WATAFITI wa masuala ya anga wamesema kwamba ongezeko
la joto duniani linachangia ongezeko la
milipuko ya radi katika maeneo
mbalimbali duniani.
Katika taarifa yao ya utafiti huo
iliyochapishwa katika jarida la sayansi wamesema ongezeko hilo limechangia kuongezeka
kwa radi.
Utafiti huo uliofanywa kwa kuangalia
takwimu kutoka katika mtandao wa vizuia radi,timu ya wataalamu wameangalia kwa
udani ongezeko la joto na ongezeko la milipuko ya radi.
"Katika milipuko miwili ya radi
katika 2000, kutakuwa na milipuko mitatu kwenye 2100," anasema David
Romps, wa Chuo Kikuu cha California, Berkeley.
Pamoja na milipuko hiyo kuanzisha
mioto katika mbuga zilizokavu, milipuko hiyo hubadili kemia ya anga.
Kundi hilo la wataalamu pia
limebainisha njia mpya ya kuangalia uhusiano kati ya joto na milipuko ya radi,
kuw akukadiria joto lililopo linalowezesha kuwepo kwa mawingu ya radi.
"Huku joto la dunia
likiongezeka vichocheo hivi vya radi navyo vinaongezeka na radi
inapotengenezwa mlipuko wake utakuwa na
nguvu zaidi," anasema profesa
Romps.
Yeye na wataalamuw enzake wamepiga
hesabu kwamba kwa kila ongezeko la joto katika dunia 1C kutasababisha kuwepo na ongezeko la mkilipuko
kwa asilimia 12.
Walithaminisha takwimu zao kwa
kuangalia kwa kipindi cha mwaka mzima takwimu zilizokusanywa na Mtandao wa Vipinga Radi nchini Marekani (US
National Lightning Detector Network) ambavyo hunasa kila mrusho wa sumaku elektroniki,
unaosababishwa na milipuko ya radi nchini Marekani.
Alisema matokeo ya takwimu hizo ni
ya kusisimua sana kwani muda, mahali ya milipuko hiyo imerekodiwa kisahihi
kabisa na kutoa takwimu zilizo sahihi zinazoonesha mfadhaiko wa dunia katika
siku zijazo.
Ingawa nusu ya mioto katika mapori
ya Marekani husababishwa na milipuko ya radi, kila mlipuko una nguvu ya kutosha
kutengeneza mzunguko wa kikemikali na nitrogen oxides.
Radi
inatengenezwa vipi
Bado haijajulikana nini hasa
inasababisha radi, lakini wanasayansi wanaamini kwamba ili kuwepo na radi ni
lazima katika mada zake zote yaani
mvuke,kimiminika na barafu ni lazima yawepo.
Mawingu ni lazima yaumuke kwa haraka
kuwezesha kunyanyua kimiminika na barafu na
kuvining’iniza.
Wakati mabonge madogo ya barafu
yanagongana yuanasababisha uwapo wa electron ambazo zinasababisha kuwepo kwa
nishati, ambapo mabonge ya garafu yenye nishati hasi yakienda chini na zile
chanya zikienda katika mabonge madogo zaidi yaliyopo juu. Mwishoni wataalamu
wanasema kwamba ni lazima kuwepo na kutenganishwa kwa pande hizo mbili ambapo
nishati hasi inaporomoka kwa nguvu na kusababisha mwale wa radi.
Profesa Romps anasema kwamba chanzo
kikuu cha gesi ya nitrogen oxide katika troposphere ya kati na ya juu ni radi
Kuwepo kwa gesi hii kwa namna Fulani
inadhibiti gesi zinazotengeneza anga linalohami dunia ikiwamo ozone na methane.
Prof Romps anasema hali hiyo ni tukio kubwa kwa kile kitu
kinachoitwa kupanda kidogo kwa joto, lakini akasem,a kama joto la dunia
litapanda kwa 4c katuika karne ya 21 mabadiliko katika uwingi wa milipuko ya
radi itakuwa ndio msingi wa mashaka ya binadamu kwani itaenda kujaza hewa
zisizotakiwa.
Alisema kiasi kikubwa cha hewa ya
kaboni kinachotupwa katika anga katika karne hii kitakaa pale kwa miaka 100,000
No comments:
Post a Comment