WATAFITI wa masuala ya anga wamesema kwamba ongezeko
la joto duniani linachangia ongezeko la
milipuko ya radi katika maeneo
mbalimbali duniani.
Katika taarifa yao ya utafiti huo
iliyochapishwa katika jarida la sayansi wamesema ongezeko hilo limechangia kuongezeka
kwa radi.
Utafiti huo uliofanywa kwa kuangalia
takwimu kutoka katika mtandao wa vizuia radi,timu ya wataalamu wameangalia kwa
udani ongezeko la joto na ongezeko la milipuko ya radi.
"Katika milipuko miwili ya radi
katika 2000, kutakuwa na milipuko mitatu kwenye 2100," anasema David
Romps, wa Chuo Kikuu cha California, Berkeley.
Pamoja na milipuko hiyo kuanzisha
mioto katika mbuga zilizokavu, milipuko hiyo hubadili kemia ya anga.
Kundi hilo la wataalamu pia
limebainisha njia mpya ya kuangalia uhusiano kati ya joto na milipuko ya radi,
kuw akukadiria joto lililopo linalowezesha kuwepo kwa mawingu ya radi.
"Huku joto la dunia
likiongezeka vichocheo hivi vya radi navyo vinaongezeka na radi
inapotengenezwa mlipuko wake utakuwa na
nguvu zaidi," anasema profesa
Romps.
Yeye na wataalamuw enzake wamepiga
hesabu kwamba kwa kila ongezeko la joto katika dunia 1C kutasababisha kuwepo na ongezeko la mkilipuko
kwa asilimia 12.
Walithaminisha takwimu zao kwa
kuangalia kwa kipindi cha mwaka mzima takwimu zilizokusanywa na Mtandao wa Vipinga Radi nchini Marekani (US
National Lightning Detector Network) ambavyo hunasa kila mrusho wa sumaku elektroniki,
unaosababishwa na milipuko ya radi nchini Marekani.
Alisema matokeo ya takwimu hizo ni
ya kusisimua sana kwani muda, mahali ya milipuko hiyo imerekodiwa kisahihi
kabisa na kutoa takwimu zilizo sahihi zinazoonesha mfadhaiko wa dunia katika
siku zijazo.
Ingawa nusu ya mioto katika mapori
ya Marekani husababishwa na milipuko ya radi, kila mlipuko una nguvu ya kutosha
kutengeneza mzunguko wa kikemikali na nitrogen oxides.
Radi
inatengenezwa vipi