Pages

Tuesday 30 December 2014

Jamaa mmoja alienda kuposa kwa mzee mmoja

Mzee: Yaani wewe umekuja kuposa huku unatafuna big G? Si dharau hiyo!  
Jamaa: Natoa harufu ya sigara.  
Mzee: Unasemaje? Unavuta sigara pia!?  
Jamaa: Nikitoka klabu kulewa ndo huwa navuta. Mzee: Tobaa! Unalewa!?  
Jamaa: Nilianza kulewa nilipokuwa jela.  
Mzee: Yaani na kufungwa pia umeshawahi!?  
Jamaa: Ah si niliua mtu.
Mzee: Duh kumbe wewe muuaji!? Astaghafillulah. Jamaa: Si kuna mzee mmoja bwege nilitaka kumposa mwanae akanikatalia, mimi nikamuulia mbali.
Mzee: Karibu baba, unataka harusi lini? Mimi sina tabu, mke tu umepata! Mkeo huyu hapa baba! 

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets