Uwanja huo una barabara ya kurukia ndege na kutua (Runway 15/33) moja yenye urefu wa futi 6,445 (1,964 m) urefu ambao unalingana na viwanja vya mpira wa miguu 21 vyenye urefu wa mita 120 (393.6 ft),moja kati ya barabara za ndege kurukia na kutua fupi sana duniani. Una jengo moja la abiria lenye check-in counters 4,geti moja la kuingilia kwenye ndege na jengo la mizigo.
KWA NINI NI HATARI ZAIDI?
Sababu za uwanja huo kuwa hatari zaidi duniani.
1. MILIMA MIREFU SANA ILIYOUZUNGUKA UWANJA. Uwanja huo umezungukwa na milima ya Himalayas yenye urefu wa zaidi ya futi 18,000 (5,487 m),urefu ambao unakaribia ule wa mlima Kilimanjaro. Hebu fikiria urefu wa mlima kilimanjaro,halafu piga picha sehemu iliyozungukwa na milima kama hiyo pande zote!
2.BARABARA FUPI YA KURUKIA NDEGE (RUNWAY). Barabara yenye urefu wa futi 6,445 tu. Runway kwenye viwanja vingi vya ndege duniani zina urefu wa kuanzia futi 10,000 (3,048 m) hivi. Hilo linafanya ndege kubwa kutoweza kutua.
3.PEPO KALI ZINAZOVUMA KUTOKA KWENYE MTO.
Sehemu yoyote yenye vyanzo vya maji kama mito na maziwa,kunakuwa na pepo kali zinazovuma kuelekea nchi kavu. Uwanja huo wa ndege umepakana na mto uliotengenezwa na bonde la ufa la mto Paro Chhu. Unaweza kuona jinsi kunakuwa na upepo mkali eneo hilo.
Ni Mashirika machache sana ya ndege yanayoutumia uwanja huo. Baadhi yao ni Budha Air, Druk Air na Tashi Air. Ni marubani nane tu duniani mpaka sasa ambao wameruhusiwa kutua katika uwanja huo. Shughuli zote za uwanja huo hufanywa mchana wakati kuna mwanga,na hakuna ndege inaruhusiwa kutua usiku au kukiwa na hali mbaya ya hewa.
~Zaidi ya huo,kuna viwanja vingine hatari kama vile Kansai International airport,Princess Juliana International airport na Madeira Airport.
LIKE PAGE YETU KWA HUFAHAMU ZAIDI
No comments:
Post a Comment