Tata Nano |
Monday, March 23, 2009 5:52 AM Shirika la kutengeneza magari la Tata Motors la India linatarajia kuzindua gari lake jipya litakalouzwa kwa bei rahisi kuliko magari yote duniani likiwa na uwezo wa kubeba watu watano. |
||||||||||||||||||||||||||||
Tata
Motors wanategemea kuzindua gari lao jipya litakaloenda kwa jina la
Nano lenye urefu wa mita tatu na lenye uwezo wa kubeba watu watano. Nano litazinduliwa jijini Mumbai leo jumatatu likiwa tayari kwa wateja watakaoweza kutoa dola 1,979 sawa na takribani shilingi za Tanzania milioni mbili na nusu. Shirika la Tata lilisema kuwa gari hilo litawawezesha watu wasio na uwezo kuweza 'kutembea wakiwa wamekaa' kwenye gari hilo la matairi manne kwa mara ya kwanza. Gari hilo lina milango minne na siti tano na lina injini kwa nyuma yenye 33bhp, 624cc. Hata hivyo gari hilo halina airbags, kiyoyozi na radio. Tata Motor imetoa gari hilo kama njia ya kujiokoa kutokana na madeni na kujiokoa kufilisika kutokana na kupungua kwa mauzo ya magari yake. |
Monday, 25 August 2014
Tata Wazindua Gari la Bei Rahisi Kuliko Yote Duniani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment