Pages

Sunday 10 August 2014

Utani na mwanajeshi wamtokea puani

 

NewsImages/6615934.jpg

Wednesday, October 03, 2012 11:33 AM
MKAZI WA Mbagala Mission , Omari Nundo anaugulia maumivu akiwa kitandani hoi kwa kichapo alichokipata kutoka kwa jirani yake baada ya kumtania
Nundo ambaye amefika zahanati ya karibu kupata matibabu sasa anaendelea kuuguza maumivu baada ya kichapo hicho ambacho hakukitegemea kutoka kwa jirani yake huyo

Akiongea kwa masikitiko leo asubuhi, Nundo alibainisha kuwa, alipata kipigo hicho jana kutoka kwa jirani yake ambaye wanaishi nyumba za jirani ambaye hakutaja jina lake

Amesema kuwa, yeye na jirani yake walikuwa katika hali ya kutaniana kama ilivyo kawaida yao wanavyofanya lakini alishangazwa na kuona jirani yake huyo akianza kumpa kichapo cha nguvu na hatimaye kumpa maumivu yaliyomfikisha hospitalini kupata matibabu

Amedai kuwa kwa kawaida yeye na jirani yake huyo huwa wanataniana utani wa jadi ambapo kwa kawaida Tanzania kunakuwa na utani wa makabila kabila fulani hutaniana na kabila Fulani ambapo utani huo ulikuwepo tokea enzi za mababu zetu ndio walioturithisha

Amedai yeye ni myao kutoka kusini na jirani yake huyo ni Mngoni kutoka Ruvuma hivyo kiasili huwa ni watani wa jadi na huwa wanataniana mara kwa mara

Amebainisha kuwa, jirani yake huyo ni mwanajeshi, hivyo siku hiyo walianza kutaniana na yeye ndipo akamwambia “Mtani unaacha mke wako uliyejenga naye nyumba, unakwenda kuoa mwanamke mwingine huoni kama kitu kibaya hicho?

“Mke wako uliyehangaika nae kujenga nae hicho kibanda unamuacha unadanganyika na huyo mwanamke sio vizuri mtani” amebainisha jinsi utani huo ulivyokuwa

Mara baada ya kumaliza hayo jirani yake huyo ambaye kazi yake ni mwanajeshi aliona kama ameguswa na ghafla alianza kumpa kichapo mtani wake huyo bila huruma kwa kuona anaambiwa ukweli na siku zote ukweli huwa unauma

Hivyo Nundo alishindwa kujitetea na alipokea kipigo hicho cha nguvu sababu hakuweza kujitetea kwa kuwa jirani yake huyo alikuwa akimpiga kwa tikiniki za kijeshi

Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alipoendelea kumuhoji amebainisha kuwa, ni kweli mwanajeshi huyo ameacha mke wake na hivi sasa anatangaza ndoa na mwanamke mwingine

Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa hadi imepeleka Omari kuwa kitandani hoi kwa kipigo alichopata kutoka kwa jirani yake huyo ambacho hajakitarajia

Hata hivyo Nundo amesema hapo umeshaingia uhasama “na kama laiti mmoja wetu amepanga angehama lakini mbaya zaidi kila mtu amejenga mahali hapo, sijui wataishi vipi’ alijihoji mwenyewe



like page yetu

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets