Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani ni Kiboko.
Kiboko ndiye mpaka sasa hivi anayeongoza duniani kwa kuwa na mdomo
mkubwa. Pia anaongoza kwa kupanua mdomo anapopiga miayo. Mdomo wake
unaweza kupanuka mpaka digrii 170 ambayo ni sawa na mstari ulionyooka
ukipungua kwa digrii kumi (10) tu.
Mnyama huyu anapatikana sehemu Ngorongoro, Ruaha, na sehemu zingine
za Afrika. Kiboko anaishi majini na Nchi kavu. Muda mwingi majini na
nyakati za jioni anatoka kwenda kutafuta malisho. Kiboko muda mwingi
anapenda kukaa kipweke na kiboko wa kiume ni mzito kuliko wa kike.
Kiboko anaweza kufikia tani 3 na kumfanya kuwa mnyama wa nchi kavu wa
tatu kwa uzito duniani baada ya Tembo na Kifaru. Kiboko pia ni mnyama wa
nchi kavu wa pili duniani kwa ukubwa baada ya Tembo. Kiboko anakula tu
majani na hivyo kuwa sawa na Ngombe, Mbuzi, Nyati, Swala, Pundamilia, na
jamii yote ya wanyama wannaokula majani tu.
like page kwa habari zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment