Tata
Motors wanategemea kuzindua gari lao jipya litakaloenda kwa jina la
Nano lenye urefu wa mita tatu na lenye uwezo wa kubeba watu watano.
Nano
litazinduliwa jijini Mumbai leo jumatatu likiwa tayari kwa wateja
watakaoweza kutoa dola 1,979 sawa na takribani shilingi za Tanzania
milioni mbili na nusu.
Shirika la Tata lilisema kuwa gari hilo
litawawezesha watu wasio na uwezo kuweza 'kutembea wakiwa wamekaa'
kwenye gari hilo la matairi manne kwa mara ya kwanza.
Gari hilo lina milango minne na siti tano na lina injini kwa nyuma yenye 33bhp, 624cc.
Hata hivyo gari hilo halina airbags, kiyoyozi na radio.
Tata
Motor imetoa gari hilo kama njia ya kujiokoa kutokana na madeni na
kujiokoa kufilisika kutokana na kupungua kwa mauzo ya magari yake. |
No comments:
Post a Comment