JESHI
la Polisi mkoani Kagera, linawashikilia watu wawili wakituhumiwa
kufukua kaburi la marehemu Baltazar John mwenye ulemavu wa ngozi
(albino) na kuchukua viungo viungo vyake.
Watuhumiwa
hao ni Laston Faustine (41) mkazi wa Lukulaijo na January Korongo (43)
wakazi wa Kadengesho wilayani Karagwe mkoani Kagera, ambapo walikutwa na
mifupa mitatu ya binadamu.
Kamanda
Mwaibambe amesema “katika mahojiano mtuhumiwa wa kwanza- Faustine,
alituambia kuwa alipewa viungo hivyo na Korongo kwa ajili ya kuviuza Sh.
20 milioni.”
Ameongeza
kuwa, Korongo alipohojiwa amekiri kwamba alifukua kaburi la mjomba wake
aitwae Baltazari John (albino), ambaye alifariki mwaka 1991 na mwili
wake kufukuliwa 2009.
“Baada
ya kumuhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi
nyumbani kwake ambapo alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu
pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali ambayo ilikuwa imefungwa kwenye
mfuko nje ya nyumba yake.
“Ili
kujiridhisha, jeshi liliomba kibali cha mahakama wilayani Karagwe ili
kufukua kaburi hilo kuhakikisha kama kweli kuna mabaki ya mwili huo.
Tulipofukua hakuna kilichopatikana,” amesema kamanda.
No comments:
Post a Comment