Pages

Sunday 10 August 2014

cheka uongeze siku za kuishi

mwizi aliyependa kutubu

 
Padri amekaa katika ki-box cha kuungamisha,kanisani hakuna mtu. Mara muumini mmoja akaingia, akapiga magoti upande wa pili na kufanya ishara ya msalaba akaanza kuungama.

"Padri naungama dhambi zangu, leo nimefanya dhambi kubwa sana"

"Endelea...."
...
...

"Bosi wangu aliniita nyumbani kwake akaniambia amegundua nimeiba shilingi milioni 50, akasema nisipotoa maelezo ya kuitisha atanipeleka polisi. Sasa ukweli mimi naogopa kufungwa, nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikachomoa bastola nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"Utasamehewa... "

"Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango unafunguliwa, kutazama loh, mke wa bosi. Akaniuliza nimemfanya nini mume wake.Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu, nikamuua na yeye. Yesu atanisamehe na hiyo?"

"Utasamehewa... "

"Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke lakinimlinzi akakataa kufungua geti akasema amesikia kama kishindo hivi! Nikaona ananiwekea kiwingu. Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Yesu atanisamehe?"

"Utasamehewa... ."

"Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi akabisha hodi nikawaza mambo gani tena. Akasema amerudi nyumbani na kukuta yaloyotokea, lakini akanionyesha diary ya baba yake inayoonesha kuwa nilikuwa na appointment naye kabla hajafa. Nikamuuliza nani mwingine anajua, akasema ameanzia kwangu kisha atakwenda polisi.

Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke yetu nikamuua. Diary nikaichomamoto. Yesu atanisamehe na hilo?"

kimya........

"padri, Yesu atanisamehe kwa hilo?"

kimya.........

Jamaa kutazama kwenye kibox padri hayupo. Lakini kwenye kona moja akaona kabati la ngou za mapadri kama linatikisika. Kufungua akamuona padri kajificha katikati ya majoho anatetemeka.... .

"Sasa baba mbona umenikimbia?"
Padri kwa taabu akajibu...

"Nilitazama huku na huku nikagundua kuwa tuko wawili peke yetu........"
 
 
 
 
 
 

 Mdada mmoja mke wa mtu alikuwa akisumbuliwa sana na jamaa mmoja aliyekuwa akimtaka kila siku, hatimae akamwambia mumewe. Mume akamwambia mkewe, we kubali tuu, ila mwambie aje mlale hapa kwetu, mi ntajificha uvunguni na panga. Akisha ingia ukiona kamaliza kuvua nguo we ning’iniza mkono anza kuuchezesha, mi nikiuona ntatoka uvunguni na kumfunza adabu.
Mdada akafuata masharti ya mumewe na hatimae wakaingia chumbani na yule bwana , mumewe akiwa tayari na panga uvunguni mwa kitanda. Jamaa alipovua shati, mke alishangaa kuona ana makovu makubwa kifuani na mgongoni;
MKE: Heee mbona una makovu hivyo??
...
JAMAA: Niwe mkweli tuu, kwako dia!! mie nina tatizo sana la kupenda wake za watu, waume wengi wamekuwa wakipanga kunifumania, nilishafumaniwa mara kumi na tisa, na wote walionifumania niliwaua. Ila jaribio la mwisho nilidakwa na mapolisi nikatumikia kifungo cha miaka 27 jela, Lakini ninavyopenda wake za watu sitaacha kuua. Hivi sina muda tangu nitoke huko jela hivyo nina ukame wa punda na nilipokuona moyo wangu ukakudondokea. Na nitatulia na wewe.
MKE: Heee! Haiwezekani jamani!!….jamaa akaendelea kuvua nguo alipomaliza mdada akaanza kujitahidi kuning’iniza mkono ili mumewe atoke uvunguni aje kumuokoa, mume akabana kimya, kila mdada akijitihadi kupunga mkono hakupata jibu, mdada akalalamika mpaka jamaa akamaliza shughuli zake akatokomea.
MKE: Huku akilia, ndio nini umenifanyia? Mbona hukutoka??
MUME: We we we, Weeeee mama naniii!!.. mwenyewe umesikia keshaua 19 ulitaka niwe wa ishirini?


  • MUME; baada ya kuoa ikawa anamwambia BI~HARUSI mke wangu! Nina Mambo 2 ya Kufurahisha na Kuhuzunisha je nianze Kukwambia lipi?
    MKE: Anza la Kufurahisha
    MUME: Akamuonyesha Uume wake; "Akamwambia umeuona MUZIKI huu ni Inchi~11
    ...
    MKE: Akafurahi ikamtoka WAOW! akalibusu kwenye kichwa MWAAaa.. Akasema~tena Haya~niambie la Kuhuzunisha
    MUME; Dude lote Hili lkn Halisimami;
    MKE; Akapoteza Fahamu!

    Kipofu kampiga mtu mpaka kamuua, akafikishwa mahakamani;

    HAKIMU: Kwanini umefanya ukatili namna hii

    KIPOFU: Mheshimiwa marehemu alisema mwenyewe,'Ukinipiga utaona', kwa vile nilikuwa na hamu kubwa ya kuweza kuona, nikajitahidi kumpiga sana ILI nipone, bahati mbaya kafariki.

     

     cheka na mr. been mchekeshaji wa kimataifa 


    jamaa alikuwa kwenye taxi akapita nje ya bar moja yenye guesthouse akamuona mkewe
    akipotelea ndani ya hiyo bar;
    JAMAA: Dreva simama. Unataka laki tatu ya chapchap?
    DREVA: Bila shaka mzee
    JAMAA: Mke wangu kaingia kwenye ile bar, picha yake hii, ingia mtoe tena
    umlete hapa ukiwa unamtandika vibao.......dreva akatoka na baada ya
    dakika chache akatoka anamburula mwanamke na makonde juu,
    JAMAA: Mbona umekosea huyo siyo mke wangu umeshaharibu mambo
    DREVA: Najua, huyu ni mke wangu, sasa ndio naenda kumtoa mkeo!!!
     
    like page yetu

    No comments:

    Post a Comment

     

    Blogger news

    Blogroll

    LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

    Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

    Powered By Blogger Widgets