Pages

Wednesday 30 July 2014

FIFA inachunguza ubaguzi wa rangi

FIFA yaanzisha Uchunguzi kuhusiana na Ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa Manchester City
Fifa imeanzisha uchunguzi kubaini ukweli wa madai ya mchezaji wa Manchester City kuwa alidhulumiwa kutokana na rangi yake timu hiyo ilipokuwa Croatia.
Shirikisho hilo la soka duniani linaendeleza uchunguzi huo kufuatia madai ya Seko Fofana, 20, kuwa alidhihakiwa walipokuwa wakishiriki mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.

Msemaji wa FIFA ameiambia BBC kuwa wanakusudia kutafuta suluhu ya tukio lililompelekea kocha wa City Patrick Vieira kuwaondoa wachezaji wake uwanjani.Wakati huohuo shirikisho hilo limeiagiza shirikisho la soka la Italia kuanzisha uchunguzi dhidi ya ,Carlo Tavecchio ambaye anatuhumiwa kwa kutamka maneno ya kuwadunisha wachezaji wenye asili ya Afrika.
Kwa upande wake shirikisho la kandanda la Croatia limeanzisha uchunguzi wake.
Msemaji huyo alisema kuwa mwenyekiti wa jopo la kuchunguza dhulma kwa misingi ya rangi Jeffrey Webb anafuatilia kwa karibu matukio hayo.
Credit: BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets