Pages

Monday 20 April 2015

Tazama chanzo cha Nyota


'''Nyota''' kwa lugha ya kawaida ni nuru ndogo zinazoonekana angani wakati wa usiku.

== Nyota ni magimba makubwa ==
Kwa kutumia darubini na vifaa vya kisasayansi imegunduliwa ya kwamba ni magimba makubwa sana katika [[anga la nje]] yanayong'aa kwa sababu yanatoa mwanga, joto na aina mbalimbali za [[mnururisho]] kutokana na [[myeyungano ya kinyukilia]] ndani yao. Lakini ziko mbali sana na kwa hiyo tunaziona kama nukta ndogo za nuru. Kwa jumla nyota zinaonekana kwenye anga kwa mpangilio usiobadilika na kila nyota huwa na mahali pake pasipobadilika kati ya nyota nyingine hata kama nyota kwa jumla zinazunguka angani juu yetu kila siku.

== Tofauti kati ya nyota zinazoonekana kwa macho ==
* Galaksi: Nyota kadhaa zinaonekana kwa darubini si gimba moja tu bali kundi la nyota mamilioni au hata mabilioni; kutokana na umbali kubwa zinaonekana kama nukta moja ya nuru. Makundi makubwa haya yanaitwa [[fungunyota]] kama idadi ya nyota iko chini ya milioni au [[galaksi]] kama ni kundi kubwa zaidi inayojitegemea.

* Sayari: Kati ya nyota zinazoonekana kwa macho kuna chache zinazobadilisha mahali angani polepole kati ya nyota nyingine. Zikihama zinafuata mwendo maalumu unaorudia kila mwaka. Nyota hizi zinaitwa [[sayari]]. Tangu kupatikana kwa [[darubini]] tunajua ya kwamba sayari ni gimba [[mango]] kubwa kama dunia yetu lenye umbo la tufe linalozunguka jua kwenye anga la ulimwengu. Kwa macho haiwezekani kutofautisha mara moja [[sayari]] na nyota nyingine. Kwa hiyo katika lugha ya kila siku sayari huitwa mara nyingi "nyota" ikionekana kwa macho. Lakini tangu milenia nyingi wataalamu waliotazama anga walijua kuna tofauti.

* Nyotamkia: Mara kwa mara yanatokea nyota mpya ambayo hayakuonekana siku kadhaa zilizopita. Hazikai mahali palepale angani lakini zina mwendo wa kila siku kati ya nyota nyingine hadi kupotea tena. Zikionekana kubwa huonyesha nuru ya pembeni kama mkia kwa hiyo huitwa [[nyotamkia]] au kometi. Hali halisi ni magimba mango yasiyo makubwa sana yanayozunkuga jua letu.

* [[Jua]] letu ni nyota iliyo karibu na [[dunia]] yetu tunapoishi ambayo ni [[sayari]] yake. Inaonekana kubwa kushinda nyota zote kwa sababu ni karibu. Uwingi wa nuru yake unaficha nyota nyingine wakati wa mchana. Imegunduliwa ya kuwa ni tufe kubwa sana yenye joto kali na kwa hiyo mada yake ni katika hali ya [[Utegili (fisikia)|utegili]] yaani kama [[gesi]] ya joto sana. Kipenyo chake ni zaidi ya kilomita milioni 1.3 na umbali wake nasi mnamo kilomita milioni 150. Kwa jumla karibu nyota zote tunazoona ni jua kama letu yaani magimba kubwa sana ya utegili wa joto. Jua letu ni kitovu cha [[mfumo wa jua]] pamoja na sayari, miezi yao, [[kometi]] na vumbi nyingi ambazo zinaizunguka.

== Elimu ya nyota ==
Habari za nyota zinakusanywa na kunfanyiwa utafiti na sayansi ya [[astronomia]]. Wanaastronomia wanatumia vifaa kama darubini kutazama nyota na kupima nuru yao. Kwa kutumia mbinu za sayansi ya [[fizikia]] inawezekana kutambua tabia nyingi za nyota ingawa ziko mbali sana.

Kuna pia [[unajimu]] ambao ni mbinu za kale sana nyingi lakini haufuati utaratibu wa kisayansi unajaribu kutabiri mambo yajayo kutokana na nyendo za nyota.

== Idadi ya nyota ==
Nyota zinazoonekana kwa macho wakati wa usiku ni kama 6000 lakini idadi yao hali halisi ni kubwa zaidi. Hakuna aliyeweza kuhesabu nyota zote; kuna makadirio ya kuwa idadi inaweza kufika 70,000,000,000,000,000,000,000.

== Galaksi na fungunyota ==
Nyota hupatikana angani katika makundi kama mawingu makubwa sana. Kundi kama hili huitwa [[galaksi]]. Galaksi yetu ikiwemo [[mfumo wa jua]] letu imekadiriwa kuwa na nyota zaidi ya 300,000,000,000. Tunaona sehemu za nyota zake angani zikionekana kama kanda la kung'aa linalojulikana kwa jina [[njia nyeupe]].

Kando la galaksi huwa makundi madogo zaidi yenye nyota mamia hadi malakhi yanayoitwa [[fungunyota]].

== Umbali kati ya nyota ==
Kutokana na umbali mkubwa kati ya nyota na nyota umbali huu hutajwa kwa kipimo cha [[mwaka wa nuru]]. Nyota jirani kabisa na jua letu inaitwa [[Alpha Centauri]] umbali wake ni 4.2 miaka ya nuru maana yake nuru yake inahitaji zaidi ya miaka minne hadi imefika kwetu. Kwa maana nyingine tunaiona nyota hii jinsi ilivyoonekana miaka minne iliyopita.

Galaksi ya jirani inayoitwa Andromeda ina umbali wa miaka ya nuru milioni 2.5. Maana yake mwanga wake unahitajia miaka milioni mbili na nusu mpaka kuonekana kwetu au kwa lugha nyingine tunaona galaksi ya Andromeda jinsi ilivyoonekana miaka hii milioni mbli na nusu iliyopita.
[[Picha:1996-04-a-web.jpg|thumb|300px|Nyota Betelgeuze ni pandikizi nyekundu; Kushoto: inavyoonekana kwa darubini; kulia: Betelgeuze ni nyota angavu juu kushoto kwenye [[kundinyota]] ya [[Orion]] mara nyingi huonekana nyekundu kwa macho matupu]]
== Maisha ya nyota ==
[[Fizikia]] na [[astronomia]] zimegundua ya kwamba nyota hazidumu milele bali zina mwanzo na pia mwisho. Kutokana na tabia hii wataalamu mara nyingi huongea juu ya "maisha", "kuzaliwa" na "kufa" kwa nyota ingawa si viumbehai.

Nyota zinaanzishwa katika [[nebula]] au katika mawingu makubwa ya gesi kwenye anga la ulimwengu. Kama wingu ambalo sehemu kuwa yake ni [[hidrojeni]] ni kubwa sana inaanza kujikaza kutokana na graviti yake. Katika muda wa miaka mioni 10-15 wingu linajikaza kuwa tufe kadhaa kubwa na ndani ya tufe hizi halijoto inazidi kupanda. Kadiri jinsi gesi inajikaza nguvu ya graviti ndani yake inaongezeka na atomi zake zinaanza kugusana. Halijoto inazidi hadi kufikia kiwango ambako [[mmenyuko mfululizo wa kinyuklia]] unaanza kutokea hadi kufikia [[mmeyungano nyuklia]] wa [[hidrojeni]] kugeukia [[heli]].

Kipindi cha mmeyungano nyuklia wa hidrojeni kinaendelea kwa miaka mabilioni hadi sehemu kubwa ya hidrojeni imekwisha. Hapa sehemu za nje ya nyota hupoa na kupanuka; halii hii huitwa [[pandikizi nyekundu]] (red giant) kwa sababu ya ukubwa na rangi yake. Mapandikizi mekundu kadhaa huonekana kwa macho tu angani yaking'aa kwa nuru nyekundu. Kama masi ya nyota bado ni kubwa mmeyungano nyuklia unaendelea kuzaa elementi nzito zaidi kwa sababu sehemu ya heli inaendelea kujibadilisha kuwa elementi za juu zaidi. Inaaminmiwa ya kwamba elementi zote ulimwenguni zilianzishwa ndani ya nyota.

Mwishowe kama masi haitoshi tena kuendeleza mmeyungano masi inaweza kujikaza; kutegemeana na ukubwa wa masi nyota inaweza kupasuka. Mabaki ya mlipuko huu yanakaa angani tu na mara nyingi huingia tena katika mwendo wa kuzaa nyota mpya; sehemu ndogo za masi hii huwa sayari.

Kama masi imejikaza sana [[shimo nyeusi]] ([[Kiingereza|Kiing.]]: ''black hole'') inatokea. Katika hali hii nguvu ya graviti ni kubwa mno inashika hata nuru yenyewe ambayo haiwezi kuoka nje tena.

like page yetu kwa habari zaidi

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets