JAMAA: "Dokta mimi nimekuja ninasumbuliwa na ndoto kila siku usiku nikilala naota Ngedere na Panya wanacheza mpira utanisaidiaje?"
DOKTA: "Kwa hilo tatizo lako ulilosema inabidi nikupe hizi dawa ukifika nyumbani uzimeze, ukizimeza kuanzia leo hauto ota tena ndoto hizo sawa!"
JAMAA: "Sawa dokta ila itabidi nianze kuzimeza kesho kwakuwa leo ndio Fainali nataka nijue nani atashinda katika mechi ya leo"
- Dokta alibaki anashangaa!


DOKTA: "Nimekupima nimekukuta unaumwa Kiharusi"
MGONJWA: "Ni kweli dokta ndio mana nilikuwa nina hamu sana ya kutaka kuoa! Kumbe naumwa kiharusi"
- Dokta alibaki anashangaa!


MWANANCHI 1: "Jamani huyu atakuwa anaumwa, tumpelekeni kwanza hospital"
MWANANCHI 2: "Mimi ninachoona tumpelekeni kwanza Polisi"
Ghafla ikasikika sauti ya Bibi mmoja akisema:-
BIBI: "Sikilizeni jamani Pengine ananjaa huyu hajala hebu mtu mmoja aende akamnunulie chips na soda ale"
Baada ya yule Bibi kusema vile mara yule mteja akainua kichwa na kusema:-
TEJA: "Jamani msikilizeni Bibi anavyosema"
Wananchi wote waliokuwa wamemzunguka wakaangusha kicheko mmoja wao akasikika akisema "KUMBE JAMAA ALIKUWA ANANJAA KISHAVUTA MI UNGA YAKE SASA UBAO UNAMCHARAZA" hahahaaaa!




No comments:
Post a Comment