Habari wakuu,
Baada ya jana ripoti kusomwa, Kama kawaida moja kwa moja kutoka bungeni
Dodoma tutajuzana hapa kupitia habari clan. Kwa wale wasio na uwezo
kufatilia moja kwa moja pia kwa wale wenye nafasi ya kufatilia lakini
wakapenda kuona mirejesho fursa ambayo haipo kwenye vyombo vingine vya
habari. Tuungane kwa pamoja katika ngwe ya leo kutoka Dodoma.
Friday, 28 November 2014
Wednesday, 26 November 2014
Maneno ya Wabunge Novemba 20 2014 bungeni kuhusiana na mamlaka za bunge na mahakama.
Kama
haukusikiliza ama kutazama Kikao cha Bunge Dodoma leo, moja ya masuala
yaliyotawala ni kuhusu Mamlaka ya Bunge na Mahakama, wa kwanza
kuzungumza alikuwa David Kafulila; “…
Naomba mwongozo kuhusiana na taarifa ya PAC kuhusiana na sakata la
ufisadi wa ESCROW kama italetwa ama haitaletwa na msingi wa swali lile
ulikuwa ukizingatia kwamba zimekuwepo taarifa za mkakati wa kuhakikisha
Mahakama inatumika kuhakikisha ripoti ile hailetwi Bungeni na kufikia
mwisho…”
Labels:
Kitaifa
Mapokezi ya Mbunge David Kafulila Bungeni leo Novemba 24 baada ya kufunga Ndoa
Siku ya Jumamosi Novemba 22 millardayo.com ilikupatia taarifa kuhusu Mbunge David Kafulila
kufunga Ndoa Kigoma, leo Novemba 24 kaingia ndani ya Jengo la Bunge
Dodoma na kupigiwa shangwe za mapokezi na Wabunge wa Bunge hilo wakati
kikao kikiwa kinaendelea.
Spika wa Bunge Anne Makinda alikuwa kwa kwanza kuzungumza wakati Wabunge wakimpigia makofi David Kafulila alipokuwa anaingia; “…
Bwana Harusi anaingia… Sasa Bibi Harusi yuko wapi mimi nilitegemea
anakuwa pale… Mchezo mbaya huo.. Haya asante nashukuru, hongera…“- Anne Makinda.
Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia January Makamba naye aliongea haya; “… Na mimi napenda kuchukua fursa ya kumpongeza Mheshimiwa David Kafulila kwa kuoa, karibu kwenye klabu yetu na hongera sana…'like page yetu hapa
Thursday, 20 November 2014
SWAGA ZILIKUWA ZAMANI BWANA, KUNA SWAGA SIKU HIZI?
Labels:
Vimbwanga
NALAANI MAPEPO YOTE YA ATM
LIKE PAGE YETU HAPA
Labels:
Vimbwanga
TATIZO LILITOKEA MIAKA KUMI ILIYOPITA
Jamaa alivunjika mguu akaepelekwa hospitali;
DAKTARI: Imekuwaje mpaka ukavunjika mguu?
JAMAA: Miaka kumi iliyopita…
DAKTARI: Staki kujua hayo nataka kujua umevunjikaje mguu?
JAMAA: Dokta nisikilize kwanza, miaka kumi iliyopita nilikuwa nafanya kazi kwa bosi moja kule Uzunguni, siku moja binti yake mzuri sana akaja chumbani kwangu na kuniuliza kama nahitaji kitu chochote, nikamjibu sitaki, akarudia tena tena na kuniuliza tena kama sihitaji kitu chochote, mimi nikasema sihitaji kitu, akaondoka anacheka.
DAKTARI: Sasa hiyo inauhusiano gani na kuvunjika mguu?
JAMAA:Sasa leo nilipokuwa niko juu ya mnazi nagema, si ndio jibu likanijia kwanini yule mrembo alikuwa ananiuliza lile swali, ndio bahati mbaya nikajisahau nikaanguka na kuvunjika mguu
like page yetu kwa vichekesho zaidi
Labels:
Vimbwanga
Subscribe to:
Posts (Atom)