Pages

Tuesday 12 August 2014

je wajua? Kampuni ya China yajipanga kujenga ghorofa refu kuliko yote duniani kwa muda wa siku 90 tu.


Kampuni moja nchini China inajiandaa kufanya ujenzi wa ghorofa refu kuliko yote duniani kwa muda wa siku 90 tu.
Kuanzia ujenzi wa msingi hadi kufikia juu, ujenzi mzima utafanyika ndani ya miezi mitatu kwa kiwango cha ghorofa tano kwa siku.
Ujenzi huo ni changamoto ambayo China pekee ndio inaweza kuifanya na kuwa ghorofa hilo litajengwa katika mji ambao watu wengi hawaufahamu wa Cha
ngsha katika Jimbo la Hunan.
Jengo hilo litaitwa Sky City na lina kuwa na urefu wa mita 838, ghorofa 220 na litakuwa limejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba milioni moja.
Katika kuwezesha ujenzi huo tani 200,00 za chuma zitatumika.
Ndani ya jengo hilo kuna nafasi ya kuwawezesha watu 31,000 kupanda na kushuka kwa kutumia lifti 104 ziendazo kwa kasi.
Asilimia 83 ya jengo hilo itakuwa kwa ajili ya makazi, yakiwa na vyumba vya kukaa watu 17,400.
Sky City litakuwa refu kuliko Burj Khalifa la Dubai.
Linakuwa na hoteli inaweza kukaa watu 1,000.
Kutakuwa na shule zitakazotoa elimu kwa mpaka watoto 4,600 na hospitali ambayo inaweza kutibu wagonjwa 1,400.
Asilimia 3 tu ya jingo hilo itakuwa kwa ajili ya matumizi ya kiofisi na zitakazobakia zitakuwa ni maduka na migahawa

usikose kulike page yetu hapa

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets