Pages

Friday 1 August 2014

MWANAUME ALIYELAZWA WADI YA WANAWAKE

Na Makongoro Oging'
MAAJABU zaidi yamebainika kuhusu kijana wa kiume, Karina Mohamed ‘Natalia’, 20, aliyelazwa wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke.
Karina Mohamed 'Natalia' enzi za uhai wake.
Karina, alilazwa wodi ya wanawake akidhaniwa ni mwanamke kwenye Hospitali ya Amana ambayo ina hadhi ya mkoa kitabibu, Ilala, Dar es Salaam, kabla ya kugundulika akiwa chumba cha maiti baada ya kufariki dunia.
Pamoja na habari hiyo ya Karina kuandikwa kwenye gazeti ndugu na hili la Risasi Jumamosi, toleo namba 1005 la Mei 4, mwaka huu, Uwazi limebaini maajabu yaliyofanya alazwe wodi ya wanawake kwa siku mbili bila kugundulika.

MAAJABU YA KWANZA; SURA
Timu ya gazeti hili imebaini kuwa sura ya Karina, haina tofauti yoyote na ya mwanamke.
Uwazi limepata ushahidi wa picha za Karina, enzi za uhai wake na kujiridhisha kwamba sura ya kijana huyo ilikuwa na sifa nyingi za kike kuliko za kiume.
MAAJABU YA PILI; UMBO
Kupitia picha ambazo alipiga akiwa amevaa nguo za kubana, imebainika kuwa Karina ambaye ana asili ya Kiarabu, alikuwa ameumbika kwa sifa nyingi za kike.
Consolata Temu, 26, aliyemfahamu Karina enzi za uhai wake, alisema: “Niwe mkweli, yule jamaa aliumbika kike kuliko wanawake wengi sana. Mimi mwenyewe niliwahi kumwambia kwamba ningeumbika kama yeye ningeringa sana.”
Akaongeza: “Hipsi za Karina ni za kike zaidi. Nimewahi kukaribiana naye na kufanikiwa kumshika, yule jamaa alikuwa na mwili laini mpaka unaweza kujiuliza alikuwa anakula nini. Maana ni mwanamke kabisa.”
Karina Mohamed 'Natalia' akiwa katika hospitali ya Amana.
MAAJABU YA TATU; SAUTI
Imeelezwa kuwa Karina alikuwa na sauti nyembamba kiasi kwamba kila aliyezungumza naye, aliamini ni mwanamke mpaka yeye
mwenyewe alipoamua kueleza.
“Akinyamaza utaondoka na imani kwamba umekutana na mwanamke. Wanaume wengi walimtongoza kwa kuamini ni mwanamke. Ukizingatia ni mzuri sana.”

MAAJABU YA NNE; KIFUA
Imebainika kuwa wauguzi kwenye Hospitali ya Amana, walishindwa kubaini kuwa Karina ni mwanaume kwa sababu kifua chake, japo hakina matiti lakini kimekaa kama cha mwanamke.
  Muuguzi mmoja (jina tunalo), alisema: “Sisi tulijua maziwa yake ni madogo, maana alivyo ni mwanamke mtupu. Tulishangaa sana kujua ni mwanaume, maana ni mzuri kuliko hata sisi wengine hapa.”

MAAJABU YA TANO; TUMBO
Muunguzi huyo alisema: “Kuna kipindi wakati wa kumhudumia, tulipandisha nguo na kumpima tumbo. Sijawahi kuona tumbo la mwanaume likiwa laini vile. Lile ni tumbo la kike. Huo ndiyo ukweli, kwa kweli hilo lilikuwa tukio la kwanza kuliona.
“Mtu mwenye sifa zote za kike, baadaye kugundulika ni mwanaume, nilishangaa sana.”

MAAJABU YA SITA; NYWELE
Kwa mujibu wa muuguzi, Karina alifika hospitalini hapo akiwa na nywele ndefu ambazo ziliwekewa dawa, kufanana kabisa na za mwanamke.
“Hakuna anayeweza kutulaumu kabisa katika jambo hili. Hata angekuwa nani, asingekubali kama yule ni mwanaume. Hata aliyegundua baadaye ni baada ya kumuona jinsia yake wakati alipovuliwa nguo,” alisema.
Ukweli kuhusu nywele, vilevile unajidhihirisha katika picha zake enzi za uhai wake, zinazomwonesha akiwa ametengeneza nywele katika mitindo mbalimbali ya kike.

MAAJABU YA SABA; NYETI
Rafiki wa Karina, aliyeomba hifadhi ya jina lake gazeti, alisema: “Yule jamaa alikuwa na ‘umbile’ dogo sana ambalo hakulifurahia. Kitendo cha kuwa na ‘umbile’ hilo, aliona mkosi, ndiyo maana alikata tamaa, moja kwa moja akaamua kujishughulisha na mapenzi ya kinyume na maumbile.
“Alijishughulisha na vitendo vya ushoga na hili linafahamika kwetu sisi tuliokuwa watu wake wa karibu na ndiyo maana alikuwa na vitendo vingi vya kike na alichukia kuitwa mwanaume.”

KUZIKWA NA JIJI
Habari zinasema kuwa Karina ni raia wa Kenya, mwenye asili ya Jiji la Mombasa, Uwazi limebaini kuwa mpaka sasa hakuna ndugu aliyejitokeza kumtambua.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi, Ilala, Dar es Salaam, Marietha Minangi, alisema: “Hakuna ndugu aliyejitokeza, endapo zitapita siku saba kabla ya ndugu kujitokeza, basi atazikwa na jiji. Siku saba zinahesabiwa kuanzia pale alipofariki dunia.”



No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets