MOJA kati ya sayari nane mpya zilizo
nje ya mfumo wa jua (letu) imeonekana kuwa na mazingira kama dunia yetu.
Sayari hizo ambazo ziko umbali wa
miaka ya mianga 475 zimeonwa na darubini maalumu ya kuangalia mifumo ya nyota
mbali na nyota yetu, inayomilikiwa na Wamarekani ya Kepler.
Kwa Mujibu wa taarifa kutoka Shirika
la Anga za Juu la Marekani (NASA)
imesema sayari tatu zinafanana na dunia yetu kutokana na hesabu za
umbali kutoka katika jua (lao) lakini moja ndio inaonekana kuwa na mazingira yanayofanana na dunia na ina joto
la juu kidogo.
Taarifa hiyo ya wataalamu
wanaoangalia taarifa kuhusu sayari nyingine nje ya mfumo wa sayari yetu
zimetolewa katika mkutano wa wanajimu wa Marekani(American Astronomical
Society)
Sayari hizo 3 ambazo zimeingia
katika jedwali la Kepler zinafanya sayari zinazoonekana kufaa kama dunia yetu
kuwa nane.
Wataalamu wamesema kwamba moja ya sayari inayotambulika kama Kepler
438b,yumkini ni karibu sawa na dunia yetu tunayoishi kuliko sayari nyingine ya
Kepler 186f .
Ikiwa ni kubwa kwa asilimia
takaribani 12, sayari hiyo mpya ni kubwa
kuliko 186f lakini iko karibu sana na joto la dunia yetu ikipata asilimia 40 ya
joto kutoka katika jua lake kuliko sisi.
Maana yake ni kuwa kama tutasimama
katika uso wa sayari 438b tutajisikia joto zaidi kuliko hapa duniani, kwa
mujibu wa Dk Doug Caldwell kutoka taasisi ya Seti (Search for Extra-Terrestrial
Intelligence) ya California.
"Na kwa kuwa karibu na nyota
yake anga lake litaonekana jekundu
kuliko la kwetu," anasema Dk Caldwell .
Kuonekana kwa sayari hizo nyingine kunafanya idadi kamili ya sayari zinazoweza kuwa na uhai kama
yetu kuwa nane.
Pamoja na sayari hizo kuonekana ni
ngumu sana kwa mwanadamu kufika huko kutokana na ukweli kuwa zipo umbali wa
miaka ya miaka 475 na kwamba haijajulikana ni aina gani ya madini zimetengeneza
sayari hizo.
Picha zilizoletwa na darubini ya
Kepler ambayo iko nyuma ya dunia ikichungulia ndani ya anga wakati, dunia
inazunguka jua, inatumika kutambua sayari hizo kwa kutumia mfumo wa kuangalia
kile kinachoitwa kisayansi "transits".
Hii inamaananisha kuona mwanga nyota
unaominywa wakati sayari inapita mbele yake.
Darubini ya kepler iliyotupwa hewani
mwaka 2009 kwa lengo la kuytafuta sayari zinazofanana na dunia yetu mwaka jana
pekee ilileta taarifa za uwapo wa sayari ambazo kitaalamu wanaziita, exoplanets,
715
Ili kuthibitisha kwamba hizo ni
sayari zinazofanana na yetu au la wataalamu hutumia takwimu za ziada kutoka
katika darubini zinazoangalia dunia kwa lengo la kuzijua vyema sayari hizo.
Miongoni mwa mambo wanayofanya ni
kuona sayari hizo zina ukubwa gani na ziko mbali kutoka katika jua la mzingo
wao kwa kiasi gani.
Imeelezwa si kila kitu
kinachozunguka nyota huwa ni sayari.
Takwimu zaidi zinaonesha kwamba
wataalamu wa NASA na wenzao wanakazi kubwa ya kuabngalia maumbo mengin zaidi ya
500 yaliyoletewa taarifa na Kepler.
Mtaalamu wa mambo ya anga za juu
Fergal Mullally amesema uchunguzi na utafiti ukiendeleza zaidi huenda sayari
hizo zikaonekana kwambna hazifanani na dunia.
Aidha alisema kuna kuweza kuwa na
mabadiliko kwa namna zinavyojiingiza kwa ndani au nje ya uwezekano wa kuwa na
maisha.
Ili kutambua kama sayari zinafaa
kuishi ni lazima wanasayansi waangalie umbali wa sayari hiyo kutoka katika jua
lake, umbali utakaowezesha kuwa na maji na wala si umbali unaofanya maji hayo
kuganda
Kazi ya kutambua uhai katika sayari
hiyo inafanyika kwa kuhisi zaidi kw akuchambua nyaraka mbalimbali na sheria za
kifizikia na kemikali
Kwa mujibu wa Dk Cardwell, ni sayari tatu tu mpya kati ya nane zinahisia
hizo na ni moja tu kati ya mbili
inaonekana kuwa na wajihi wa dunia tunayoishi sisi.
Hata hivyo amesema kwamba taarifa za
ndani zaidi ni ngumu kupatikana.
"Kutoka katika darubini ya
Kepler ,vipimo vyake na vipimo vingine tunavyovitumia hatujui kama sayari hizi
zina bahari na samaki na bara lenye miti," alisema Dk Caldwell wakati
akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
"Tunachojua sasa ni nishati
inayopoipkelewa kutoka katika nyota yao(jua).
"Kwa hiyo tunaweza kusema: Vyema,
zina ukubwa wa sayari yetu inaonekana ina miamba na nishati wanayopata ni sawa
na ya kwetu.
"Wakati tukijaza mapengo haya
ya taarifa, tunajifunza nini maana ya kuwa na dunia kama yetu kwa namna
nyingine."
Akizungumza katika tukio jingine,
Profesa Debra Fischer kutoka chuo kikuu cha Yale alisema anakumbuka mara ya
kwanza wanaona sayari hizo na mazungumzo ya wataalamu miongo miwili iliyopita.
"Nakumbuka wanajimu waliokuwa
na shaka sana kuhusu hilo," alisema.
"Tulijikuta tukisema labda
picha hiyo ni sawa na Star Trek.Nilijisikia
vibaya sana."
Prof Fischer amesema kwamba darubini
hiyo Kepler imeleta taarifa nyingi zenye heshima kubwa.
"Tunazungumzia sayari nje ya
sayari yetu na mfumo wetu na tunaweza
hilo kwa kutumia darubini yenye nguvu kubwa.
"Na tunaweza kuchora grafu na
kutoa taswira na kufanya majadiliano ya kisayansi. Hili ni tukio la kushangaza
sana.
No comments:
Post a Comment