Meneja
Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na
wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari za jijini Dar kuhusiana na
shindano kubwa lililoshirikisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika la
kuandika Insha na kuchora picha kuhusiana na mambo ya Anga linaloitwa
DStv EUTELSAT STAR AWARDS ambapo mshindi wake atapata nafasi ya kwenda
Paris nchini Ufaransa na wazazi wake kushuhudia namna safari ya kwenda
mwezini inavyofanyika kabla ya kumkaribisha Mwanaanga wa Kwanza Afrika
Kwenda mwezini Patrick Baudry ambaye atazungumza nao kuhusiana na uzoefu
wake kuhusiana na masuala ya Anga.
Barbara
amesema kwamba mshindi wa shindano hilolililodhaminiwa na
Dstv atatangazwa hapo kesho katika hafla maalum ya chakula cha jioni
itakayofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro.
Mwanaanga
wa kwanza kutoka Barani Afrika kwenda mwezini Patrick Baudry leo ametoa
mafunzo kwa wanafunzi shule za Sekondari za jijini Dar es Salaam juu ya
mpangilio mzima wa safari ya kwenda mwezini na kurudi tena duniani.
Baudry
ametoa mafunzo hayo katika ukumbi wa Nkurumah ikiwa ni semina maalum
kwa wanafunzi wa shule za sekondari hapa nchini ambao wameshiriki kwenye
shindano kubwa la kuandika Insha na kuchora picha kuhusiana na masuala
ya Anga. Baudry mwenye umri wa miaka 66 ni mzaliwa wa Cameroon.
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Hindu Mandal.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Jangwani wakitega sikio kwa umakini.
Baadhi
ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakimsikiliza kwa makini
Mwanaanga Patrick Baudry (hayupo pichani) aliyezungumza na wanafunzi wa
Shule za Sekondari katika Ukumbi wa Nkuruma wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam leo.
Patrick Baudry akijibu maswali aliyokuwa akiulizwa na wanafunzi hao. Kulia ni Barbara Kambogi.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Jangwani akiuliza Swali kwa Mwanaanga Patrick
Baudry (hayupo pichani) wakati akizungumza na Wanafunzi jijini Dar es
Salaam leo.
Baadhi ya Walimu wa shule mbalimbali nchini waliombatana na wanafunzi wao.
Patrick Baudry akitia saini Autograph za Wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu.
No comments:
Post a Comment