni shida za kila aina yote, ikiwemo ugonjwa na kifo. Hata kama wanyama hawana dhambi ya kibinafsi mbele za Mungu (wao si viumbe wa maadili), bado wanateseka na kufa (Warumi 8:19-22). Yesu Kristo alikufa kuondoa adhabu ambayo tulistahili ya dhambi. Wakati atakaporudi, ataiondoa laana ambayo imekuwa ikidumu tangu Adamu (Ufunuo 21-22).
Juu ya uumbaji, kwenye Warumi 8:19-22 imeandikwa kuwa viumbe vyote wanangoja wakati huo. Ni muhimu kutambua kwamba Kristo alikuja kufa kwa ajili ya mwanadamu na kwamba afe mara moja pekee (Waebrania 7:27; 9:26-28; 10:10).
Kama viumbe wote sasa wanateseka chini ya laana, maisha mengine mbali na ya duniani watateseka pia. Ikiwa ni kwa sababu ya pingamizi, ikiwa viumbe wenye maadili wanaishi katika sayari nyingine, kwa hivyo pia hao wanateseka na kama si sasa, basi siku nyingine, hakika watateseka wakati kila kitu kimetoweka kwa ile sauti kubwa na kila kitu kitayeyuka kwa ule moto mkali (2 Petro 3:10). Ikiwa hawakutenda dhambi, basi Mungu hatakuwa wa haki kwa kuwaadhibu. Lakini ikiwa walikwishatenda dhambi na Kristo angekufa mara moja (ambayo alifanya katika ardhi), basi wameachwa ndani ya dhambi zao, ambazo pia itakuwa kinyume na tabia ya Mungu ( 2 Petro 3:9).
like kwa habari zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment