Meneja
Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza na
wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari za jijini Dar kuhusiana na
shindano kubwa lililoshirikisha wanafunzi kutoka nchi zote za Afrika la
kuandika Insha na kuchora picha kuhusiana na mambo ya Anga linaloitwa
DStv EUTELSAT STAR AWARDS ambapo mshindi wake atapata nafasi ya kwenda
Paris nchini Ufaransa na wazazi wake kushuhudia namna safari ya kwenda
mwezini inavyofanyika kabla ya kumkaribisha Mwanaanga wa Kwanza Afrika
Kwenda mwezini Patrick Baudry ambaye atazungumza nao kuhusiana na uzoefu
wake kuhusiana na masuala ya Anga.
Barbara
amesema kwamba mshindi wa shindano hilolililodhaminiwa na
Dstv atatangazwa hapo kesho katika hafla maalum ya chakula cha jioni
itakayofanyika katika Hotel ya Hyatt Regency Kilimanjaro.