Pages

Saturday, 29 August 2015

JE wajua kiumbe anayeishi mda mfupi kuliko wote duniani

Kiumbe Anayeishi Muda Mfupi Kuliko Wote Duniani anaitwa Nzi (Adult mayfly) ambaye anaishi siku 1 mpaka 3 tu
like page yetu kwa habari zaidi

Friday, 28 August 2015

Je Wajua Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani?

Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani ni Kiboko.
Kiboko ndiye mpaka sasa hivi anayeongoza duniani kwa kuwa na mdomo mkubwa. Pia anaongoza kwa kupanua mdomo anapopiga miayo. Mdomo wake unaweza kupanuka mpaka digrii 170 ambayo ni sawa na mstari ulionyooka ukipungua kwa digrii kumi (10) tu.

Je wajua treni iliyofishwa uku imesheheni dhahabu tangu vita ya pili ya dunia yapatikana?

 
Afisa mmoja wa serikali ya Poland, amesema kuwa ana imani kuwa treni moja ya kijeshi ambayo imefichwa tangu vita vya pili vya dunia, zaidi ya miaka sababini iliyopita, na kusemekana kubeba vitu vya dhamani, imepatikana, chini ya ardhi Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

VIUMBE HAWA 10 NDIVYO WANAOVUNJA REKODI DUNIANI.

DUMA.

Hakuna anayekimbia kwa kasi zaidi yake: duma wanaweza kufikia kasi ya hadi kilomita 120 kwa saa. Ni jambo linaloendana na mazowea yao ya kuwinda. Wanyama hao huwinda mchana, ambapo wanamnyemelea mnyama mwingine na kisha kukimbia kwa kasi na kumkamata kwa kushtukiza. Hata hivyo hawawezi kukimbia kwa muda mrefu na hivyo wasipomkamata swala baada ya mita kama mia moja wanakata tamaa.

VIUMBE WA AJABU WAISHIO ANGANI!

MPENZI msomaji ungana nami katika simulizi hii mpya ya kweli inayohusu viumbe wa ajabu waishio angani. Kama ni msomaji wa vitabu vitakatifu, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Inahisiwa kuwa visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.
Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizizopita wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).
Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.
Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknolojia kuliko binadamu, tatizo tu hawavai nguo!

MAAJABU YA DUNIA NCHINI JAMAICA : MOTO UNAOWAKA WENYEWE KWENYE MAJI BILA KUZIMIKA.


Monday, 24 August 2015

UWANJA WA NDEGE HATARI ZAIDI KUTUA DUNIANI!

    Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Paro (IATA:PBH, ICAO:VQPR) ulio nchini Bhutan katika milima ya Himalayas,ndiyo uwanja unaofikiriwa kuwa uwanja hatari zaidi duniani kwa ndege kutua na kuruka. Uwanja huo,upo kilomita 6 hivi toka mji wa Paro kwenye bonde la ufa la mto Paro Chhu.
    Uwanja huo una barabara ya kurukia ndege na kutua (Runway 15/33) moja yenye urefu wa futi 6,445 (1,964 m) urefu ambao unalingana na viwanja vya mpira wa miguu 21 vyenye urefu wa mita 120 (393.6 ft),moja kati ya barabara za ndege kurukia na kutua fupi sana duniani. Una jengo moja la abiria lenye check-in counters 4,geti moja la kuingilia kwenye ndege na jengo la mizigo.

Mwezi (gimba la angani)


Chombo cha angani Galileo ilipiga picha hii ya Ardhi na mwezi

Sunday, 23 August 2015

Sakafu ya Bahari Siri Zake Zafunuliwa


TWAHITAJI kuelewa kindani kidogo jinsi ambavyo dunia imeumbwa ili tuweze kuelewa mambo yaliyoonwa na watafiti waliokuwa kwenye chombo cha Alvin. Yaaminika kuwa dunia yetu imefanyizwa na tabaka thabiti (linaloitwa lithosphere) linalokalia mwamba ulioyeyuka, unaosogea polepole. Kwa wazi, tabaka thabiti la nje lina kina cha takriban kilometa 100 nalo hufanyiza asilimia 0.6 hivi tu ya dunia yote. Tabaka la nje kabisa, si laini, ni nene mno chini ya mabara na jembamba kiasi cha kilometa sita chini ya safu ya milima iliyo katikati ya bahari.

Ulimwengu Uliojaa Maajabu

MIAKA 100 hivi iliyopita, wanasayansi waliamini kwamba ulimwengu mzima unapatikana katika kikundi chetu cha nyota cha Kilimia. Hata hivyo, kwa sababu ya maendeleo makubwa ya astronomia, fizikia, na tekinolojia katika karne ya 20 wanasayansi wamegundua ukubwa halisi wa ulimwengu. Baadhi ya mambo ambayo wamegundua yamewanyenyekeza. Kwa mfano, katika miaka ya hivi karibuni wataalamu wa kuchunguza nyota wamegundua kwamba hawajui kile kinachofanyiza zaidi ya asilimia 90 ya ulimwengu. Isitoshe, ugunduzi ambao umewafanya wafikie mkataa huo umewaacha wanasayansi wakijiuliza ikiwa kweli wanaelewa kanuni za msingi za fizikia. Maswali kama hayo si mageni.

Friday, 21 August 2015

Viumbe Hatari Kabisa Duniani, Anayeshika Namba Moja Ni Mbu!



Simba, Nyati, Faru, Chatu....haya ndiyo majina ya wanyama yanayoweza kukujia akilini pindi ukiulizwa MNYAMA YUPI NI HATARI ZAIDI KWA MWANADAMU. Well, amini usiamini, kiumbe hatari zaidi ni mdogo mara elfu kadhaa akilinganishwa kiumbo na hao majabali tunaowafahamu. Na udogo wake si katika umbile pekee bali pia hata sauti yake ni ndogo kulinganisha na mbwa, paka au mbuzi, achilia mbali wababe kama Simba, Chui au Faru. Kiumbe huyo hatari wa kuogopwa kwa gharama yoyote ile ni MBU.

Viumbe wa ajabu wa baharini








WATU wengi wanadhani kuwa utafiti kuhusiana na wanyama umekamilika. Lakini ukweli ni kuwa bado kuna maswali mengi sana kuhusiana na maisha ya wanyama mbalimbali ambayo hayajapatiwa majibu.
Ndio maana kila kukicha unajitokeza ugunduzi mwingine mpya ambao mara nyingi unawaacha watafiti vinywa wazi lakini baadaye unatoa mwanga wa masuala kadhaa waliyokuwa hawayaelewi awali.
Mathalani, tunafahamu visa kadhaa vya watoto kuzaliwa wakiwa wameungana. Lakini hivi karibuni watafiti wa huko Mexico walimgundua nyangumi wa kijivu walioungana.
 

Blogger news

Blogroll

LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZA KILA WAKATI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets