Pages

Monday 24 August 2015

Mwezi (gimba la angani)


Chombo cha angani Galileo ilipiga picha hii ya Ardhi na mwezi
Picha maarufu sana ya dunia yetu iliyopigwa na mwanaanga Mmarekani Bill Anders wakati wa ujumbe wa Apollo 8 tarehe 24 Desemba 1968. Apollo 8 ilikuwa mara ya kwanza chombo cha angani cha kubebea watu kushikwa na graviti ya mwezi na kuzunguka mwezi kwa ajili ya graviti hiyo.

Mwezi ni gimba la angani linalozunguka sayari.

Yaliyomo

Miezi ya sayari

Sayari inaweza kuwa bila mwezi au na miezi mingi. Dunia yetu ina mwezi moja tu. Mshtarii ina miezi zaidi ya 60, mingine mikubwa kama sayari ndogo mingine midogo yenye kipenyo cha 1 km tu. Utaridi haina mwezi.
Mwezi hauna nuru mwenyewe bali kunang'aa jwake kunatokana na nuru ya jua inaoakisiwa usoni mwake kama kwenye kioo.
Sayari yenye miezi katika mfumo wa jua:
Sayari zisizo na miezi katika mfumo wa jua:
Mwendo wa mwezi

Mwezi wa Dunia (ardhi) yetu

Mwezi wa dunia yetu ni mkubwa kushinda miezi mingine katika mfumo wa jua. Hakuna jina tofauti kuliko "mwezi" isipokuwa watu wametumia neno la Kilatini "luna" kwa ajili ya mwezi wakitaja mwezi wetu ili kuutofautihsa na miezi ya sayari nyingine.
Huwa tunaangalia uso wake upande mmoja tene uleule tu. Sababu yake ni ya kwamba siku ya mwezi ni sawa na kipindi cha mwezi duniani. Mwezi unazunguka kwenye kipenyo chake katika muda wa siku 27.321 661 za dunia. Upande wa nyuma wa mwezi uko gizani wakati sisi tunaona mwezi mpevu. Wakati kwetu mwezi hauonekani upande wa nyuma unapokea nuru ya jua.
Uso wa mwezi unajaa mashimo ya kasoko yaliyosababishwa kwa kugongwa na meteoridi. Mwezi hauna angahewa inayozuia mapigo ya meteoridi ndogo au kupunguzu nguvu yao jinsi ilivyo duniani.
Picha inayoonyesha umbali baina ya dunia na mwezi kulingana na ukubwa wao. Umbali wa wastani baina ya mwezi na dunia ni kilomita 384,400. Mwezi wetu una upana wa kilomita 3,470. Dunia yetu ina upana wa kilomita 12,800 [1].

Mwezi (wakati) kama kipimo cha wakati

Awamu za mwezi kuanzia mwezi mwandamu kupitia robo ya kwanza, nusu mwezi, mwezi mpevu, robo ya tatu hadi mwezi mwandamu tena
Uso wa mwezi jinsi unavyoonekana duniani hubadilikabadilika. Mwezi mpevu unaonekana kama duara kamili la kung'aa lakini baada ya kuonekana hivi umbo lapungua kila siku hadi kutoonekana kabisa na hali hii huitwa mwezi mwandamu. Baadaye mwezi unaonekana tena kama hilali nyembamba na kuongezeka hadi kuwa duara tena. Muda wa mabadiliko yote kupit mara 1 ni siku 29 1/4.
Muda wa mabadiliko kati ya mwezi mwandamu hadi kupotea na kuwa mwezi mwandamu tena ni kati ya siku 28 - 29. Kipindi hiki kinakumbukwa kirahisi, kinatazamiwa na watu wote wakati uleule kwa hiyo pamoja na kipindi cha siku kilikuwa kati ya vipimo vya kwanza vya wakati kwa binadamu.
Awamu za mwezi zilikuwa vipindi vya kuhesabu wakati tangu mwanzo wa kalenda. Hadi leo kuna kalenda ya mwezi ndiyo kalenda ya Kiislamu inayopanga wakati kutokana na hali halisi ya awamu za mwezi.

Safari kwenda mwezini

Nyayo za mwanaanga Edwin Aldrin mwezini <br />(Apollo 11)
Mwezi wetu ni gimba la anga la kwanza ambako wanadamamu wamefika. Tarehe 21 Julai 1969 mwanaanga Mwamerika Neil Armstrong alikuwa mtu wa kwanza wa kukanyaga uso wa mwezi. Waamerika 11 walimfuata katika miaka hadi mwaka 1972. Baadaye safari za kwenda mwezini hazikufanywa tena kutokana na gharama kubwa.

Mwezi mali ya watu?

Hata kama Warusi na Waamerika walifikisha mabendera yao mwezini hakuna anayedai mali huko. Katika mkataba wa kimataifa kuhusu anga wa nje nchi 192 za dunia zimepatana ya kwamba mwezi utaangaliwa sawa na maeneo ya kimataifa ya bahari. Walipatana pia ya kwamba itakuwa marufuku kupeleka silaha kali kama kinyuklia angani. Mataifa mengi ya dunia yamejiunga na mkataba huo isipokuwa nchi chache hasa za Afrika hazikutia sahihi kama vile Tanzania.
Lakini kuna watu binafsi wanaodai mali ya mwezi. Kwanza kuna familia ya Jürgens wanaoishi Westerkappeln (Ujerumani) walipewa hati ya kumiliki mwezi na mfalme wa Prussia Friederich II. tarehe 15.07. 1756 BK. Mfalme alitoa hati kama zawadi ya shukrani kwa huduma bora akiamuru ya kwamba Martin Jürgens atakuwa mwenye mwezi na haki hii itarithiwa na mtoto wa kwanza.
Bila shaka ilhali hakujua haki za mali za Mjerumani katika mwaka 1980 Mwamerika Dennis M. Hope alifika mbele ya msajili wa viwanda mjini San Francisco akidai mwezi ni wake. Kufuatana na sheria ya Marekani kiwanda ni mali ya mtu akiandikisha dai lake na katika muda wa miaka minane hakuna upingamizi dhidi ya dai lake. Kwa njia hii -iliyowahi kufaulu tayari wakati wa karne zilizopita Wazungu walipojipata Amerika ya Kaskazini (hakuna aliyepinga madai yao mbele ya msajili)- alipata hati ya kumiliki akijaribu kuuza sasa mwezi polepole.

Vyanzo


  1. ["http://solarsystem.nasa.gov/planets/profile.cfm?Object=Moon" "NASA Solar System Exploration: Planets"]. NASA. Iliwekwa mnamo 2010-10-01.

Mfumo wa jua na sayari zake
Jua - Utaridi - Zuhura - Dunia (Mwezi) - Mirihi - Mshtarii - Zohali - Uranus - Neptun
Sun - Mercury - Venus - Earth (Moon) - Mars - Jupiter - Saturn - Uranus - Neptune

Science-symbol-2.svg


 like page yetu kwa habari zaidi                  

No comments:

Post a Comment

 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets