Saturday, 18 April 2015
Jua ni nyota iliyopo karibu zaidi na sayari yetu ya Dunia kuliko nyota nyingine zote. Kuwa karibu na Dunia kumesababisha nuru au miale yake kuleta joto na mwanga katika uso wa dunia kuliko nyota nyingine tunazoziona.
Nyota hiyo ya Jua ipo umbali wa Kilometa Milioni 149.6 kutoka katika Sayari yetu ya Dunia. Pia zipo nyota nyingine angani ambazo ni kubwa kuliko Jua nyota hii na zina mwanga mkali kuliko ule wa Jua.
Uang’avu wa Jua unatokana na anuali za kemikali na mwanga wa Jua huweza kutufikia Duniani kwa njia ya mnunurisho kwa muda wa dakika 8 na nusu tuu, ambapo mwanga wa nyota nyingine huchukua muda wa miaka kadhaa kufika duniani.
Zaidi ya Jua kuna magimba mengine angani, Magimba haya ni Sayari, Asteroidi, na Mwezi.
Katika usiku mwang’avu usio na mawingu unaweza kuona vitu mbali mbali angani vikiwamo Mwezi na Nyota.
Nyota huwa ni ndogondogo na huonekana kama nukta zinazong`aa au kumweka, ambazo hutoa nuru za rangi Nyekundu,Njano au Bluu.
Pia wakati mwingine hasa wakati wa usiku,ukiangalia angani unaweza kuona nukta za nuru, ambazo huwa angavu, kubwa kwa umbo na hazimweki. Hizo huitwa Sayari.
Je nitazitambuaje Sayari Angani? au Nini tofauti kati ya Sayari na nyota?
Tofauti iliyopo ni kwamba, nyota humweka na nuru yake haitulii,wakati nuru ya Sayari imetulia na haimweki ,Nyota huonekana kama nukta za nuru angani na ziko mbali sana na Jua na Dunia, na pia Sayari hujongea angani toka sehemu moja hadi nyingine.
Sayari hulizunguka Jua kupitia kwenye njia maalumu inayoitwa Obiti au njia ya mzingo.
Hadi sasa Sayari zinazofahamika ni nane tu, nazo ni Zuhura,Zebaki, Dunia, Mirihi,Sumbula,Sarateni, Zohali,na Kausi
like page yetu kwa ufahamu zaidi
https://www.facebook.com/pages/Habari-Clan/597345927049107
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment