Pages

Thursday, 19 March 2015

Norway Nchi Bora Kuishi duniani, Tanzania ya 151



NewsImages/3280494.jpg
Vivutio vya Norway
Nchi ya Norway ndiyo nchi bora kuliko zote duniani kutokana na maisha bora huku Niger ndio nchi choka mbaya kuliko zote duniani wakati Tanzania inashika nafasi ya 151 kati ya nchi 182 duniani.
Norway imeendelea kushika nafasi ya kwanza kama nchi yenye maisha bora kuliko nchi zote duniani na watu wengi wangependa kuishi nchini Norway kutokana na vivutio mbali mbali, ilisema taarifa ya shirika la maendeleo la Umoja wa mataifa UNDP.

Nchi ya Niger ambayo imeathirika zaidi na vita na balaa la ugonjwa wa ukimwi, ndiyo inayoshika mkia katika nchi zote duniani.

Takwimu za matokeo haya zilichukuliwa mwaka 2007 kabla ya msukosuko wa mfumo wa fedha duniani kuanza.

Katika tatu bora kuna Norway, Australia na Iceland ambazo zimetajwa kuwa na maisha bora zaidi kuliko nchi zingine. Uingereza inashika nafasi ya 21 duniani.

Katika nchi tatu za mwisho kuna Niger inayoshika mkia ikifuatiwa na Afghanistan na Sierra Leone.

Takwimu hizo zilifanyika kwa kuangalia kipato cha taifa cha mwananchi, kiwango cha elimu na matarajio ya urefu wa maisha (life expectancy).

Kwa kuangalia kiwango cha kipato cha Mtanzania kwa mwaka, kiwango cha elimu yetu na matarajio ya umri wa kuishi wa Mtanzania, Tanzania inashika nafasi ya 151 duniani. Kenya inashika nafasi ya 147 wakati Uganda inashika nafasi ya 157.

Raia wa Niger anatarajiwa kuishi miaka 50 wakati raia wa Norway anatarajiwa kuishi miaka 30 zaidi yake.

Katika kila dola moja ambayo mtu mmoja nchini Niger anajipatia kwenye kipato chake, angekuwa nchini Norway angejipatia dola 85.

Wajapan ndio watu wanaoishi miaka mingi kuliko wote duniani, wanakadiriwa kuishi miaka 82.7 wakati waafghanistan ndio wanaoishi miaka michache kuliko watu duniani, hutarajiwa kuishi miaka 43.6 tu.

Katika nchi 10 zinazoshika mkia, nchi nyingi zaidi ni za Afrika. Nchi 10 zinazoshika mkia ni Guinea Bissau-173, Burundi-174, Chad-175, Jamhuri ya Congo-176, Burkina Faso-175, Mali-178, Jamhuri ya Afrika ya Kati-179, Sierra Leone-180, Afghanistan-181, Niger-182.
 LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets