Pages

Saturday 16 August 2014

Kutana na nyumba ndogo

Kichekesho cha Jamaa Mmoja na Nyumba Ndogo
Kuna jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa na mke mdogo kwa siri katika jiji la Ar. Siku moja katika kutenga muda wa kutosha wa kujirusha na bi mdogo jamaa kapanga safari ya kikazi na kumuaga mke wake kuwa anakwenda Dar kikazi wiki nzima. Kumbe huku nyuma alipanga kutanua na bi mdogo.
Baada ya starehe za usiku wa jana yake na bi mdogo huyo, jamaa akiwa ofisini aliamua kumtumia meseji ya kushukuru bi mdogo
Jamaa katuma meseji hii:
“Asante baby kwa staili ya jana, ilikuwa kali sana na nimeipenda. Ndio maana nakupenda wewe kuliko wanawake wote duniani” na kuituma.
Baada ya kutuma jamaa kagundua kakosea namba na ilienda kwa waifu, yaani kwa mke wa ndoa
Jamaa katika kuhaha kuzuia meseji isimfikie mke wake alikwenda kwa wahudumu wa VodaCom ili kuomba msaada wa kuzuia meseji na mazungumzo yakawa hivi:
Jamaa: Kuna meseji nilikuwa niitume kwa bi mdogo kwa bahati mbaya imekwenda kwa waifu wangu, je mnaweza kuizuia?
Mhudumu: Wahi kwenye mnara
like page yetu hapa

like page yetu hapa

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets