Pages

Wednesday 30 July 2014

Toure: nataka kusalia Etihad


Yaya Toure anataka kusalia Etihad kwa miaka zaidi.
Kiungo cha kati wa Ivory Coast na Manchester City ya Uingereza Yaya Toure amesema kuwa angependa kusalia Etihad milele.
Awali ripoti zilikuwa zimeashiria kutoridhishwa kwake na jinsi anavyothaminiwa na wamiliki wa klabu hiyo bingwawa ligi kuu ya Uingereza.
Lakini sasa Toure anasema kuwa swala wakati huo halikuwa uhamisho bali ilikuwa ni utatuzi swala ibuka.Wakala wake Dimitry Seluk,alikuwa amenukuliwa akidai kuwa Toure alikuwa anahisi kutelekezwa na wenye klabu.
Seluk alikuwa amesema kuwa wamiliki wa klabu hiyo walipuuza Toure siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake mwezi mei timu hiyo ilipokuwa ziarani katika Milki za Kiarabu .
Man City ilikuwa UAE kusherehekea ushindi wa ligi kuu ya Premia ya Uingereza.
Wakati huo Toure alidhaniwa kutilia pondo matamshi ya wakala wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter alipodai kuwa hakujuwa ataichezea klabu ipi msimu huu.
Yaya Toure angependa kusalia Etihad
Seluk aliiambia BBC Yaya angefurahia kukaa Etihad milele.
Sasa Toure mwenyewe amepuzilia mbali dhana kuwa alikuwa anapanga kuondoka Etihad akisema kuwa sasa anataka kusalia huko kadri anavyoweza.
Toure, ambaye alitia sahihi kandarasi ya miaka minne mwaka uliopita anapendekeza kusajiliwa kwa wachezaji wengine wapya ilikuimarisha klabu hiyo.
''ikiwa tunataka kuwa klabu yenye sifa lazima nasi tushinde mataji yote''

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets