Pages

Friday 24 October 2014

Vituko vya mwishoni mwa wiki, achana talaka




Tuesday, June 07, 2011 11:19 AM
KATIKA hali ambayo haijazoeleka katika jamii, mwanamke mmoja [jina kapuni] [26] ameshangaza wanafamilia kwa kuchana talaka iliyoandikwa na mume wake mara baada ya kukabidhiwa na mumewe huyo.
Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe kwa kile kilichodaiwa kuvunja moja ya amri alizopewa na mume huyo wakati wanaingia katika mkataba kabla ya kufunga ndoa yao.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe akiwa mkoani Pwani katika moja ya sherehe za unyago mkoani humo.

Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo aliondoka jijini Dar es Salaam akimuaga mumewe huyo kuwa anaenda kwenye sherehe ya harusi ya moja ya ndugu zake katika ukoo wake kama mbinu ya kuruhusiwa na mume wake.

Imedaiwa awali mume huyo kabla hajamuoa mwanamke huyo walikubaliana kuwa mkewe asiwe anahudhuria shughuli za ngoma za unyago zinazopendelewa kufanywa mara kwa mara katika familia yao ikiwa ni kuenzi utamaduni endelevu wa kabila hilo. Walioana mwaka mmoja uliopita baada ya kuafikiana masharti hayo.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo aliweza kuvumilia kutohudhuria shughuli hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na kudaiwa kupata malalamiko kutoka kwa ndugu zake kuwa ametengana na familia kwa kuwa hahudhurii shughuli hizo na ilidaiwa kuwa familia yake ilitishia kumtenga iwapo hatakuwa akihudhuria sherehe hizo.

Mwanamke huyo alimdanganya mumewe na kumuomba ruhusa kuhudhuria moja ya harusi kumbe alikuwa anakwenda kuhudhuria shughuli hizo za kitamaduni ambazo mume wake huyo alimpiga marufuku.

Mume huyo alifanya uchunguzi na alibaini kuwa hakukuwa na shughuli ya ndoa bali kulikuwa na shughuli ambayo hapendi mke wake ahudhurie na alimpiga marufuku kuhudhuria.

Imedaiwa mume huyo alipandwa na jazba na aliandika talaka moja apelekewe mkewe.

Mkewe alipokabidhiwa talaka hiyo aliichana hadharani na akidai hakuna kosa alilolifanya na aliendelea na shuhguli zake zilizompeleka huko na kudaiwa atarudi nyumbani kwake leo.
Kitakachoendelea mtafahamishwa
   

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets