Jibu:
Je, kuna Mungu? Ninaona ni jambo la kusisimua ya kwamba umakini mwingi
umepawa mjadala huu. Katika takwimu zetu hivi sasa zasema ya kuwa zaidi
ya asilimia 90 ya watu duniani wanaamimi kuweko kwa Mungu au Mamlaka ya
kiwango cha juu. Jukumu linabaki kwa wenye kuamini kuthibitisha ukweli
wa kuweko kwake. Mimi nafikiri ingewapasa wale hawaamini
watuthibitishie.
Kuweko kwa Mungu hakuwezi kutothibitishwa wala kuthibitishwa. Bibilia
inasema inatupasa kukubali kwa imani kuwa Mungu yuko, “Na pasipo imani
haiwezekani mtu kumpendeza Mungu, kwa kuwa kila ajaye kwake sharti
aamini kuwa yuko na ya kuwa huwapa vitu wale wamtafutao kwa bidii”
(Waebrania 11:6). Kama Mungu alingetaka iwe, angejitokeza tu mbele ya
ulimwengu wote kuwajulisha wote kuwa yeye yuko. Lakini, angefanya hivyo
hakungekuwa na haja ya imani. “Tena Yesu kamwambia, ‘kwa kuwa umeniona,
umeamini; heri wale ambao hawakuniona na wameamini” (Yohana 20:29).
Hiyo haimaanishi ya kuwa hakuna idhibati ya kuweko kwa Mungu. Biblia
inasema, “Mbingu zatangaza utukufu wa Mungu; anga zatangaza kazi za
mikono yake. Siku baada ya siku zamimina hotuba zake; usiku baada ya
usiku zaonyesha ufahamu. Hakuna hotuba au lugha ambayo haisikiki. Sauti
zao hutapakaa duniani kote, maneno yao mpaka mwisho wa dunia” (Zaburi
19:1-4). Ukitazama nyota, ukijaribu kufahamu kina cha anga, na kutazama
maajabu ya kiasili, huku ukiona urembo wa kutua kwa jua - haya yote
yanaashiria kuweko kwa Mungu muumbaji. Kuna ushahidi wakuweko kwa Mungu
ndani ya mioyo yetu. Mhubiri 3:11 inatuambia, “….ameweka pia umilele
ndani ya mioyo ya wanadamu…” Kuna kitu ndani yetu kinachotujulisha ya
kuwa kuna kitu zaidi baada ya maisha haya tunayoishi na mwingine zaidi
yetu nje ya dunia hii. Hata tukipuuza bado kuna uwepo wa Mungu maishani
mwetu. Biblia inatuonya ya kuwa kuna wengine watakuwapo watakaokataa
kuwepo kwa Mungu, “Mjinga amesema moyoni mwake hakuna Mungu” (Zaburi
14:1). Kwa kuwa zaidi ya asilimia 98 ya watu wa tamaduni mbali mbali
katika vizazi vilivyopita ndani ya mabara yote duniani ni waumini wa
kuwepo kwa Mungu wa aina Fulani – lazima kuwe kuna mtu ama kitu Fulani
kinachohisi na kusababisha imani hii.
Kuongezea, kuna maoni mbali mbali ambayo hutumika kuthibitishia pia.
Maoni ya kwanza yasema kwa kuwa Mungu ni kile ambacho zaidi yake hakuna.
Basi uwezekano wa kuwepo kwake ni mwingi. Na kama Mungu hayuko basi
hakungekuwa na ambacho zaidi yake hakuna. Maoni ya pili ni kwamba kwa
kuwa ulimwengu unaonyesha kazi nzuri ya ustadi iliyofanyika basi lazima
kuweko na aliyeifanya. Kila kitu kina fanya kazi vyema kwa wakati wake
na kwa kipimo mwafaka. Kama hewa yetu ingeharibika tu kidogo viumbe
vyote vingekufa.
Maoni ya tatu ni kwamba kwa chochote kufanyika lazima kuweko na mwenye
au chenye kusababisha. Kwa vile ulimwengu upo lazima kuwe na
aliyeusababisha uweko na huyo ndiye Mungu. Maoni ya nne ni kwamba katika
kila utamaduni, mila na desturi za watu duniani kuna aina Fulani ya
mfumo wa sheria ya kuelekeza; yenye kutambua mema na mabaya. Kuua,
uongo, wizi na uchafu wa kitabia ni mambo yanayokataliwa ulimwenguni
kote. Hali hii ya kutambua meme na mabaya ilitoka wapi Kama si kwa Mungu
Mtakatifu?
Biblia inatuambia, watu watakataa ukweli wa kuweko kwa Mungu na kuamini
roho za uongo. Warumi 1:25 inasema, “walibadilisha ukweli wa Mungu na
kutumikia uongo hata kuiabudu na kuitumikia miungu waliyoiumba kwa
mikono yao kinyume na Mungu aliyewaumba –ambaye daima husifiwa. Amina.”
Biblia pia inasema, watu hawana sababu ya kutomwamini Mungu, “Kwa kuwa
tangu kuumbwa kwa ulimwengu siri za uwepo wake – Nguvu zake za milele na
utisho wake umethibitika na kufahamika kutokana na yale aliyoyatenda
kwa hivyo wanadamu hawana kisingizio” (Warumi 1:20).
Watu husema hawamwamini mungu kwa sababu si kisayansi ama hakuna
kithibitisho cha kuweko kwake. Sababu halisi ni kwamba kwa kukubali
yuko,mtu anahitajika kuwajibika mbele zake na kuomba msamaha (Warumi
3:23; 6:23). Kama Mungu yuko basi tunawajibika kwa matendo yetu. Kama
hayuko, basi tunaweza kufanya mapenzi yetu wenyewe bila kujali hukumu.
Huenda ikawa hii ndiyo sababu ya watu wengine kushikilia mawazo ya kuwa
dunia ilifanyika tu kwa njia ya vitu tofauti tofauti kubadilika umbo
polepole kupitia mabadiliko ya kimazingira ili waepukane na ukweli wa
kuna Mungu muumbaji wa yote. Mungu yuko na kila mmoja anajua hivyo.
Mwenye kubishana ni mbishani tu lakini huwa hata yeye anajua yuko.
Je, nitajuaje kuwa Mungu yuko? Najua Mungu yuko kwa kuwa nazungumza naye
kila siku. Simsikii masikioni akinijibu lakini ninahisi uwepo wake,
nahisi kuongoza kwake, najua upendo wake ninatamani neema yake.Mambo
yaliyotendeka maishani mwangu hayana maelezo mengine ila Mungu. Mungu
ameniokoa kimiujiza na kuyabadilisha maisha yangu mpaka sasa nimebaki tu
kumtukuza. Maelezo haya yote hayawezi kumfanya mtu anayetaka kukataa
kuwepo kwa Mungu akubali. Muhimu ni kumkubali kwa imani (Waebrania
11:6). Imani kwa Mungu si bure kama kubahatisha gizani bali ni sawa na
kutembea salama ndani ya chumba chenye nuru ambamo asilimia 90 ya watu
waliomo wamesimama.
like page yetu ka habari zaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment