“Simama kimya, uzifikiri [“uzizingatie,” “NW”] kazi za Mungu za ajabu.”—AYUBU 37:14.
1, 2. Ni uvumbuzi gani wa ajabu uliofanywa mwaka wa 1922, nao ulionwaje?
MWAKIOLOJIA mmoja
na mheshimiwa mmoja Mwingereza walikuwa wameshirikiana kwa miaka mingi
kutafuta hazina. Hatimaye, Novemba 26, 1922, katika makaburi ya mafarao
wa Misri kwenye Bonde maarufu la Wafalme, mwakiolojia Howard Carter na
Mheshimiwa Carnarvon walipata hazina hiyo—kaburi la Farao Tutankhamen.
Walitoboa shimo kwenye mlango uliokuwa umezibwa kabisa kisha Carter
akaingiza mshumaa na kuchungulia ndani.