Na Anugrah Kumar
MAOFISA wa serikali nchini Marekani, wamekamata aina mbalimbali za nyoka
wapatao 50 waliokuwa wakihifadhiwa katika Kanisa la Tabernacle Church
of God la LaFollette, Tenn., na Mchungaji Andrew Hamblin, ambaye
amejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha “Wokovu wa Nyoka”
kinachorushwa katika kituo cha televisheni cha National Geographic,
anakabiliwa na kesi ya kukutwa na wanyama hatari kwa binadamu.
Mchungaji Hamblin akiwa ameshika nyoka 'albino' wakati wa ibada kanisani
"Mimi sitadanganya. Wameuliza kama (nyoka) walikuwa nyumbani kwangu,
nimesema hapana, lakini walipouliza kama wako kanisani, niliwaambia
ndiyo,” Mchungaji Humblin ameuambia mtandao wa WBIR.com.
Hamblin, ambaye kwa mara ya kwanza alionekana katika kipindi hicho
kinachojulikana kwa kimombo kama "Snake Salvation," mapema mwezi
Septemba, anaamini kuwa kanisa lake limelengwa na ‘kufuatwafuatwa’.
"Makanisa mengi siku hizi yanafichaficha mambo. Mimi sina cha kuficha."
Kushikilia majoka, kama ambavyo Mchungaji Hamblin amekuwa akifanya
katika ibada imepigwa marufuku katika eneo la Tennessee tangu mwaka
1947, na mchungaji huyo anatuhumiwa kukutwa na mnyamna hatari wa daraja
la kwanza, kwa mujibu waWBIR. Alitarajiwa kupandishwa katika mahakama ya
Campbell County leo Ijumaa Novemba 15.
Kitendo cha kufanya ibada kwa kutumia nyoka katika maeneo kadhaa nchini
Marekani imekuwa jambo la kawaida katika vikundi kadhaa vya Kipentekoste
vyenye wafuasi wapatao 1000 hivi. Hawa huamini kuwa wameagizwa na Yesu
Kristo katika Marko 16:15-18 na hasa mistari ya 17 na 18 katika Biblia
ya King James, kushika nyoka.
Imeripotiwa kuwa Hamblin amewahi kung’atwa na nyoka wakati wa ibada
kiasi cha mara tatu, lakini anadai kuwa kitendo cha kupandishwa kwake
kortini ni kuingilia uhuru wa kuabudu.
"Sitajali sana kutokana na kuchukuliwa kwa nyoka waliokuwa kanisani kwa
sababu nina uwezo wa kupata nyoka wengine wengi tu,” Mchungaji Hamblin
alisema. “ Kinachoniumiza ni kwamba, hapa sio sehemu ya biashara. Hapa
sio nyumbani. Ingekuwa ni nyumbani au sehemu ya biashara, sawa,
wangewachukua (nyoka). Lakini hapa ni sehemu ya kuabudu”.
Hamblin pia alisema anawalisha vizuri nyoka wale, na kuna mashine ya joto kwa ajili yao wakati wa baridi kali.
"Ninaamini katika nguvu za Mungu… Lakini, sasa ninakabiliwa na kifungo
jela, ninakabiliwa na hali ambayo nitatenganishwa na mke wangu, watoto
wangu.Ninakabiliwa na hali ya kutupwa nje ya kanisa langu kwa sababu tu
nilienda porini kukamata nyoka na kuwaleta kanisani kwa ajili ya kufanya
huduma kama inavyosema kwamba tutashika nyoka,” alisema Mchungaji
Humblin.
Pamoja na hatua hiyo, Mchungaji Hamblin alisema kanisa lake litaendelea na huduma ya waumini kushika nyoka, hapo baadaye.
Kipindi cha televisheni cha "Snake Salvation" tangu kianze kurushwa
hewani kimekuwa kikiwachanganya Wakristo na watu wengine kwa ujumla.
LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment