Pages

Monday 13 June 2016

Visiwa vya ajabu duniani: Kisiwa kilichojaa nyoka



Ilha de Queimada Grande au "Kisiwa cha nyoka" kipo yapata maili 90 hivi kutoka kwenye jili la São Paulo nchini Brazil.

Inakadiriwa kuwa wapo nyoka 2,000 wanaoishi katika kisiwa hicho chenye ukubwa wa meta za mraba 430,000 kwa hivyo kuna nyoka mmoja kila unapokaribia kumaliza meta za mraba kati ya moja hadi tano.

Katika kisiwa hicho ndipo anakopatikana pekee mmoja wa nyoka wenye sumu kali kabisa duniani, Golden Lancehead Viper (Bothrops insularis). Wataalamu wanasema sumu ya nyoka huyo ina nguvu karibu mara tano ya nyoka yeyote anayepatikana katika ardhi ya dunia kiasi cha kuweza kuyenyusha nyama ya mwili wa mwanadamu.

Nyoka hawa hupata chakula chao kutokana na kuwala ndege wanaohama hama na kufanya kisiwa hicho kuwa sehemu yao ya mapumziko bila kujua hatari inayowakabili.

Jeshi la Wanamaji la Brazili limepiga marufuku kwa yeyote kutua ama kutia nanga katika kisiwa hicho, isipokuwa tu kwa watafiti wa kisayansi wenye ruhusa maalum.

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets