Simba,
Nyati, Faru, Chatu....haya ndiyo majina ya wanyama yanayoweza kukujia
akilini pindi ukiulizwa MNYAMA YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU. Well,
amini usiamini, kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa
akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu. Na udogo wake si
katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na
mbwa, paka au mbuzi, achilia mbali wababe kama Simba, Chui au Faru.
Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.
Kwa mujibu wa takwimu, Mbu ni kiumbe
hatari zaidi kuliko wote duniani. Kiumbe huyo hatari ni maarufu kwa
kuambukiza rundo la magonjwa, kubwa zaidi ikiwa ni homa ya malaria.
Lakini pia mbu hueneza homa ya matende (elephantiasis), homa ya manjano
(yellow fever), kindiga popo (dengue fever) na homa ya Mto Nile.
KESI DHIDI YAKE: Mbu anawajibika kusababisha kati ya vifo milioni 2 hadi 3 kwa mwaka.
VIJIWE (Hangout) VYAO: Takriban dunia nzima lakini zaidi barani Afrika, Asia na Amerika ya Kaskazini.
ANAVYOSABABISHA MAAFA: Mbu huambukiza
maradhi ya kuuma kwenye ngozi ya binadamu na kumwaga mate yake yenye
vijidudu vinavyosababisha homa husika. Ukiweka kando vipele vidogo
vinavyotokea mahala alipouma mbu, anayeambukizwa na mbu hatambua
maambukizo hadi pale kinga za mwili inaposhtuka (na kuleta dalili
mbalimbali).
JINSI YA KUMKWEPA: Njia ya kupambana
na mbu na maambukizo ni pamoja na kutumia chandarua kilichomwagiwa
kinga, kuangamiza sehemu za mazalio ya mbu na vidonge vya kinga.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nyoka Wenye Sumu Kali
Japo kuna zaidi ya aina 2,000 za nyoka, 450 kati yao wenye sumu,ni aina 250 tu kati yao ndio wenye uwezo wa kuua binadamu.
KESI DHIDI YAO: Nyoka wenye sumu kali husababisha kati ya vifo 50,000 na 250,000 kwa mwaka.
VIJIWE VYAO: Zaidi ni Afrika,Asia na Amerika ya Kaskazini
WANAVYOSABABISHA MAAFA: Nyoka wana
kasi sana na sehemu yoyote katika mwili wa binadamu inaweza kuwa
kugongwa na kiumbe huyo hatari.Lakini ni hatari zaidi nyoka anapomgonga
mtu kwenye mshipa wa damu kwani hiyo huharakisha kusambaa kwa sumu ya
kiumbe huyo.Nyoka hutumia sumu yao kumlegeza mtu na pengine kumpotezea
fahamu.Majoka makubwa kama Mfalme Kobra (King Cobra) yanaweza kusimama
hadi usawa wa kichwa cha binadamu,huku wengine wakiweza kutema na
kurusha sumu yao kutoka mbali kwenda kwenye macho ya mwanadamu.
JINSI YA KUWAKWEPA: Mara nyingi nyingi
nyoka hushambulia pale tu pale anapobughudhiwa.Kwahiyo ushauri muhimu
wa kuepuka shambulizi kutoka kwa viumbe hao ni kujiepusha nao (Stay
away!).Pia ni muhimu kuvaa mabuti kwenye mazingira yanayoweza kuwa na
nyoka.Epuka mapori yanayoweza kuwa makazi ya nyoka.Na ikitokea umeomwona
nyoka,inashauriwa urudi kinyumenyume taratibu kwani anaweza kujirusha
mara nusu ya urefu wake,na mtikisiko kidogo tu unaweza kumasha hasira za
kiumbe huyo hatari.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Nge
Ni kiumbe hatari mwenye sura mbaya
maradufu.Inaaminika kuwa ng'e anaweza kuwa anasababisha vifo vingi zaidi
ya vile vinavyorekodiwa rasmi,sababu ya kuhisi hivyo ikiwa ni mazingira
wanayoishi viumbe hao na ugumu wa kupatikana tiba dhidi ya sumu
yao.Hata hivyo,japo kuna aina tofauti 1500 za ng'e ni 25 tu kati yao
ambao ni hatari kwa uhai wa uhai wa binadamu.
KESI DHIDI YAO: Ng'e husababisha kati ya vifo 800 hadi 2,00 kwa mwaka
VIJIWE VYAO: Duniani kote hususan Afrika,America ya Kusini na Kaskazini na Asia ya Kati.
WANAVYOSABABISHA MAAFA: Ng'e humlegeza
binadamu baada ya kumdunga sumu kwa kutumia "vijisindano" vilivyopo
kwenye mikia yao.Kama ilivyo kwa sumu nyingine za
wadudu/wanyama,binadamu walio hatarini zaidi ni wale wenye aleji,japo
ng'e wengi wenye sumu wanaopatikana Afrika wanaweza kumdhuru mtu yeyote
yule.
JINSI YA KUWAKWEPA: Ng'e huwa active
zaidi nyakati za usiku na hupendelea kujipumzika mchana.Kwahiyo ni
muhimu kuhakikisha sehemu ya kujilaza ipo salama kabla ya kuubwaga
mwili.Kadhalika ni muhimu kupunga mavazi na/au soksi kuhakikisha hakuna
ng'e humo,vinginevyo itakuwa balaa.
-----------------------------------------------------------------------------------like page yeu kwa habari zaidi
No comments:
Post a Comment