Pages

Friday 3 April 2015

Je wajua Sayari 10 Zinazoweza kuwa na Maisha?

Mpaka kufikia Aprili 2014, kuna Sayari 21 nje ya mfumo wetu wa Jua, ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuwa na maisha ukiachana na Sayari yetu (Dunia).
Katika sayari hizi 21, zipo ambazo wanaSayansi hawana uhakika zaidi, kwani wanaendelea kuzisoma mazingira yake.
Ifuatayo ni orodha ya Sayari 10, ambazo mpaka sasa; zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na namna fulani ya maisha/ viumbe hai.

image
Kabla ya kuanza, ningependa kufanunua, maana ya ‘mwaka wa nuru’ (light year) kwa faida, kwa kuwa ntakuwa nikiitumia mara kwa mara katika makala hii…
Mwaka wa Nuru (Light Year):
Mwaka wa nuru ni kipimo si cha muda lakini cha umbali. Kinataja umbali unaopitiwa na nuru ikitembea kwa muda wa mwaka mmoja wa dunia yaani siku 365.
Msingi wa kipimo hiki ni kasi ya nuru ya kuwa nuru inatembea takriban kilomita 300,000 kwa sekunde. Idadi kamili ni mita 299,792,458 kwa sekunde moja. Mwezi wa dunia yetu una umbali na sisi kama sekunde moja ya nuru au kilomita lakhi tatu na dunia.
Katika mwaka mmoja umbali huo unafika mita 9.461 × 1015.
Kipimo hiki kinahitajika kutaja umbali kati ya nyota na nyota angani.
Sasa Tuanze:
10. Kepler-186fimage
Kepler-186f ni Sayari ambayo inafanana zaidi kiukubwa na Dunia kuliko zote ambazo zimepatikana. Sayari hii ipo umbali wa miaka ya nuru (light-years) 490 kutoka Duniani.

9. Gliese 581g
image
Sayari hii bado inakumbana na utata miongoni mwa wanaAstronomia mbalimbali. Iligundulika kwa mara ya kwanza, mwaka 2010. Pamoja na kwamba, bado kuna wanaSayansi wanaopata tabu kuihakikisha; Chuo cha Puerto Rico kilichopo Arecibo kinasema Gliese 581 g ni mhitimu wa kwanza kama tunatafuta viumbehai katika Sayari nyingine.
Sayari hii ipo umbali wa miaka ya nuru 20 kutoka Jua letu, na ina ukubwa mara tatu ya Dunia yetu. Sayari hii inazunguka nyota yake iitwayo Gliese 581 kila baada ya siku 30, na ipo katika Kundinyota (constellation) Libra.

8. Gliese 667Ccimage
Sayari ipo katika kundi la Sayari tuziitazo “Super-Earth”, kwani inaizidi kiukubwa Dunia yetu mara 4.5.
Ipo umbali wa miaka ya nuru 22 kutoka Duniani, na ipo kwenye Kundinyota Scorpius. Inazunguka nyota yake iitwayo GJ 667C ndani ya siku 28.

7. Kepler-22bimage
Kepler-22b ni kubwa kuliko Dunia mara 2.4. Inazunguka nyota ambayo inafanana kwa karibu na Jua letu kwa ukubwa na Joto.
Kepler-22b ipo umbali wa miaka ya nuru 600, kwenye Kundinyota Cygnus.

6. HD 40307gimage
HD 40307 g ni Sayari nyingine iliyo kwenye kategoria ya “Super-Earth”. Ipo umbali wa miaka 42 ya nuru katika Kundinyota Pictor…

5. HD 85512b
image

HD 85512b ilitangazwa mwaka 2011 ikiwa ni miongoni mwa Sayari 50 zilizogundulika kwa kutumia chombo cha HARPS (High Accuracy Radial Velocity Planet Searcher) kilichopo nchini Chile.
Sayari hii inaizidi kikubwa Dunia mara 3.6, na ipo umbali wa miaka 35 ya Nuru kwenye Kundinyota Vela.

4. Tau Ceti e
image

Sayari ya Tau Ceti e iligundilika Desemba, mwaka 2012.
Ipo kwenye Kategoria ya “Super-Earth”, ikiizidi Dunia kiukubwa mara 4.3. Sayari hii ipo umbali wa miaka 11.9 ya nuru.

3. Gliese 163c
image

Ukubwa wa Sayari hii, unafanya WanaSayansi wasiwe na uhakika ni Sayari ya aina gani. Inaizidi ukubwa Dunia mara 7, which means inaweza ikawa Sayari mwamba kubwa sana, au yaweza kuwa Sayari ya gesi kama Mshtarii (Jupiter).
Gliese 163c huzunguka nyota yake kila baada ya siku 26. Ipo umbali wa miaka 50 ya nuru kutoka sayari yetu, na ipo kwenye Kundinyota Dorado.

2. Gliese 581d
image

Sayari hii inaizidi kiukubwa Dunia mara 7 pia, na ipo umbali wa miaka 20 ya nuru.


1. Tauceti f
image

Tauceti f pia ipo kwenye Kategoria ya “Super Earth” kama sayari nyenzake Tauceti e.
Tauceti f inaizidi ukubwa Dunia mara 6.6…

(Na hizo ndizo Sayari 10 zinazoweza kuwa na maisha/viumbe hai… Nitoe Shukrani kwa ‘space.com’ kwa kunisaidia kupata taarifa hizi.)

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets