Mto Kiwira unazidi kupanda chati kuliko mito mingine wilayani humo kutokana na kuwapo kwa Daraja la Mungu.
Lakini pia karibu na daraja hilo yapo maajabu
mengine yakiwamo ya chekeche la uchafu unaokusanywa na maji kabla ya
kuingia eneo maarufu la Kijungu.
Kijungu nayo ni sehemu ya Mto Kiwira, ni eneo la
ajabu kwa sababu mwamba wake umeumba kitu kama chungu kinachopokea maji
yote na kuyapeleka chini bila kupitisha juu ya mwamba.
Inaelezwa kwamba mtu anayetaka kuvuka salama
kwenye mwamba juu ya Kijungu kutoka upande wa Mashariki lazima atumie
mguu mmoja wa kulia na akitokea Magharibi atumie mguu wa kushoto tu ili
asitumbukie.
Maajabu mengine ni kuwapo kwa taarifa zinazodai
mtu akizama kwenye mto huo, lazima afuatwe mzamiaji mmoja aliyerithi
kazi hiyo kutoka kwa aliyekuwa kiongozi wa kimila na kwamba bila huyo,
aliyezama hawezi kuonekana mpaka siku saba zitakapopita.
Lakini jambo kubwa linaloonekana na kustaajabisha
ni kuwapo kwa daraja linaloaminiwa na wakazi wa eneo hilo na wilaya
nzima ya Rungwe kwamba lilitengenezwa na Mungu kwenye eneo la Mto
Kiwira unapotenganisha Vijiji vya Lugombo kwa upande wa Mashariki mwa
mto huo na kile cha Mboyo kilichopo Magharibi.
like page yetu kwa habari zaidi
like page yetu kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment