Pages

Friday 3 April 2015

Vyombo vinavyoongozwa kwa fahamu zetu tu

Katika miaka ya hivi karibuni, tumeona teknolojia ikikua kwa kasi ya ajabu mno.
Mambo ambayo hapo nyuma yalionekana kama ndoto au stori tu, sasa yameweza kufanywa kuwa Halisia.Na bado teknolojia hii yaendelea kukua kila iitwapo leo.
Leo ningependa kuongelea teknolojia ambayo inamuwezesha mtu kukiongoza (ku-control) kifaa fulani kwa kufikiri/kwa mawazo tu.
Ni kitu ambacho wengi hukiona kwenye movie tu (haswa kwa wale wenzangu na mimi ambao hupenda movie na tamthilia za Sci-Fi). 
image

Kwa sasa, teknolojia hii, si stori tena; kwani inazidi kuboreshwa kila siku…
Game za Computer (Computer Games):Hakuna sekta katika teknolojia hii ambayo inaenda kwa kasi, kama sekta ya ma-game ya computer. Wameichukua teknolojia hii, na kuindeleza mno…Kwa mfano: Kampuni moja iitwayo “NeuroSky" iliyopo San Jose, Marekani imetengeneza kifaa kiitwacho "MindWave Mobile Headset" chenye sensor katika kipaji cha uso, ambacho kinasikiliza na kutambua signal kutoka kwenye Ubongo wa mtu.
Kifaa hichi huchukua “EEG Signals" hizi kutoka kwenye Ubongo na hupeleka taarifa kwa kutumia bluetooth kwenye game, ikimuwezesha mchezaji ku-control vitu kadhaa kwenye game kwa kuvifikiria tu…
image
Ma-game kadhaa yameshetengenezwa maalumu kwa kutumia teknolojia hii, na pengine huko mbele ndivyo ambavyo tutakuwa tukicheza ma-game yetu ya computer, siyo kwa vidole tena, bali kwa fahamu zetu tu!

Viti vya walemavu vinavyoongozwa na mawazo ya aliyekikalia:Nyuma kidogo (mwaka 2009), wanaSayansi kutoka chuo cha South Florida, walitengeneza kiti cha walemavu wa miguu, ambacho kinaweza kutembea chenyewe, kugeuka kushota, kulia na hata kurudi nyuma kwa kuongozwa na fahamu tu za mtu aliyekikalia.
Kiti hicho kiliambatana na Kofia iiyounganishwa na nyaya za electrode zinazodaka mawimbi ya P-300 kutoka kwenye Ubongo, na kubadilisha mawimbi hiyo ili kuongoza kifaa mechanical.
Kiti hicho, kilichopewa jina “smart wheelchair" kinampa uwezo mtu aliyekikalia kukiongoza kwa ukamilifu, bila kuhitaji msaada wowote…
Toyota waliichukua teknolojia hiyo na kuiboresha zaidi… Nadhani, kwa sasa watakuwa wameshaanza kuviuza viti hivyo kabisa.
image
Mkono wa Kibioniki unaongozwa na fahamu tu:
(waweza soma zaidi kuhusu hili, katika moja ya nakala nilizoandika hapo nyuma)
Samsung, na tablet zinazoongozwa kwa Fahamu:Samsung nao hawajataka kuachwa nyuma kabisa, kwani nao wameshatangaza kwamba wanaifanyia kazi teknolojia inayomuwezesha mtu ku-control “Galaxy Note 10.1” kwa kutumia ufahamu wake tu.
Bado kuna muda mrefu mpaka waweze kuifanya teknolojia hii kutumiaka na watu wote. Bado ipo kwenye utafiti zaidi, na kwa sasa inamlazimu mtumiaji kuvaa li-kofia lenye sensor za signal kutoka kwenye Ubongo.
image
 Yote haya yanaonyesha namna teknolojia inazidi kukua kwa kasi ya ajabu. Na, mimi na wewe twaweza imagine tu, namna teknolojia itavyokuwa miaka kumi tu ijayo. I’m so Proud!
like page yetu kwa habari zaidi

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets