Mtoto huyo aliyezaliwa Julai 16 mwaka huu, licha ya kuzungumza, pia amekuwa kituko kutokana na kutaka aitwe majina matatu ya Glory, Halima na Upendo, pindi anapoitwa na mtu yeyote akitaka kumsalimia.
Akizungumza mama wa mtoto huyo Bi Rosemary Mhina , mkazi wa mtaa wa Bin Seif, wilayani Muheza, alidai kuwa mtoto wake huyo ni wa ajabu kwani tangu akiwa mjamzito wa miezi saba, alikuwa akilia tumboni.
"Kwanza nilipokuwa na mimba, tumbo lilikuwa linaniuma sana, nilipofikisha miezi saba tumbo likiniuma, utamsikia mtoto analia timboni, nikaenda hospitali, nilianzia Teule, nikaja huku Bombo na Tumaini, nilipopigwa 'ultra sound' madaktari wakanieleza kuwa nitajifungua mtoto wa kiume, waliyemwona tumboni kwa kifaa hicho," alisema Bi Rosemary Mhina.
Akielezea zaidi kuhusu namna alivyobaini mtoto wake kuwa na mawasiliano na watu, mama huyo alidai kuwa mara baada ya kuzaliwa alipofikisha miezi miwili, siku moja alilia sana wakati akimbembeleza "Nyamaza mwanangu usilie ngoja nikupe maziwa"
Alisema baada ya kumweleza hivyo, mtoto huyo alitamka maneno yaliyomtisha mama yake huyo: "Mama usione nalia, nalizwa na mengi, kwanza baba alitaka uniue nikiwa tumboni, halafu maisha yako si mazuri mama nakuonea huruma"
Bi Rosemary alikiri kwamba baada ya kupata ujauzito kutoka kwa mwanaume(Jina limehifadhiwa) ambaye amedai kwamba anafanya kazi katika hospitali ya Mount Meru Arusha, alimpa sh.30,000 ili akaitoe hospitalini wakati mimba hiyo ilipofikisha miezi sita.
"Yule baba alitaka nikatoe mimba ya mtoto huyu nikakataa, hata hivyo wazazi wangu hawakutaka mimi nizae baada ya kuwa na watoto wawili, niliogopa pengine ningefanya hivyo ungekuwa mwisho wangu", alidai Rosemary.
Aliendelea kudai kuwa tangu mwanawe huyo awe naye amekuwa akitokewa na miujiza mingi na kipindi alichoanza kuzungumza, alimpeleka kwa wachungaji mbalimbali ili kumwombea, lakini kila anapokwenda huko akirudi anatokewa na vituko.
"Kipindi kimoja nilimpeleka kuombewa, usiku niliona paka wengi ndani nilimolala wakaniparua huku mwanangu Upendo akinicheka", alidai.
Mambo makubwa hayo je ingekuwa wewe ungefanyaje?
No comments:
Post a Comment