Pages

Saturday, 16 August 2014

Lampard atangaza kuachana na klabu yake ya Chelsea wakati mkataba wake utakapotamatika

  
Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard
Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard
Reuters

Na Emmanuel Richard Makundi
Kiungo mkongwe wa klabu ya Chelsea na timu ya taifa ya Uingereza, Frank Lampard ametangaza kuwa ataachana na klabu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake unaotarajiwa kutamatika mwezi June mwaka huu.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa alipewa mkataba mwingine ambao haukuwa wa muda mrefu lakini mwenyewe akaamua kutamatisha kandarasi yake mwisho wa mkataba wake.
Frank Lampard akishangilia na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Uingereza
REUTERS/Paul Hanna
Hatua hii inamfanya kiungo Frank Lampard kutamatisha kandarasi ya kuitumikia klabu yake baada yakuwa klabuni hapo kwa takribani miaka 13.
Kuna taarifa kuwa wakala wa mchezaji huyo amekuwa kwenye mazungumzo na viongozi wa timu ya New York City ya Marekani na kwamba huenda mchezaji huyo akahamia kwenye ligi ya Soka ya Marekani "Major League Soccer".
Vilabu zaidi ya kumi vinavyoshiriki ligi kuu ya nchini Uingereza vinaelezwa kutaka kumsajili mchezaji huyo ikiwemo klabu iliyoshuka daraja msimu uliopita QPR.
Lampard amefunga mabao 211 katika mechi 649 alizoichezea timu yake na kumfanya kuwa moja ya wachezaji maarufu wa klabu hiyo waliofunga mabao mengi zaidi kwenye historia ya timu hiyo.
Frank Lampard akishangilia bao na mchezaji mwenzake wa zamani Didier Drogba
Reuters
Lampard alijiunga na Chelsea mwaka 2001 wakati huo ikiwa chini ya uongozi wa mwenyekiti Ken Bates kabla ya kununuliwa na tajiri wa Urusi Roman Abramovich ambaye aliwekeza fedha nyingi na kuibadilisha klabu hiyo.
Akizungumza na wanahabari, Lampard anasema "wakati nilipowasili kwenye klabu hii miaka 13 iliyopita sikuwa na hakika ya kucheza mechi nyingi na kufurahia maisha kwenye timu hii na kupata mafanikio haya". Alisema Frank Lampard.
Wachezaji wenzake wa timu ya Taifa wamemuelezea Lampard kama mmoja wa wachezaji wakongwe na wenye uzoefu mkubwa na kuwa nae kwenye timu ya taifa ni wazi kunawapa faraja na kujifunza kutoka kwake.

like page yetu hapa

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets